Wabunge wamkana Spika Anne Makinda kuacha ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wamkana Spika Anne Makinda kuacha ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Anna Makinda Samamba Speaker wa bung la Tanzania

  Baadhi ya wabunge wa Bunge, wamesema uongozi wa umma sio fedha pekee na kwamba hawana mpango wa kuachana na siasa kutokana na kulipwa mshahara na posho kidogo. Walitoa kauli hiyo walipozungumza na NIPASHE, kufuatia kauli ya Spika, Anne Makinda, kuwa nusu ya wabunge hivi sasa wanatamani kuachana na siasa na kwenda kufanya walizosomea kutokana na kulipwa mshahara mdogo pamoja na posho.

  Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde, alisema uongozi sio fedha na kwamba kama mbunge alitaka kuingia bungeni kwa ajili ya kupata utajiri anaweza kuona kazi hiyo kwa sasa haifai na kukiri kwamba mshahara wanaopata wabunge hauotoshi ikilinganishwa na mahitaji ya wananachi wanaowawakilisha, lakini hiyo sio sababu ya kutosha.

  Alisema kitu cha kwanza wanachoangalia kwa wabunge makini ni kuwawakilisha wale waliowachagua na kwamba fedha kinakuwa kitu cha mwisho katika kufikiria badala ya kukitanguliza. Alisisitiza kuwa uongozi ni dira na wala fedha haina nafasi yoyote kwa kiongozi makini kama mbunge na kwamba mtu anayetaka ubunge ili awe tajiri hafai kuchaguliwa.

  Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndasa, alisema wabunge hawakuchaguliwa kwa lengo la kwenda kupata mshahara mnono badala walipewa jukumu hilo ili kuwatumikia wananchi. Alisema mbunge makini hawezi kutegemea mshahara na posho pekee na badala yake anatakiwa kufanya kazi zingine za ujasiliamali ili kujiingizia kipato. “Nilitaka kwenda bungeni ili kuwawakilisha wananchi na sio kutafuta utajiri hivyo sioni shida yoyote mpaka nitamani kuachana na siasa eti kutokana na posho ndogo au mshahara mdogo kama alivyosema Spika,” alisema.

  Mbunge wa Serengeti (CCM), Dk. Kebwe Stephen Kebwe,, alisema hana mpango wowote wa kuachana na siasa kutokana na kipato kidogo na badala yake ataendelea kuwawakilisha wananchi wake kama kawaida. Alisema alipoomba nafasi hiyo mwaka 2010 aliwaambia wananchi wamchague ili awawakilishe bungeni, lakini sio wamchague ili akapate utajiri kupitia mishahara na posho nono.

  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Margareth Sitta, alisema kuna haja ya kumuuliza Spika Makinda ili aeleze alikopata takwimu kwamba nusu ya wabunge wanatamani kuachana na nafasi zao na kwenda kufanya kazi walizosomea. “Mimi sina takwimu manake isije ikawa Spika alizungumza na wabunge wawili halafu akasema nusu ya wabunge wanatamani kuachana na ubunge kutokana na posho na mshahara mdogo,” alisema.

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), alisema hana uhakika kama kweli wabunge wametaka kujiuzulu kutokana na kulipwa kidogo. Alisema kama kuna watu wanawaza hivyo hao sio wabunge na kwamba walipaswa kujiondoa muda mrefu kwa kuwa hawafai kuwawakilisha wananchi. Mbunge wa Karatu (Chadema), Israel Natse alisema wabunge wa CCM ndio wanaotamani kujiuzuru, lakini kwa upande wa upinzani hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wao sio wabunge wa posho na kwamba wanajali kwanza kuwatumikia wananchi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mshangai

  Mshangai JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 331
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  Sasa Makinda kila asemacho kinakuja dhihirika kuwa ni uongo mtupu. Uongozi wa Bunge kwa kweli umepwaya sana toka wamuwekee Sita kauzibe ya kukosa sifa ya kuwa na jinsia ya kike ili wampitishe.
  Ingekuwa ni mchezo wa mpira na kuwalinganisha yeye na Sita katika possession ingekuwa MAKINDA 3% -SITA 93%
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Makinda ni mwongo, anajaribu kutumia mgongo wa wabunge kusimamisha masilahi yake bianfsi. Mbona hata baadhi ya wabunge wa CCM wanakana kauli yake?
   
 4. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Katika maspika wote waliowahi kushika wadhifa huu, huyu ndiye Mwanaasha wao! Hivi kanuni za Bunge zinasemaje, spika lazima akae mpaka miaka mitano? Hawezi kuenguliwa? Anatia kichefuchefu!
   
