Wabunge wanaolipa uhai Bunge la Jamhuri ya Tanzania

Jamani wanaja JF nawaomba/kuwasisihi tuwe wawazi, bila kuwa na itikadi, upendeleo wala ushabiki na ushushushu. Wabunge wa chama gani wanafanya maelfu ya watu kupenda kusikiliza/hata kuangalia bunge letu?. CHADEMA, CCM, CUF, NCCR, UDP, CCJ au chama gani.? Mimi bila kupendelea kama wasingekuwepo wabunge wa CDM wala nisinge sumbuka kuangalia wala kusikiliza bunge.
Nawasilisha.

hapo kwa red unamaanisha mzee 6 na mwakyembe au?
 
miaka ya nyuma likiwa bunge la chama kimoja wala halikuwa na mvuto au kusikia watu wanzanungumzia ila moto unaowashwa na wabunge wa upinzani unafanya bunge linapendeza sana, ila kwa sasa Tindu Lisu anangarisha sana Bunge......... akisimama mama makinda, wabunge wa ccm na mwawaziri nywele zinawasimama, ia kikwete anatambua hilo!
 
mimi januari makambalio na brig. hassan ngwilizi, wana hoja nzuri sana kushinda hata za mwenyekiti wa CCM kitongoji cha mwitongo kata ya mwalengalilo
 
Wewe ni mdogo wake wa Anna Makinda bila shaka. Utasikia Lindu Lisu kaa chini. Mimi nawakubali wengi miongoni mwa wabunge wa Chadema sepecifically Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Zitto, Mnyika, Susan Lyimo, Halima Mdee, Ezekia Wenje, Mbunge wangu Msigwa, Chiku Abwao, Godbless Lema, Vincent Nyerere, Mchungaji Israel Natse,Susan Kiwanga, Regia mtema, Anna Maulidah Komu, Silinde na Esther Matiko. Pia Kafulila, Mkosamali (NCCR), Habib Mnyaa na salum Baruany (CUF) na Harrison Mwakyembe, Christopher Ole Sendeka na James Lembeli, Mama Tibaijuka na John Magufuli (CCM)

Umeongea vyema kabisa ndugu, ila mimi bado sijamkubali Anna Tibaijuka, nilitegemea makubwa sana toka kwake bado anapwaya ardhi, labda tumpe muda.
 
Leo Sugu kanifurahisha sanaaaa,anawaambia magamba nayo yakaandamane yaone kama yatapata watu kama CDM...hili ndo liliwafanya ccm kuomba mwongozo wa spika,Xellent Mr.2
 
Bigirita umeniacha hoi na coment yako kuhusu john komba ila mie napenda wabunge wanaotetea masilahi ya taifa sio wale wanapiga makofi bora siku iende
Kwa posho wanayopata lazima waitumikie kwa kutoa hoja za msingi kwa wabunge wa CHADEMA au kukupiga makofi na kuzomea kwa wabunge wa CCM!
 
Da kuna mbunge mmoja jana alikuwa anaongea shudu mpaka nikajiuliza hata vitabu sijui uwa anatungiwa hau la.
 
mi napenda wa magamba, tena kama hawa watu sura zao zikakaa pamoja s.wasila, a.mwanri, pinda na makinda unaweza usitazame tena bunge na kukimbia.
 
Tuache unafiki. Unadhani isingekuwa hawa wabunge waliovuma ktk media, hasa wa CDM, ungekuwa na hamu ya kufuatilia bunge? Acha kumfagilia mbunge wako ambaye hana hata mvuto. Kazi kulala tu mjengoni. Asante sana mtoa mada.
 
Back
Top Bottom