Wabunge waliopitisha budget kwa kura ya ndiyo, majimbo yao yapewe kipaumbele

Sinda69

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
378
218
Ninabaki ninashangaa, Mbunge ametumwa kuwawakilisha watu wa eneo lake, huyu mbunge amekuwepo toka mjadala wa budget unaanza, na amechangia mawazo yake ya kuboresha hiyo bajeti(budget) na mawazo yake yamefanyiwa kazi, yakatumika kuiboresha bajeti (budget).

Imekuja siku ya kuipitisha bajeti huyu mbunge, amepiga kura kuipinga budget isipite.

Humo ndani ya hiyo budget ndimo kutoke fedha ya maendeleo ya jimbo lake lakini kaipinga na haitaki, humo ndo mshahara wake utoke lakini kaikataa.

Hivi huyu mbunge anawakilisha mawazo ya watu wake au anaamua apendavyo?

Mnaweza weka msimamo wa kichama lakini huyu mbunge kasau kwamba maendeleo kimajimbo yanatofautiana, amesahau shida za watu wake.

Ni vizuri sasa ili kutoa funzo kwa wabunge hawa wasiojuwa na wasiojali shida za aliyewatuma, wasipewe kipaumbele katika budget hii. Kipaumbele kiende kwa wale walioikubali.

Na kama mbunge hakuipitishs budget akose manufaa fulani kwa ajili ya jimbo lake na yeye mwenyewe maana ameikataa.

IFIKE MAHALA WABUNGE WAJITAMBUE KWAMBA NI WAWAKILISHI WA MAJIMBO YAO NA SI MATUMBO YAO.

Soma hii kama mtu huru usisome kama mtumwa JIONGEZE.
 
Lakini wanapopinga wana sababu zao na sababu zingine huwa ni za msingi. Pia, inaongeza umakini kwa kuandaa bajeti nzuri kwa kipindi kijacho. Vinginevyo bajeti isiyokosolewa hatuwezi tukajua ubaya wake hasa ukizingatia siyo watu wote wenye utaalamu mambo ya fedha
 
Kondoa , chamwino na mtera pamoja na kuripotiwa kuishi kwa dhiki kubwa iliyofikia hata kula viwavi jeshi mithili ya kunguru mwenye doa jeupe , WABUNGE WAO WANAONGOZA KUGONGA MEZA KUUNGA MKONO BAJETI TANGU BUNGE LA TANGANYIKA HADI LEO TANZANIA .
Ni vema kuheshimu mawazo ya Wapinzani. Rais Magufuli ameonyesha mfano kwa kukubali mawazo ya Wapinzani kuhusu madini na kukataa mawazo ya Chama Tawala ya kupiga meza kuunga mkono mikataba ya kijambazi inayopora mali asili zetu
 
Kondoa , chamwino na mtera pamoja na kuripotiwa kuishi kwa dhiki kubwa iliyofikia hata kula viwavi jeshi mithili ya kunguru mwenye doa jeupe , WABUNGE WAO WANAONGOZA KUGONGA MEZA KUUNGA MKONO BAJETI TANGU BUNGE LA TANGANYIKA HADI LEO TANZANIA .
Ni haki yao kupiga meza kwa sababu serkali sasa imeweka vipaumbele vipya. Zamani mawaziri naxwatendaji naxmawaziri wakuu 4 walitoka, eneo moja shule bwerere hospitali bwerere lami kila mahali navumeme kijijini hadi migombani. Lakini kwa uchoyo wao sasa wameshiba fadhila za CCM wanaitukana baada ya kupanga vipaumbele upya.
 
Uongo utakusaidia nini ? Hivi yale mauaji ya WATAFITI yaliyofanyika karibu na makazi ya waziri mkuu Malecela kwa kisingizio cha wanyonya damu yalitokana na nini ? Jamii inauwa watafiti kwa kisingizio cha uchawi leo hii !

Hii ni aibu ambayo mimi binafsi siwezi kushiriki .
 
Ninabaki ninashangaa, Mbunge ametumwa kuwawakilisha watu wa eneo lake, huyu mbunge amekuwepo toka mjadala wa budget unaanza, na amechangia mawazo yake ya kuboresha hiyo bajeti(budget) na mawazo yake yamefanyiwa kazi, yakatumika kuiboresha bajeti (budget).

Imekuja siku ya kuipitisha bajeti huyu mbunge, amepiga kura kuipinga budget isipite.

Humo ndani ya hiyo budget ndimo kutoke fedha ya maendeleo ya jimbo lake lakini kaipinga na haitaki, humo ndo mshahara wake utoke lakini kaikataa.

Hivi huyu mbunge anawakilisha mawazo ya watu wake au anaamua apendavyo?

Mnaweza weka msimamo wa kichama lakini huyu mbunge kasau kwamba maendeleo kimajimbo yanatofautiana, amesahau shida za watu wake.

