Wabunge waliotangulia mbele za haki bado familia zao zinalipwa posho za vikao vya Bunge.

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nauliza swali hili nikijua kuwa hawalipwi, ila nauliza kutaka kuwaomba wanadamu kuacha kuthamini pesa kuliko afya zao.

Zamani pengo lilikuwa alizibiki ila siku hizi linazibwa Tena kabla ujafika mafumbini.

Ni kweli pesa za vikao viwe vya Bunge au eneo jingine zipo,ila zinalipwa kwa wale walioudhuria kikao tu. Aidha pengo lako kwenye serikali au shirika lako litazibika ila ndani ya familia yako alitozibika.

Kama nafsi yako inakutuma kwenda kazini hata pasipo lazimu wewe nenda, ila Kama kwa mujubu wa majukumu yako na kwa elimu yako unaona kukaa ndani ni salama kwako na familia yako basi kaa ndani uiokoe familia yako.

Mungu amekupa nafasi ya Ubunge au ukurugenzi kwa miaka kadhaa Sasa, naamini uwezo wa kulisha familia unao usiangaike na fedha ukaumiza familia yako aidha kwa kutangulia wewe au kuwatanguliza wao kwa kirusi ulichonunua kwa laki tatu ya kikao.

Panapowezekana kukaa nyumbani na kuchukua taadhari fanya hivyo, usiwaze chama chako wala wadhifa wako maana wapo wenye nyadhifa kubwa tu wamekaa nyumbani kwao kwanini wewe uaminishwe kuwa posho Ni kubwa kuliko uhai wako.

Stay home
 
Huyu mmpe huyu mruke huyu mruke huyu mmpe...haaa hawa ni wapiga kura wangu usiwabomolee..hawa wapo ndani ya hifadhi ya barabara wanabomolewa na hawapewi ata senti tano.
 
Back
Top Bottom