Wabunge wamgomea Spika kuwaziba midomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wamgomea Spika kuwaziba midomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 18, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wabunge wamkatalia Spika kuwaziba mdomo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 18 August 2012 12:46 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Boniface Meena
  Mwananchi


  WABUNGE wamemkatalia Spika, Anne Makinda kuwaziba mdomo kuhusu kuzungumzia tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi yao wakiwa majimboni. Wakizungumza baada ya kauli hiyo ya Spika Makinda, wabunge hao walisema hawaoni mantiki ya kuzuiwa kuzungumzia suala hilo wakati ufisadi ni moja ya matatizo ya kitaifa.

  Juzi, Spika Makinda wakati akiahirisha Mkutano wa Nane wa Bunge, aliwazuia wabunge kujadili wakiwa majimboni, tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi yao zilizoibuliwa wakati wa Bunge hilo la Bajeti.

  Spika alitoa msimamo huo kama mwongozo, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa hoja ya kuliahirisha Bunge hadi Novemba, mwaka huu. Alisema ni muhimu wabunge wakaacha kulijadili suala hilo wakiwa majimboni kwa kuwa bado linafanyiwa kazi na kamati ndogo inayoongozwa na Hassan Ngwilizi.

  “Napenda kuwasihi waheshimiwa wabunge msiende kuzungumzia masuala ya rushwa kwenye majimbo yenu, kamati iliyoundwa ni quasi judicial (mahakama ndogo), hivyo ina nguvu ya kimahakama,” alisema Spika Makinda. Alisema ameiongezea muda kamati hiyo ndogo hadi Septemba 14, mwaka huu kumaliza kazi yake.

  “Nimesema msilizungumzie kwa sababu kuna baadhi ya magazeti pia yatahojiwa kwa sababu tayari yamekuwa yakiandika taarifa ambazo haijulikani zimetoka wapi,” alisema Spika Makinda.

  Maoni ya wabunge
  Baadhi ya wabunge wamekuwa na maoni tofauti kuhusu msimamo huo wa Spika. Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere alisema hatua hiyo ni kuwafunga mdomo wabunge wanaochukia rushwa ili wasiendelee kuikemea. “Watoaji na wapokeaji rushwa hawataiacha tabia ya rushwa, siyo kwa kuwa wana nguvu kubwa ila kwa kuwa wanaoichukia rushwa wananyamazishwa,” alisema Nyerere. Alisema wito huo wa Spika Makinda hautekelezeki kwani wananchi majimboni lazima watawauliza wabunge wao kuhusu tuhuma hizo zilizowakumba baadhi ya wabunge na kusababishwa kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe alisema wabunge kusemana wenyewe ni jambo jema katika mapambano dhidi ya rushwa. “Bunge halijachafuka kwa suala hilo lakini kilichotokea ni hatua njema ya kupata Bunge zuri hapo baadaye, tumejisema wenyewe ili kujiangalia,” alisema Filikunjombe.

  Filikunjombe alisema hata Sheria ya Rushwa inayolalamikiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah kuwa inamzuia kuwafikisha wala rushwa wakubwa mahakamani mpaka apitie kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), inawezekana iko hivyo kwa ajili ya kulindana.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema haoni kama kuna tatizo kwa mbunge yeyote kuzungumzia suala la rushwa kwa ujumla, kitu muhimu ni kutokutaja majina ya watu.

  Alisema jambo muhimu ni kuwa yale madai yaliyoko kwenye kamati yasizungumziwe kwani kufanya hivyo ni tatizo kwa wale ambao wanatuhumiwa. “Wengine wanaweza kutumia majukwaa kujisafisha na tuhuma hizo wakati bado kamati inaendelea na uchunguzi wake kitu ambacho si sawa kwenye mwenendo wa kazi za Mahakama,” alisema Rashid.

  Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema wabunge wana akili na kwamba hawawezi kuacha kuzungumzia masuala ya rushwa kwa kuwa wanazijua kanuni na taratibu za kisheria zilivyo.

  Alisema wabunge lazima waendelee kuikemea rushwa kwa nguvu zote kwani kuna namna ya kuzungumzia masuala hayo bila kuingilia ushahidi wa kamati inayochunguza.
  “Sioni kama kuzungumzia masuala ya rushwa kuna tatizo, wabunge ni watu wazima na wanaelewa mipaka yao hivyo sidhani kama wataingilia kazi za kamati ,”alisema Bulaya.