Ni vizuri sasa ili kutoa funzo kwa wabunge hawa wasiojuwa na wasiojali shida za aliyewatuma, wasipewe kipaumbele katika budget hii. Kipaumbele kiende kwa wale walioikubali.

Na kama mbunge hakuipitishs budget akose manufaa fulani kwa ajili ya jimbo lake na yeye mwenyewe maana ameikataa.

IFIKE MAHALA WABUNGE WAJITAMBUE KWAMBA NI WAWAKILISHI WA MAJIMBO YAO NA SI MATUMBO YAO.

Soma hii kama mtu huru usisome kama mtumwa JIONGEZE.
Unaonaje pia katika majimbo hayo wafanya biashara waondolewe kwenye mfumo wa kodi?bajeti kutimizwa inategemea na ukusanyaji wa kodi pia.Watu wenye akili finyu kama wewe ndo mnasababisha Tanzania kudumaa.
 
Yaani serikali iache kujenga fly over jimbo la ubungo,barabara za lami makao makuu ya Afrika Mashariki jumbo la Arusha mjini au mji wa kitalii Moshi ipele fedha Kongwa au Mtera kwa kuwa tu wabunge wake waligonga meza? Haitakaa itokee,mtaendelea kunywa maji dimbwi moja na ng'ombe mpaka mtie akili! Ubungo,Kawe,Kinondoni,Kibamba,Arusha,Moshi,Mbeya,Tanga na majimbo mengine ya upinzani yataendelea kupata fedha za bajeti hakuna namba!
 
Miaka yote huwa wanapewa kipaumbele, zikifika zinapelekwa tumboni street, wanaosema hapana zinakwenda kwa shida sana na kutumika kwa ubora mkubwa, ndio kisa kwenye akili wanajua wamchague yupi
 
wenye kumbukumbu NZURI naomba mnisaidie? kura ya HAPANA kwenye siku ya kupitisha bajeti kuu ya serikali ni mara ya kwanza imetokea mwaka huu? swali la pili:mabunge ya nchi zingine kitu kama hiki cha kura ya HAPANA hakuna?
 
Ninabaki ninashangaa, Mbunge ametumwa kuwawakilisha watu wa eneo lake, huyu mbunge amekuwepo toka mjadala wa budget unaanza, na amechangia mawazo yake ya kuboresha hiyo bajeti(budget) na mawazo yake yamefanyiwa kazi, yakatumika kuiboresha bajeti (budget).

Imekuja siku ya kuipitisha bajeti huyu mbunge, amepiga kura kuipinga budget isipite.

Humo ndani ya hiyo budget ndimo kutoke fedha ya maendeleo ya jimbo lake lakini kaipinga na haitaki, humo ndo mshahara wake utoke lakini kaikataa.

Hivi huyu mbunge anawakilisha mawazo ya watu wake au anaamua apendavyo?

Mnaweza weka msimamo wa kichama lakini huyu mbunge kasau kwamba maendeleo kimajimbo yanatofautiana, amesahau shida za watu wake.

Ni vizuri sasa ili kutoa funzo kwa wabunge hawa wasiojuwa na wasiojali shida za aliyewatuma, wasipewe kipaumbele katika budget hii. Kipaumbele kiende kwa wale walioikubali.

Na kama mbunge hakuipitishs budget akose manufaa fulani kwa ajili ya jimbo lake na yeye mwenyewe maana ameikataa.

IFIKE MAHALA WABUNGE WAJITAMBUE KWAMBA NI WAWAKILISHI WA MAJIMBO YAO NA SI MATUMBO YAO.

Soma hii kama mtu huru usisome kama mtumwa JIONGEZE.
Ujinga wetu ndiyo mtaji wao!Wakati unawataka wabunge waliopitisha bajeti wapewe kipaumbele kwenye majimbo yao,usisahau pia wabunge hao hao unaotaka wapendelewe ndiyo walioshiriki hatua kwa hatua kujadili na kupitisha vifungu vya sheria vilivyouza utajili wa Rasilimali zetu.

Nchi yenye watu mbumbumbu wenye matobo kwenye vichwa vyao haiwezi kuendelea,ingekuwa nchi makini leo kusingekuwa na upuuzi wa wendawazimu kuandamana kwa kisingizio cha kuunga mkono kuzuiwa kwa "makinikia", badala yake wangeandamana kuipinga serikali ya ccm iliyowakabidhi kila kitu wawekezaji kupitia sheria zetu mbovu zilizopitishwa na bunge hili hili unaloomba liwapendelee wapiga makofi na wagonga meza wa ccm.

