Wabunge wanaoamini MAGEUZI kufanya mkutano na waandishi saa tisa alasiri leo hii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wanaoamini MAGEUZI kufanya mkutano na waandishi saa tisa alasiri leo hii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Apr 22, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Na Zitto Kabwe:

  Tutakuwa na mkutano na Waandishi wa habari leo saa tisa mchana Bungeni Dodoma. Ajenda 1) kuutaarifu Umma kwamba #Sahihi70 zimetimia 2) kwamba Spika atakabidhiwa Hoja kesho Jumatatu 3) kutoa ufafanuzi kuhusu sharti la siku 14 kabla ya siku ya hoja

  UDATES:

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012


  · Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini

  · Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

  Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

  Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

  Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

  (a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

  Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

  Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

  Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

  Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
  …………………………….


  Kabwe Zuber Zitto.
  Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
  22/04/2012.
   
 2. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Tupo pamoja sana na hao wabunge. Ila wanatakiwa kujua tatizo sio Pinda
   
 3. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa ni saa tisa na dakika tisa!!

  Any pdates??
   
 4. m

  mchambakwao Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Pinda anaonewa lakini wakuu Pinda ni msimamizi au kiongozi wa kazi serikali bungeni.So hili hawezi kulikwepa otherwise ajiuzulu.Hapa tatizo ni mzee wa Upepo utapita!
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,110
  Likes Received: 10,466
  Trophy Points: 280
  pamoko tupeni manews..
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nimechoshwa na hizi sinema za bungeni.
   
 8. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...ooh...oooh!!
  Huu upepo bado wavuma tu. Natamani kiwe kimbunga.
  Kila la heri.
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mh. Pinda naona afadhali ajiuzulu tu amnwachie mkwer.e serikali yake ili tuitoboe macho, hatuwezi kuwa na serikali isiyowajibika
   
 10. l

  liverpool2012 Senior Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama sio pinda ni nani,wewe ukifanya mambo ya kijinga watu watasema umepata malezi mabaya toka kwa wazazi,so pinda mzazi ameshinda kuwa wajibisha watoto,tunamwajibisha yeye.

   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Zitto fanyeni kweli,4 the seek of the nation makinda kesho akikataa apigwe pale na ang'olewe kwa mabavu kama ukraine then naibu spika Ndugai..aweke hoja mezani
   
 12. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Mh! Yetu macho,mimi huwa nasema kila siku wanasiasa siyo waungwana hata kidogo hata hawa akina zitto nao wakichukua haya yatatokea tu, unacheza na watanzania waliozoea kulalamika>
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Any update?!
   
 14. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Weee lama nchi inayoongozwa kisheria kitu kama hicho hakiwezekani, ongea point bwana acha kushauri utumbo.
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  pinda anafanywa Bangusiro mwingine.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Updates please, 9:30 sasa!
   
 17. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nawashauri hao wabunge wasiache kuingia japo na mayai viza kwenye kikao cha kesho ili Makinda akileta upuuzi wake basi wamfikishie ujumbe wao kwa njia mbadala!
   
 18. b

  buzz Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Zito komaaa na msimamo wako kesho hoja ipelekwe bungeni kutokuwa na imani. Tukisema eti Pinda hana makosa wakati yeye hataki kuwawajibisha mawaziri basi yeye abebe msalaba wao. Baada ya Pinda kutoka atafuata JK tena atatoka kwa aibu zaidi. JK kwa sasa hana tofauti na Gadaffi aliye waita wananchi mapanya. Hatumtambui kwa sababu hajasema kwa kinywa chake lakini anaonyesha jinsi anavyolidharau bunge ambalo ni wananchi pia. Wabunge wa CCM nao wamekuwa makondoo na kupiga domu tu bila maamuzi. Akina Jan Makamba nilidhani jasiri kumbe domu tu vitendo hakuna. Sasa hilo zoezi alilolianzisha Zitto limetusadia kujua nani mbunge wa wananchi na nani mbunge wa mafisadi. Not longer than sooner you will step down.
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  safi sana
   
 20. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Zitto tupo pamoja kaba magamba mpaka washangae.
   
Loading...