 5. d

  dguyana JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bunge la safari linachekesha sana.

  Yaani spika muongo????? Nimeamini itafika sehemu nchi itashindwa kutawalika maana hakuna wa kumnyoohsea kidole mwenzie.

  Hii ndio shida ya mtandao.

  Waiter!!
   
 6. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  M just dissappointed.......hivi hakuna kipengele cha kura ya kutokuwa na imani na spika jamani ?????

  1. Mh Kigwangallah hebu mtujuze wapiga kura hali kama hii ya sintofahamu inayosababishwa na spika huwa mnaichukuliaje mkiwa kama wananchi-cum-wabunge ????

  2. Mkikaa nje ya bunge huwa mnapata nafasi ya kumuambia kama nje ya bunge mathalani humu JF huwa tunajadili na kuwapima mnayoyafanya mule ndani na nje ukumbi ??????
   
 7. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli
   
 8. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sijamuelewa huyu bibi.Hivi ana hadhi kweli ya kuendelea kuwa spika ilihali ni muongo hivi?
   
 9. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Juzi niliposema huyu mama ni mchawi wengi hawakunielewa. Ana ubinafsi uliokithiri huyu mama. Kule Sinza aliwahi kuwa na mzozo na mtaa mzima baada ya kuziba njia eti asiibiwe. Akaongopa kuwa amepata kibali cha manispaa lkn baadaye uongozi wa Wilaya ulimkana na kusema wenyewe kwanza hauhusiani na njia za mitaani.
   
 10. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gender equity inawatokea puani, wapeni wenye mioyo migumu nafasi nyeti kama hizo, hayo ndio maumbile aliyoyaumba mwenye nguvu na mfalme wa wafalme, mfumo wowote mpya wa kibinadamu lazima uprove failure.
  BWANA ASIFIWE
   
 11. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wanawake mnamuona mwanamke mwenzenu?

  Ndio kweli huyu anawapigania wanawake wenzake kwa style hii?
   
 12. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Nilishasema - Makinda kaongea uongo huu ili kumjibu JK na kutaka kurudisha heshima yake baada ya kupopolewa na JK juu ya suala la posho. Kwanza atuambie ni wapi wabunge wa Kenya waliwacheka wabunge wa Tanzania juu ya kulipwa posho ndogo. Nawashauri wabunge wa Kenya wamshtaki kwenye bunge la Afrika Mashariki. Hili ni kosa kubwa sana sana, Makinda anachonganisha Tanzania na Kenya kama alivyofanya Idd Amin!
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama viongozi wanatoa kauli za kupinga, Makinda anatakiwa kuwajibika
   
 14. m

  mlaso Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwaaaa kwaaa kwaaaa!!! mama anatia aibuuuuu!!uongo mkubwaaaa....mchana kweuuuupeeeee!!looo.atachomwa na moto wa bluee kiama ikifika
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Huyu Mama kumbe ni muongo eeh! dah! hastahili tena kuendelea kuwa Spika wa Bunge wala mbunge. Ni bora tu awajibike kwa kusema uongo.
   
 16. M

  Mponjori JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 2,210
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiv ana watoto?mbona anawadhalilisha wanae kila kukicha uongo??chezea siasa makinda!
   
 17. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kweli huyu bibi kila kukicha yeye ni kujibebesha milawama ya ajabu ajabu tu kwa kauli zake za kuzani huu ni wakati wa utoto wake walipokuwa wanadanganywa hovyo, hapa la muhimu ni alichosema huyu mama six, tulitakiwa tumuulize huyu bibi hiyo reaserch na takwimu zake kazitoa wapi, lakini kwa kuwa siku hizi tunawaandishi vihiyo wanaojali zaidi matumbo yao hawahoji hata zaidi
   
 18. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ivi ana boyfriend,2peleke posa manake kukosa.... Ndo kunamwathiri
   
 19. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du hilo poz
   
 20. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Msishange sana, ndo siasa za "maji taka" hizo. Huyu si ndo mtetezi mkubwa wa mafisadi? Limama lizima linadhubutu kutunga uwongo mkubwa namna hiyo. Bungeni muongo, uraiani nako muongo, wapi ataaminika sasa? Hao wabunge wa CCM si ndo walimpitisha? Wacha waendelee kula matunda ya uozo na upumbavu! Walivyokuwa wanashadadia kwa kugonga meza walidhani kitu gani?
   
Loading...