Wabunge wanaposhangilia Posho Mpya za Madiwani...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wanaposhangilia Posho Mpya za Madiwani...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kivumah, Jun 25, 2012.

 1. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Waziri Mkuu Pinda ametangaza katika hotuba yake ya Bajeti leo Bungeni kwamba kuanzia mwaka huu wa fedha Madiwani wataanza kulipwa Posho mpya zilizoboreshwa, cha kushangaza wabunge wakapiga mameza yao kushangalia hilo....!!
  Hivi kweli tumefikia hapa pa kushangilia hili wakati hospitalini leo hakuna Madaktari waliogoma kwa kutolipwa!!
   
 2. m

  mob JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  kilichobaki ni sisi watanzania bila ya kujali itikadi zenu na vyama vyetu kusimama na kudai huduma bora na kuwatetea hawa madaktari kwa kuwa hawa ndio wanatutibu sisi ila wao wakiugua wanapelekwa india kwa matibabu .
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Kwani hao madiwani sio madiwani wetu? au haujui kwamba madai ya mafao yao nalo ni jambo la msingi pia?
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo hutaki madiwani waongezewe posho?
   
 5. ndinga

  ndinga Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nao pia ni madiwani kikatiba ndo maana wakashangilia,wabunge wetu wapo kimaslahi zaidi.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Safi sana, kwa hiyo wanashangilia kwamba wameongezewa posho zingine sio?
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  safi sana, madiwani walikuwa na hali ngumu sana iliyofanya waweze kununulika kirahisi na wakurugenzi pamoja na wasaka tenda
   
 8. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanashangilia Kwani wanajua Madiwani watapunguza kuwapiga Mizinga!
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mambo yote ya maendeleo kwa wananchi aliyosema waziri Mkuu hayakushangilia kwa nguvu na muda mrefu kama yongeza ya posho ya wabunge
   
 10. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Wabunge pia ni Wajumbe katika Baraza la Madiwani, hivyo wanajua kuwa ikiongezeka ni sawa na wao pia wameongezewa ya kule Baraza la Madiwani.

  Ndio maana wanashangilia posho hiyo mpya.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 11. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tatizo huku kwetu kila mtu mjuaji.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Halafu tunashangaa kwa nini bajeti ya maendeleo ni asilimia 30 tu! Tuendelee tu kugharamia SIASA kama mazezeta huku Wabunge wetu wakishangilia. Fedha za matumizi ya kawaida zitazidi kuongezeka tu kwa sababu zifuatazo:
  -Tunaongeza kata na hivyo madiwani nao wanaongezeka sambamba na posho zao;
  -Tunaongeza Majimbo na kuongeza idadi ya Wabunge na mishahara na posho zao;
  -Tunaongeza Wilaya na hivyo kuongeza wakuu wa wilaya, maDAS, maOCD, maDSO,...;
  -Tunaongeza Mikoa na wakuu wa mikoa na maRAS, maRSO, maRPC,...;
  -Tunaongeza mawizara, mawaziri, maNaibu wao, maKatibu wakuu, maKamishna, waKurugenzi,...;
  Yaani kila tatizo linapojitokeza tunaongeza WANASIASA. Kila kitu tunadhani ufumbuzi wake ni wa kisiasa. Ni kuongeza posho. Tuendelee tu kugharamia SIASA.
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi nashangaa, kwa nini inakuwa rahisi kwa viongozi wa KIsiasa kuongezewa Posho lakini ni vigumu kwa Madaktari na waalimu kuongezewa Posho?????

  Au kwa vile madiwani wengi wanakula madili na Wabunge.
   
 14. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,113
  Trophy Points: 280
  Another silly season.
  WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
   
 15. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sababu mojawapo ya kusababisha usimamizi mbaya ama dhaifu wa madiwani katika shughuli za maendeleo hasa miradi ya maendeleo ni kutokana na kukosa sauti ya kuwahoji wakurugenzi kutokana na malipo madogo sana wanayolipwa, hivyo wakurugenzi wanapotaka wapitishe mambo yao kiulaini wanachofanya ni kuwapa madiwani vitripu vya kwenda kujifunza kwenye halmashauri nyingine na kuwajaza miposho mbalimbali.

  Kutokana na njaa walizonazo hujikuta wanalegea kusimamia fedha za umma.
  Ingawa kuwalipa posho nzuri hakuwezi ku-guarantee kwa 100% utumishi bora zaidi lakini ni ukweli kwamba itawapa nguvu ya kuwa makini zaidi na angalau kwa kiasi fulani itawasaidia kuwafanya wawe huru zaidi kusimamia fedha za umma kwakuwa watakuwa wanajimudu kiasi fulani badala ya kutegemea fadhila ya mkurugenzi.

  Hata hivyo tunatakiwa kutathmini mfumo bora zaidi wa kuwalipa posho na stahili mbalimbali watumishi wote wa umma, ikiwa ni pamoja na wabunge na madiwani. Kwakuwa ni jambo lisilowezekana kutegemea utumishi bora kutoka kwa mtu ambae halipwi kiasi kinachomuwezesha kukidhi mahitaji yake. Kwahiyo sidhani kama tunaweza kukwepa kuigharmia siasa kwa wakati huu.

  Na kuna baadhi ya watu wanasema madiwani wanatakiwa kuwa na kazi zao za kuwaingizia kipato ili wafanye kazi za udiwani kwa kujitolea kitu ambacho kwa hakika kinashusha ufanisi wao kwakuwa wanalazimika kujitafutia riziki kwanza ndipo baadae wafanye shughuli za wananchi.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nyahende,
  Hakuna posho au mshahara utakaomtosha diwani aache kuomba kwa mkurugenzi wa Halmashauri. Wabunge wana mishahara na posho nyingi sana. Wameacha kuomba? Wameacha kuchukua bahasha za khaki kwenye taasisi zetu za umma? Mawaziri wana mishahara na posho kubwa sana lakini angalia wanavyozitafuna taasisi zilizo chini ya wizara zao. Kwa nini tunageuza nafasi za KISIASA kuwa vitega uchumi? Kwa nini tunageuza nafasi za kisiasa kuwa AJIRA? Fedha ambazo zingewanufaisha WATANZANIA kuboresha huduma za kijamii tunagharamia wanasiasa na siasa!
   
 17. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  wacha we kwa hiyo solution ishapatikana maana kama swala ni kipato kina idd simba wasingeuza UDA
   
 18. p

  petrol JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Nasikitika sikubaliani nawe kabisa. Mbona Wabunge na Mawaziri wanalipwa vizuri sana lakini mipango ya maendeleo inelekea kukwama. Tutafute sababu za msingi kwa nini mambo yetu yanakwama karibu kila kona.
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  watalipwa sh ngapi na serikali ili wasipewe mgao wao wa rushwa mfano tenda moja million 20?

   
 20. O

  Orche Senior Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Madiwani kulipwa posho halali kulingana na kazi wanayofanya ni haki yao, ila inatisha wabunge wanaposhangilia kwa kuwa na wao ni madiwani. Hawajui kuwa kuwalipa posho kubwa Wabunge bila kujali mahitaji wa wataalaam na watendaji imeleta dhahama kubwa kwa wananchi. Wabunge wetu uzalendo haupo na wapo kimaslahi tu, wanachi tuione hilo.
   
Loading...