Wabunge wanaohama kabla ya muhula wao kuisha Wananchi hatuwataki tena

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
431
577
Kwa wale viongozi wa kisiasa walio hama chama kati kati ya muhula yaani kabla ya kipindi chao kuisha hawa hatuwahitaji.

Hawa viongozi badala ya kututumikia sisi wananchi wao wanatumia vyama vya siasa na matumbo yao zaidi.

Kumbuka kipindi tulipo wachagua wale viongozi wa upande mwingine tuliwaona lakini tukasema tunawataka wa upande huu. Lakini kwa upande wao wao wameonesha kuwa sisi wananchi tulifanya makosa kuwachagua wa upande huu bali tunge wachagua wa upande ule na kama tungefanya kama wao wanavyosema sasa baada ya kuwapa nafasi adimu ya kutuongoza tungechagua kama wanavyosema inamaana wao wasingepata nafasi hizo.

Ila wametufunza tutakachofanya kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwa wale wasio na msimamo kisiasa tutapiga chini kuanzia ngazi ya chama hadi kwenye ngazi ya familia tutawanyima uongozi na jua hata kupewa ukuu wa mkoa ama wilaya tumefanya makosa maana hawa na malaya wa kisiasa hatuwataki na tena watukome


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom