Wabunge wamlipua Luhanjo wa Ikulu; WAMTUHUMU NDIYO CHANZO KIKUU CHA UFISADI MALIASILI NA UTALII! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wamlipua Luhanjo wa Ikulu; WAMTUHUMU NDIYO CHANZO KIKUU CHA UFISADI MALIASILI NA UTALII!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 17 August 2011 20:18[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG]

  Katibu Mkuu Kiongozi Phillemon Luhanjo
  Neville Meena, Dodoma
  KAMATI ya Wabunge wa CCM imeendelea kuwa mwiba kwa Serikali baada ya jana baadhi yao kumtaja kwa jina, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba ni chanzo cha ufisadi na uozo katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Wabunge hao wamemtaja Luhanjo ikiwa ni siku moja baada ya kukataa kufungwa mdomo katika kujadili Bajeti ya Maliasili na Utalii na kutaka iwasilishwe kwanza bungeni ili wapate fursa ya kuchangia kama wabunge wengine, kuliko kuwa na msimamo wa kichama katika kuipitisha bila kuijadili kwa kina na uwazi.

  Jana, kamati hiyo ilikutana mnamo saa 7:00 mchana katika kikao ambacho kilichukua takriban saa mbili na nusu na kutoa maelekezo magumu yanayoitaka

  Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma unaofanywa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, inayoongozwa na Waziri Ezekiel Maige.

  Maelekezo mengine yaliyotolewa na wabunge hao kwa mujibu wa taarifa ambazo zilipatikana ni kumtaka Waziri Maige kushughulikia tatizo la ukabila katika Idara ya Wanyamapori, kufutwa kwa vibali vya kukamata na kusafirisha wanyama hai nje ya nchi na kurejeshwa kwa wanyama waliotoroshwa na kupelekwa nje Novemba mwaka jana, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zilidokeza kwamba awali, wabunge hao walikuwa wametishia kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama walivyofanya ile ya Nishati na Madini, lakini waliridhishwa na ahadi za Serikali kwamba itachukua hatua stahili.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Luhanjo alitajwa kwa jina kwamba amekuwa chanzo cha utendaji mbovu katika Idara ya Wanyamapori iliyoko chini ya wizara hiyo kwa kushawishi uteuzi wa watendaji kwa misingi ya ukabila ili kulinda kile kilichodaiwa kuwa ni maslahi yake binafsi.

  “Hata orodha ya watendaji wa idara hiyo ambao wanatoka kwa mheshimiwa huyo wa Ikulu imesomwa pale na tumeomba Serikali ichukue hatua, sasa watafanya nini watajua wao wenyewe,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza:

  “Idara hiyo ni nyeti na ndiyo inasimamia wanyamapori, sasa haiwezekani watendaji wake wote wakatoka sehemu moja tu ya nchi tena kabila moja, hapa tumenusa kitu na tumesema Serikali ikifanyie kazi.”

  Awali, wabunge hao walihusisha hata uhamisho wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi kwamba ulilenga kulinda kile kilichodaiwa kuwa ni “maslahi ya Luhanjo” wizarani hapo lakini baadaye walijulishwa kuwa katibu mkuu huyo hakuwa sehemu ya mkakati huo.

  Luhanjo aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani alimteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Martin Lumbanga ambaye sasa yuko Geneva, Uswisi akiiwakilisha Tanzania katika mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko nchini humo.

  Luhanjo anena
  Alipopigiwa simu kujibu madai hayo ya wabunge Luhanjo alionekana kupata taarifa hizo kabla ya kupigiwa simu kwani aliuliza: “Unaulizia hao wabunge waliokutana kwenye kikao na Waziri Mkuu siyo... sasa unasemaje?”

  Baada ya kuulizwa juu ya tuhuma hizo alijibu kwa kifupi: “Sikubaliani na hoja zao hizo, si kweli ni majungu, achana na hiyo kitu bwana.”

  “Mimi ni Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi nzima, sasa hayo mambo ya wizara mimi naingiaje huko, si kweli kabisa na mimi sikubaliani nao,” alisema kisha kukata simu akijiepusha na kombora hilo.

  Kamati ya Bunge
  Mapema akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, mwenyekiti wake, James Lembeli alisema kamati yake inasikitishwa na hatua ya Serikali kupuuza mapendekezo yake kuhusu suala la kufuatilia na kurejeshwa kwa wanyama waliotoroshwa nchini.