  Kamati inayoendesha uchunguzi huo inaongozwa na Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi. Wajumbe wake ni John Chiligati (Manyoni Magharibi), Riziki Omar Juma (Viti maalumu), Said Amour Arfi (Mpanda Mjini) na Gosbert Blandes (Karagwe).  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Amefundishwa na waliomweka kwenye hiyo nafasi, maana ukitamka chochote kuhusiana na ufisadi tayari unaongezea msumari kwenye jeneza la ccm!
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wabunge ni wawakilishi wa wananchi,unaposema wabunge wasiongelee rushwa ni sawa na kusema wananchi walioweka serikali hii madarakani wasiongelee swala la rushwa kisa kuna kikundi kidogo cha watu kinachoitwa 'kamati'

  isitoshe kamati zenyewe hazitoi majibu!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280

  Na ukizingatia misumari iliyopo ni ya kutosha. Sijui hata siku ya parapanda/kiama kama watatoka.

  Ati quasi judicial, my foot! Walizoea kusema suala liko mahakamani lisijadiliwe!

  Moto hauzimwi kwa kuufunika na khanga. Source: king'asti
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kweli liwalo na liwe. Watu hawa wanaonyesha wameshakata tamaa ya maisha kisiasa.
   
 6. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wabunge wanapinga kauli/agizo la Spika nje ya kikao?mitaani?kwanini hawakumpinga pale pale na ikawekwa kwenye hansard?usanii
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama miongozo ni marufuku unategemea nini zaidi ya kuongelea mambo nje ya bunge.
  Ni dhahiri hata wabunge wamekosa imani na taasisi yao.
   
 8. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nimekupata mkuu,na recently tumeona spika na wote walioachiwa kiti kile walivotumia nguuvu nyingi kubinya wapinzani
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Haipiti siku moja bila ya kusikia kiroja toka kwa CCM. Last kicks.............
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wanawake wa Tanzania watadhurika sana na utendaji wa huyu Spika. Amekuwa anazuia mijadala yenye maslahi kitaifa kwa kisingizio cha mahakama. Sasa hao hao waliompa cheo wanamwambia ajifiche na maneno 'quasi judicial', na kwa sababu alipewa cheo mezani hana ubavu wa kutofanya kama alivyoagizwa. What an embarrassment!
   
 11. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli huyu Madam Spika anatuaibisha sana wanawake.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Na kuanzia sasa mpaka 2015 ndiyo Viroja vya magamba vitazidi kuongezeka kutokana na kuweweseka kwao na uchaguzi ujao.

   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Huyu mama ni mzigo, yaani JK na serikali ya ccm wafanya watakavyo. Rushwa ndani ya CCM ni takrima, JK aliingia madarakani kwa takrima, na ndio maana Ubadhilifu mkubwa ulifanywa na wana CCM. Rushwa, Ufisadi na Unyanyasaji wa wananchi ni sumu inayoimaliza CCM.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mwasi, nimeisoma hii dikshonari imenichanganya kidogo kuhusu hii neno "madam" mbona inasomeka eti ni mwanamama anayeendesha shughuli za danguro,

  hivi hii ndiyo shughuli ya makidra?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Mzee wa ngano

  Mzee wa ngano Senior Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anne Makinda vakhu dzombe tunaomba ubadilike hata kidogo bac, nchi hii iko pabaya so nyie wenzetu mliepata nafasi tusaidieni ili sauti za kutetea haki zimfikie kila mwenye sikio wa nchi hii.
  Twisukha nguluvi akhutangakhe bheeee.
   
 16. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huo mwongozo unawahusu wanaCCM na siyo vyama vingine, sijawahi ona mwanamke mwenye roho isiyo ya huruma kama huyu
   
 17. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jogi, "Madam" lina maana nyingi, hiyo uliyosema ni moja wapo, kwa maana nyingine linatumika kumu-address mwanamke kiheshima.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  hapana shaka, kwa kuwa huyu mama marito statasi yake inavyosomeka, madam ya danguro inaweza kufit uzuri au vipi!
   
Loading...