Wabunge wamepoteza uhalali wa kuwa wawakilishi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wamepoteza uhalali wa kuwa wawakilishi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jul 30, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  BUNGE LIMEKOSA UHALALI WA KUWAWAKILISHA WANANCHI

  Bunge la jamhuri ya Tanzania limekosa uhalali wa kuwatetea watanzania kutokana na baadhi ya sababu zifuatazo;
  1. wabunge kuingia mikataba ya kifisadi na shirika la Taneco kiasi cha kuuza mafuta kwa bei ya juu, kitendo cha wabunge kufanya biashara na tanesco na kutetea mabaya.


  2. kujipandishia mishahara mikubwa huku wafanyakazi wengine tukiendelea kuumia licha ya kazi ngumu tunazofanya kama vile kwalimu, madaktari na wengine. Leo hii wanajifanya wanataka kujadili mgomo wa walimu wanafiki wakubwa! Hadi mgomo uwepo kwani hawajui kuwa walimu tunaishi mazingira magumu mpaka tugome maana ya kuwa na wawakilishi nini?

  Wao wanajipandishia mishahara na marupurupu kwa impact gani waliyo nayo katika jamii, kusinzia?kuunga hoja mkono hata kama ni mbaya? kuibia Serikali. Hivi nimegundua hawna lolote wapo kwa maslahi yao tu. Wanaogopana hata kutajna majina hakika bunge hili halina viwango!

  wanaogopa kutaja majina kwa vile wanafahamiana kuwa na wo hawako safi. Wanatuzingua kama wanasimamia serikali huku wanakula na mashirika ya umma. Wasipowawajibisha wahusika na kuwaondoa bungeni kuna haja ya watanzania kumshinikiza Rais avunje bunge tufanye uchaguzi upya. Japo Rais naye ndiyo walewale. Hivi Tanzania tuna laana gani?

  EE MUNGU TUOKOE NA SERIKALI DHALIMU HII YA CCM!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...