Wabunge wanaposhangilia Posho Mpya za Madiwani...!

Wabunge DHAIFU hawana habari kuwa Madaktari wamegoma kwa kuitaka serikali iboreshe malipo yao na vitendea kazi, na Serikali imesema haina hela za kuwalipa Madaktari ila inazo za kuwalipa Madiwani na wabunge 2 Wanasiasa Tanzania ni Bora kuliko fani nyingine yoyote, Acha tufe hatuna serikali inayojali wananchi wake
 
Nyahende,
Hakuna posho au mshahara utakaomtosha diwani aache kuomba kwa mkurugenzi wa Halmashauri. Wabunge wana mishahara na posho nyingi sana. Wameacha kuomba? Wameacha kuchukua bahasha za khaki kwenye taasisi zetu za umma? Mawaziri wana mishahara na posho kubwa sana lakini angalia wanavyozitafuna taasisi zilizo chini ya wizara zao. Kwa nini tunageuza nafasi za KISIASA kuwa vitega uchumi? Kwa nini tunageuza nafasi za kisiasa kuwa AJIRA? Fedha ambazo zingewanufaisha WATANZANIA kuboresha huduma za kijamii tunagharamia wanasiasa na siasa!

Mkuu WildCard hoja yako ina mantiki kubwa sana, na kimsingi ninakubaliana na wewe kwamba si jambo jema kwa ustawi wa nchi kuigharimia sana siasa kuliko miradi ya maendeleo ya nchi.

Lakini pia tukubaliane kwamba si watumishi wote wa umma wanao misuse public funds, si wabunge wote wanaovuta bahasha kwenye mashirika yetu, si mawaziri wote wanaoyafilisi mashirika yetu. Tukitumia hoja ya wachache kuboronga na kui-generalize itatufanya sasa tusiwalipe vizuri watumishi wote wa umma kwakuwa upo ushahidi wa wazi kwamba kumekuwa na ubadhirifu wa mali za umma kwa viwango tofauti tofauti vya uongozi na utawala.

Kwahiyo tunachotakiwa kufanya ni kuwalipa vizuri watumishi wote lakini kuwe na usimamizi makini, hasa viongozi wakuu wa nchi, kwani bila wao kuwa makini, waaminifu na wakali, ama wakiwa nao ni wadokozi basi hawatakuwa na uwezo wa kuwadhibiti ama kuwakemea wenzao wakiiba.

Tukikubaliana kwamba tuache kuwalipa vizuri basi tutakuwa tumekubali kukosa kabisa maendeleo hata hayo madogo tunayoyaona. Mimi binafsi siamini kwamba kuwaongezea posho madiwani kutaifanya nchi hii ishindwe kuwekeza vya kutosha katika shughuli za maendeleo, kwani siamini kwamba posho za madiwani kwa mwaka zinaweza kufikia sh.100bilioni!!, kwahiyo kiwango hicho hakiwezi kutukwamisha kujiletea maendeleo.

Fikiria mabilioni yaliyoliwa katika halmashauri mbalimbali na taasisi mbalimbali, kama fedha hizo zingesimamiwa vizuri nina uhakika zingetusaidia kutatua matatizo mengi ya kijamii, lakini kwa sababu ya watendaji wachache fedha zikaliwa na hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.
 
Last edited by a moderator:
Nasikitika sikubaliani nawe kabisa. Mbona Wabunge na Mawaziri wanalipwa vizuri sana lakini mipango ya maendeleo inelekea kukwama. Tutafute sababu za msingi kwa nini mambo yetu yanakwama karibu kila kona.

Katika hili jibu langu ni jepesi kabisa,
Kama nchi tumekosa usimamizi imara kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali.
Kama raisi angekuwa imara, bila shaka wasaidizi wake nao wangekuwa imara kusimamia fedha za umma.

Kama mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wahasibu na viongozi wengine wengi katika ngazi mbalimbali wanalipwa vizuri lakini baadhi yao bado wanadokoa, hiyo haimaanishi kwamba tuache kuwalipa vizuri kwakuwa wanatuibia, kinachotakiwa ni kuweka mfumo mzuri utakaotuwezesha kuwadhibiti wabadhirifu wote kwani hakuna nchi yeyote duniani isiyokuwa na watumishi wachache wabadhirifu lakini kwakuwa wana mifumo mizuri, basi inakuwa rahisi kwao kuepusha ubadhirifu na hata kuwabaini na kuwachukulia hatua. Hapa kwetu wezi wanapigiwa makofi ya pongezi na huenda ndio sababu kila mmoja kaamua kuwa mkwapuaji.