  “Mapendekezo hayo ya kitaalamu yalilenga kuisaidia Serikali kuhakikisha upatikanaji wa wanyama hao. Ni jambo la kufedhehesha Mheshimiwa Spika, kuona kwamba tangu utoroshwaji wa wanyama hao ufanyike Novemba 24, 2010 hadi leo bado Serikali ilikuwa haijui wanyama hao wako wapi hali inayotia shaka na kuhoji kulikoni?,” alisema Lembeli na kuongeza:

  “Yapo maswali mengi ya kujiuliza kuhusu suala hili la utoroshwaji wa wanyama hao. Katika wanyama 116 waliotoroshwa wenye thamani ya Sh163,732,500 ni pamoja na twiga wanne. Kama ndivyo, Kamati inauliza kwa nini Sheria ya Wanyamapori inayozuia raia wa kigeni kupewa leseni ya kukamata wanyama wakiwamo twiga ambao ni nembo ya taifa haikuzingatiwa?”

  Alisema hali hiyo inaashiria kuwapo kwa dalili kubwa ya uzembe na kulindana ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kwamba hicho ndicho chanzo cha kigugumizi katika kuchukua hatua.

  Lembeli alisema shaka hiyo inajidhihirisha wakati wa uhamisho wa maofisa uliofanyika hivi karibuni na kwamba haukuwagusa kabisa wa kitengo cha Uwindaji wakiwamo wa Arusha na kuongeza kwamba licha ya kadhia hiyo ya kutorosha wanyama, baadhi ya maofisa hao wamepandishwa vyeo.

  Kamati hiyo ya Bunge iliitaka Serikali kuwabaini wote waliohusika na kashfa hiyo na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola mara moja, huku ikipendekeza kuwepo kwa ofisa wanyamapori wa kudumu katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro ambacho nyara nyingi zinazosafirishwa nje hupitia.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh, hatari!
   
 3. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  SASA HAPA HEBU TUWEKANI WAZI KWA KWELI.....HIVI LUHANJO AMBAYE ALIWEZA KUMSIMAMISHA KATIBU MKUU WA WIZARA JAIRO...AMBAYE MASAA YOTE YUPO NA RAIS IKULU NA INAWEZEKANA HATA MENU WANAPATA PAMOJAAA...HIVI MAIGE ATAMFANYA NINI??? HATA MSEKWA MAIGE ATAMFANYA NINI?? DOGO HUYU KWAOOO JAMANIII..hapa kweli mbwa anataka kubweka kwa tembo aliyevamia Shamba..hahahah,.,So funny
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Huu ni usanii tu,kila siku tuhuma zinaibuliwa but nothing is going on,so serikali imekuwa kiburi au haina uwezo wa kuwawajibisha?
   
 5. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kuna mtu mmoja serikalini aliyebakia na maadili mema ni huyu mzee. Tatizo watendaji wake wanamdanganya kama ilivyo kawaida ya watumishi wengi wa serikali.
  Ila akijuwa umempa taarifa zisizo za kweli, umekwisha. Hii naona ni njama ya kumchafua mzee wa watu aondoke ili walafi wale vizuri sababu anawabana sana.
  Huyu mzee sio wa 10% na akikumata umekwisha na wengi wanamchukia kwa hilo.
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu umenena hii ni sawa na mbuzi kulazimishwa kuwinda chui,
  hahahahahahaha TANZANIA kuna mambo, kuna siku mkuu wa wilaya
  hata ambiwa amchukulie hatua kikwete kwa kutoa ahadi hewa wilayani kwake hahahahahaha
   
 7. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo ubaya wa mamlaka ya raisi unapoonekana,maadamu kateuliwa na raisi anawajibika kwake tu,wengine hawawezi kumwajibisha.katiba mpya njoo haraka.
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama ni mkali hivyo inakuwaje mambo yako hivi kwenye mawizara , tena uchafu mkubwa unafanywa na makatibu wakuu walio chini yake,
  na yeye kumshauri kikwete achukuwe hatua kuhusu wizi anangoja nini?
   
 9. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,747
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Chimbeni chimbeni kote
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Acha hizo banaaa. Jamaa anaweka kwenye post watu wa kabila lake kwa hila hila tu hata kama hawana uwezo.
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Majuzi Masoud Kipanya alitoa kibonzo chake akisema amekuja gundua kuwa wenye matatizo ni sisi watanzania kwani kila kifanywacho na viongozi wetu sisi ndio tuna tokomea kabisa kwenye umaskini hivyo basi sisi ndio tuchukue jukumu la kuifanyia nini serikali yetu.

