Wabunge wanapoanza kujadili mradi wa umeme wa maji kuwa unafaa au haufai wakati ujenzi umesha fikia asilimia 40%

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Binafsi huwa naona kama vile wanapoteza muda wanapoanza kujadili mradi wa umeme unaotokana na maji wakati tayari ujenzi umeshafikia 40% na bado kazi inaendelea usiku na mchana na raisi mpya ameahidi kuhakikisha unakamilika.

Ukweli ni kwamba wanapoteza muda wao kama bunge pia wanatupotezea mda sisi wananchi tunao wasikiliza kwa sababu hu mradi hauwezi kusitishwa ni lazima ukamilike.

Lakini pia kwa elimu yangu ndogo niliyonayo kuhusu umeme nashindwa kuwaelewa wale wanaosema umeme wa maji ni gharama kuliko wa mafuta.

Ninachojua mimi umeme unazalishwa na generator na ili generator lizalishe umeme lazima lizunguushwe.

Hivyo inaweza ikawekwa mashine inayotumia mafuta au gasi ili kulizungusha hili generator liweze kuzalisha umeme.

Au hili generator linaweza likawa linazungushwa moja kwa moja kwa kutumia nguvu ya maji yanayo tiririka yani mto.

Sasa Mimi hainingii akilini kuwa umeme unaozalishwa kwa kutumia mitambo inayotumia gasi ambayo inauzwa kwa Lita ikawa sawa na umeme unaozalishwa kwa kutumia nguvu ya maji ambayo hainunuliwi ni natural power ambayo Mungu ametuwekea.

Wabunge fanyeni kazi acheni siasa.
 
Ni uzwazwa wa wanasiasa wetu tu...na hii ni mahusi katika kutaka kuchelewesha ratiba za Bunge Ili wajiongezee ratiba na maposho kibao
 
Kwa miezi mitatu watakao kaa Bungeni kwa kipindi hiki watalipwa karibu kila mmoja milioni 90 na kitu na wengine mpaka 100
 
Prof. Mussa Assad "alishathema"bunge ni "thaifu"! Wakipaswa kufanya hivi toka "thiku" ile "watho" la kujenga hilo bwawa ilipofufuliwa na jiwe ila kwa sababu ni dhaifu hawakufanya hivyi.

Waache lijengwe maana faida zake ni kubwa kwetu wanachi.
 
Rubber Stamp Parliament

In the situation where a dictator's legislature is a "rubber stamp", the orders they are meant to endorse are formalities they are expected to legitimize, and are usually done to create the superficial appearance of legislative and dictatorial harmony rather than because they have actual power.
 
Bunge letu ndio mfano halisi wa - Watu wazima wenye uwezo mdogo wa kujitambua na kufikiri.
 
Laiti magufuli angeyajua haja angepumzika tu chato kuliko kila diku kuzunguka hii Tanzania 🇹🇿 akisikiliza mapambio ya wanafiki.
 
Prof. Mussa Assad "alishathema"bunge ni "thaifu"! Wakipaswa kufanya hivi toka "thiku" ile "watho" la kujenga hilo bwawa ilipofufuliwa na jiwe ila kwa sababu ni dhaifu hawakufanya hivyi.
Waache lijengwe maana faida zake ni kubwa kwetu wanachi.

Aisee wewe ni me au ke, embu jibu haraka alafu nikuambie kitu.

Mbona unaandika kama....
 
Ukiona tu quotation mark ukiwa katika hali ya utimamu unaelewa kilichomaanishwa kukusudiwa.
 
Back
Top Bottom