Nadhani tusiwaonee madiwani peke yao, kama ni suala la usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi pamoja na tatizo la kupokea rushwa tunapaswa kujitazama upya mfumo wetu mzima, badala ya kuwatolea macho tu madiwani peke yao.
 
kilichobaki ni sisi watanzania bila ya kujali itikadi zenu na vyama vyetu kusimama na kudai huduma bora na kuwatetea hawa madaktari kwa kuwa hawa ndio wanatutibu sisi ila wao wakiugua wanapelekwa india kwa matibabu .
Mkuu unamaanisha tuwatetee kupitia kwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wetu si ndio hivo, lakini cha ajabu huo mgomo
una siku ya tatu leo na sioni juhudi za wawakilishi wetu wabunge kuibana Serikali kulikoni!!.
 
Kwani hao madiwani sio madiwani wetu? au haujui kwamba madai ya mafao yao nalo ni jambo la msingi pia?
..Mafao kwa kazi ipi wanayofanya, mfano mdogo; Moja ya Kazi ya Diwani ni kuisimamia halmashauri ya Wilaya, una uhakika hawa wanasimamia kikamilifu hizo halmashauri??!, vinginevyo tusingekuwa na Ripoti chafu hizi za CAG kila mwaka za halmashauri nyingi. Kumbuka pia Mbunge ni Diwani
 
..Mafao kwa kazi ipi wanayofanya, mfano mdogo; Moja ya Kazi ya Diwani ni kuisimamia halmashauri ya Wilaya, una uhakika hawa wanasimamia kikamilifu hizo halmashauri??!, vinginevyo tusingekuwa na Ripoti chafu hizi za CAG kila mwaka za halmashauri nyingi. Kumbuka pia Mbunge ni Diwani
Hiyo ni issue ingine mkuu, au unataka tukueleze madudu ya makitari wetu nini?
 
Kwa hiyo hutaki madiwani waongezewe posho?
Nadhani na wewe ni Diwani. Fine Serikali imekubali kuwaongezea posho, lakini mnafanya nini kuwaondolea umasikini watanzania huko mnapowaongoza?. Hebu pima kati ya Posho na Uzalendo kwa nchi hii masikini...
 
Hiyo ni issue ingine mkuu, au unataka tukueleze madudu ya makitari wetu nini?
Ukizungumzia madudu, yapo kila idara ya serikali tena huko halmashauri ndo hakufai. Ninachofahamu Madaktari wanagoma kwa sababu yapo madai yao hayajatelezwa (Hayatekelezeki???) na Serikali. kama kuna mengine weka hapa tuyajadili
 
safi sana, madiwani walikuwa na hali ngumu sana iliyofanya waweze kununulika kirahisi na wakurugenzi pamoja na wasaka tenda
Hivi hizo posho zimeongezeka kiasi cha Madiwani kuacha kununulika?!!, sidhani.
 
Ukizungumzia madudu, yapo kila idara ya serikali tena huko halmashauri ndo hakufai. Ninachofahamu Madaktari wanagoma kwa sababu yapo madai yao hayajatelezwa (Hayatekelezeki???) na Serikali. kama kuna mengine weka hapa tuyajadili

sasa hayo ya madiwani nani kakuambia yameibuka leo? nadhani kwa hali tuliyonayo ni busara kufurahia mafanikio popote pale yanapoonekana sababu kila raia ana malalamiko yake dhidi ya serikali, lakini ni ujuha kutaka nchi nzima isimame sababu madakitari wanagoma au wanataka kugoma.
 
Waziri Mkuu Pinda ametangaza katika hotuba yake ya Bajeti leo Bungeni kwamba kuanzia mwaka huu wa fedha Madiwani wataanza kulipwa Posho mpya zilizoboreshwa, cha kushangaza wabunge wakapiga mameza yao kushangalia hilo....!!
Hivi kweli tumefikia hapa pa kushangilia hili wakati hospitalini leo hakuna Madaktari waliogoma kwa kutolipwa!!

wameshangilia coz wananjua na wao mgao wao unakuja......
 
Posho? you mean sitting allowance?

mkuu Mungi kwa sasa madiwani wanapata posho ya shilingi za kitanzania 120,000 kwa mwezi.
Bila shaka hizo ndio zimeongezwa, ingawa hatujaambiwa ni kwa kiasi gani. Sitegemei kusikia wameongeza sitting allowance, kwakuwa hiyo haikubaliki hata kwa wabunge na watendaji wemgine wa kiserikali, na tunataka ifutwe.
 
Last edited by a moderator:
Hivi wanapogombea hizi nafasi hadi kutoa rushwa huwa hawajui changamoto zilizopo mbele yao!!! hawajui kuwa posho ni ndogo huko!
 
Back
Top Bottom