Ni akili zilizovurugwa na vumbi la makinikia tu ndizo ziwezazo kuwaza upuuzi wa kiwango hiki cha lami,hivi hufahamu kuwa bunge letu ndiyo chanzo cha migogoro yote ambayo leo hii inageuzwa kuwa sababu ya watu kuimba " Ritania za sifa na utukufu"kwa anayeonekana mtetezi wa Rasilimali wakati na yeye alikuwa sehemu ya cabinet na bunge lililopitisha na kuridhia upumbavu huu unaolitafuna Taifa?

Kwa kupitia bungeni,miswada yote ya uwekezaji ama ilipitishwa kwa mbinu chafu au kwa hati za dharura,kisha bunge hilohilo lililokosa aibu eti linaunda kamati ya kuandaa pongezi kwa rais wakati utumbo wote unaolitafuna Taifa ulipitia bungeni.

Endeleeni za uzezeta wenu,watu makini hawaipingi bajeti eti kwa sababu wana nia mbaya,wanajaribu kufanya hivyo ili kuihimiza serikali iwe na vipaumbele sahihi vya kibajeti vinavyoweza kuleta tija kwa mwananchi wa kawaida,uchovu wa fikra wa watu wa aina yako ndiyo unaowafanya msitambue nia njema ya wapinzani wanapopinga mambo ambayo hayana tija kwa Taifa.Wapinzani waliipinga mikataba yote ya madini,leo hii kwa kiburi cha kutowasikiliza serikali inapambana na wawekezaji kwa kugombea "vumbi la makinikia" kwa mikataba iliyosainiwa na serikali yenyewe huku bunge likimtimua Mh.Zitto aliyekuwa anaupinga mkataba wa Buzwagi/ACACIA uliosainiwa hotelini London
 
Mtu unaamka na mning'inio wa mataputapu ya jana, unkuja kusema mawazo ya wabunge yameboresha bajeti!!
Mtukufu anajua kila kitu na alikwisha toa million kumi kumi kwa wabunge wake wapitishe chochote atakacho.,hakuna cha kushauri lolote
Unadhani kuna wa kumwambia asinunue "dream liner aongeze bajeti ya pembejeo?
 
Mambo hubadirika na twaweza kuwa waanzilishi wakafuata hao wa mabunge mengine. Kutounga mkono budget ulioshiriki kuitengeneza una maana gani.
 
You have missed the point bro ongelea budget.
 
Ni haki yao kupiga meza kwa sababu serkali sasa imeweka vipaumbele vipya. Zamani mawaziri naxwatendaji naxmawaziri wakuu 4 walitoka, eneo moja shule bwerere hospitali bwerere lami kila mahali navumeme kijijini hadi migombani. Lakini kwa uchoyo wao sasa wameshiba fadhila za CCM wanaitukana baada ya kupanga vipaumbele upya.
....Hivi bajeti iliyopita utekelezaji asilimia ngapi vile?
 
Mtu unaamka na mning'inio wa mataputapu ya jana, unkuja kusema mawazo ya wabunge yameboresha bajeti!!
Mtukufu anajua kila kitu na alikwisha toa million kumi kumi kwa wabunge wake wapitishe chochote atakacho.,hakuna cha kushauri lolote
Unadhani kuna wa kumwambia asinunue "dream liner aongeze bajeti ya pembejeo?
Uelewa wako ni mdogo nenda shule kwanza hoja hii siyo size yako
 
Ninabaki ninashangaa, Mbunge ametumwa kuwawakilisha watu wa eneo lake, huyu mbunge amekuwepo toka mjadala wa budget unaanza, na amechangia mawazo yake ya kuboresha hiyo bajeti(budget) na mawazo yake yamefanyiwa kazi, yakatumika kuiboresha bajeti (budget).

Imekuja siku ya kuipitisha bajeti huyu mbunge, amepiga kura kuipinga budget isipite.

Humo ndani ya hiyo budget ndimo kutoke fedha ya maendeleo ya jimbo lake lakini kaipinga na haitaki, humo ndo mshahara wake utoke lakini kaikataa.

Hivi huyu mbunge anawakilisha mawazo ya watu wake au anaamua apendavyo?

Mnaweza weka msimamo wa kichama lakini huyu mbunge kasau kwamba maendeleo kimajimbo yanatofautiana, amesahau shida za watu wake.

Ni vizuri sasa ili kutoa funzo kwa wabunge hawa wasiojuwa na wasiojali shida za aliyewatuma, wasipewe kipaumbele katika budget hii. Kipaumbele kiende kwa wale walioikubali.

Na kama mbunge hakuipitishs budget akose manufaa fulani kwa ajili ya jimbo lake na yeye mwenyewe maana ameikataa.

IFIKE MAHALA WABUNGE WAJITAMBUE KWAMBA NI WAWAKILISHI WA MAJIMBO YAO NA SI MATUMBO YAO.

Soma hii kama mtu huru usisome kama mtumwa JIONGEZE.
Hovyooooo
 
Back
Top Bottom