Wabunge Wameshtuka; Kumbe Kuna Maisha Nje ya CCM

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,757
71,132
Ni kama mtu aliyekuwa amefunikwa blanket gubigubi wakati kumekucha kisha ulitoe akutane na mwanga ndivyo ilivyotokea kwa wabunge wa CCM Jana baada ya kushuhudia viongozi wa zamani wa chama chao waliojiondoa wakitinga na sura za bashasha, afya njema na bila kinyongo wala hofu.

Ndani ya viunga hivyo vya bunge makundi ya baadhi ya wabunge wa ccm walisikika wakisema "maisha haya ya kujipendekeza na kushindwa kuwa huru mpaka lini? Sasa tusimamie ukweli kama ni kufukuzana potelea mbali."

Wamesema mbona ma PM wanaweza kuiacha ccm sisi ni nani hadi tufie ndani ya moto wakati huko nako maisha ya kawaida yapo?
Kuna walio apa kabisa kuwa wameingia bungeni sio kwa msaada au nguvu ya ccm bali kukubalika kwao na wananchi na kuwa hata wakigombea kwa tiketi ya chama kama TLP watapita tuu.

My Take;
Jee kitendo cha Mbunge wa Shinyanga kumwaga ubuyu kuisema serikali huku akishangiliwa na bunge zima ndio uasi umeanza?
Au uongo wa Jenister Mhagana ambao siku za nyuma ungeshangiliwa lakini Jana ulizomewa ndio mwanzo wa kukataa ukondoo?

Kila la kheri kama mtakuwa mmegundua kuwa nje ya ccm nako kuna maisha, tena yaliyo huru. Hakuna kitu kibaya kama mtu mzima kuishi kama mnafiki na kujipendekeza kiasi cha kushindwa kusimamia ukweli na huku unajua kuwa watu na familia yako wanajua umekuwa mnafiki
 
hata wao wamechoka kuwa wanafki
Hanna kitu kinaumiza ukijua wananchi waliokuamini sasa wanakuona mnafiki.
Na mbaya zaidi mkeo/mumeo na watoto nao wanashangaa umepatwa na nini hadi kuwa mnafiki?
 
Sijaona hoja yao yoyote ya maana au atakuja kuzungumza tena kwa hoja.
 
Kwa mbunge wa ccm ukimsikia anasema ujue anavizia uwaziri pale mwenzake atakapotumbuliwa hawawezi kuamka hawa jamaa. Labda bunge liwe la walimu wa primary kama lilivyokuwa la nyerere
 
Nadhani tatizi wamekatiwa milija ya wizi....walivyozoea naskia mwingine kakamatwa na bunduki za kuwindia mapembe ya mandovu hukooooo
 
Ha ha haa!..wameanza kukataa ukondoo wa kushikishwa akili na mtu.
Amtegemeae mwanadamu amelaaniwa!...
 
Hali ya maisha huku uraiani imekuwa ngumu kupindukia! Ni wajibu sasa kwa Waheshimiwa Wabunge wote bila ya kujali itikadi mkae pamoja muieleze serikali hali halisi ilivyo bila ya woga! Tunataka tuishi kwa raha kwenye nchi yetu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu na sio kuishi Kishetani shetani kwa sababu za kujitakia tu!
 
nakiona kifo cha ccm pale utakapofanyika uteuzi wa sektretariat ya taifa

pale utakapofanyika uteuzi wa makatibu wa mkoa

pale utakapofanyika uteuzi wa makatibu wa wilaya

pale utakapofanyika uchaguzi wa viongozi ndani ya chama,hapa utakuwa msimu wa mavuno kwa takukuru
 
Back
Top Bottom