  Hapa itakuwa ni mchezo ule ule na ndio maana wanakimbilia sheria ya kurekebisha kuhusu swala la maaandamano wakijua fika wananchi wanakuja barabarani muda si mrefu, Tatizo Umeme a.k.a mgao wa kiza, Mafuta,Hali ya maisha iko juu,Rasilimali zetu zinaibiawa wanayama ,madini bado wananchi wa tanzania ni wavumilivu ila serikali yake ndio haisikii na kujisifia kila siku bungeni ati ni sikivu sijui kwa lipi haya yote yanayo taajwa bungeni ni kuwa wananchi munaaambiwa tuingie mitaani sasa na sio tusubiri ati serikali yetu itufanyie kitu
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  sie yetu macho .maana naona sasa mmekuwa kama samaki mwalana wenyewe kwa wenyewe. hakuna mzalendo.

  hata nyie mkipata mwanya, mnamaliza kabisaaaa kuliko Luanjo.
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Luanjo, kwa kweli mimi binafsi huwa simuelewi kazi yake.
  Huwa namuona tu pale rais akimuapisha mtu, kasimama pembeni mvi nyingi sana kichwani
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umepotea kidogo, lakini muda bado unarhusu unaweza pata njia
   
 15. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,857
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Ukitaka Kujua Ndoa iliyopo kati Ya Ndugu Luhanjo na Hiyo Wizara ni kupata Habari Zinazomuhusu Ndugu Savere, Na Luhanjo enzi hizo Mmoja ni Mkurugenzi na Mwingine ni katibu Mkuu, Huku katibu mkuu akimpigia magoti Mkurugenzi ili wagawane Keki waliyoipata!! Just Make a follow up and Flush Back!!!
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Hapa nchi ilipofikishwa na magamba bora kiwake.
   
 17. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mzee P Luhanjo alishawahi kukaa pale wizara ya utalii na maliasili, b4 kuhamishiwa foreign affairs n then Chief Secretary...!,
  Utamu wa asali ya pale anaifahamu vizuri sana....,
  So tutegemee nn kutoka kwake ktk hii govt legevu ya swahiba wake JK?

  Hao wabunge watapiga kelele pasipo kutaka kuibana govt ichukue hatua kali dhidi yake...., mifano ipo, everytym hutoa lawama kwa Govt mjengoni, baadae kupitisha bugdet ya wizara husika kisa ooooaah sisi ni CCM na hii Govt legevu ni ya kwetu..! huwa wanashangilia Govt yao legevu kuendelea kuwa hivyo na kuitukuza usiku na mchana...!

  Waweza kuta baadhi ya wabunge wanamtumia Luhanjo memos, kutaka kuteuliwa kuwa mawaziri au kutafuta nafasi za jamaa zao ili kupata nyadhifa mbalimbali ktk Govt na Mashirika yake!
  Yeye ni mshkaji wake JK, katibu mkuu kiongozi nk, ana nafasi kubwa ktk kuchangia uteuzi wa mtu, tumeona jinsi alivyoingilia kwa maslahi yake binafsi, na ya wabena society ktk uteuzi wa DG wa NHC,
  leo tumeona ktk uteuzi wa Idara ya wanyama pori na wizara husika.

  Aliweza pia kuingilia BOT pale ilipowashtaki wale wafanyakazi wake (baadhi watoto wa VIgogo) waliokuwa wanatuhumiwa kuwa na certificates fake, kisa mwanae alikuwa mmoja ya watuhumiwa!!!

  Tuna tegemea nn? kutoka ktk hii Govt ya JK iliyo Legevu na isiyo sikivu kwa wananchi wake!!
   
 18. TGS D

  TGS D Senior Member

  #18
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaudhi tena inakera sana kwa ufisadi huu.

  Tafakari chukua hatua!
   
 19. C

  Cognitivist JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 778
  Likes Received: 986
  Trophy Points: 180
  Aaaah! Tanzania nchi yangu, nakuskitikia sana, sijui ni wapi unapoelekea If things are just like this... Pole sana. Pple wake up! It's tym 2act and not 2complain.
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi narudi kule kule kwenye misingi ( power map). Kama katiba iko kimya juu ya udhaifu fulani, Rais anakuwa ndo jawabu - anatoa mwelekeo. Ukiwa na Rais kama Nyerere ambaye ni objective, hutahisi tatizo. Ukimpata kama Kikwete kila mmoja wetu jibu analo.
   
Loading...