Wabunge waliopitia JKT kwa mujibu wa sheria ni wazalendo zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waliopitia JKT kwa mujibu wa sheria ni wazalendo zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by capito, Jun 21, 2012.

 1. capito

  capito JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Katika kipindi cha Baragumu (majadiliano) kinachorushwa na Channel 10 leo asubuhi kulikuwa na mjadala kuhusu suala la vijana wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria.
  Wengi waliochangia walisema JKT itasaidia kuongeza uzalendo kwa vijana.
  Kwa upande wangu nimekuwa na mtizamo tofauti kuhusiana na hili suala la JKT kuongeza uzalendo katika kipindi hiki tulichopo ambapo matumizi ya mali ya umma si mazuri labda iliwezekana enzi zile za mwalimu.
  Katika nchi ambayo ni corrupt kama yetu ukiamua kuwa mzalendo unaonekana mbaya na baadhi wanakubeza.

  Tuchukue mfano wa mijadala ya bunge la budget inayoendelea kwa sasa huko Dodoma. Je, mijadala na michango ya budget imesaidia kuonesha kweli kwamba kupitia JKT kunasaidia kuongeza uzalendo?

  Kati ya wabunge wengi vijana hasa wa upinzani ambao hawakupitia JKT kwa mujibu wa sheria na wabunge wazee waliopitia JKT ni nani wamekuwa na michango yenye masilahi kwa nchi na hivyo kuwa na uzalendo zaidi?

  Malumbano yaliyolipotiwa na gazeti la Mwananchi la jana kati ya Esther Bulaya na Steven Wassira yanatoa picha gani kuhusu uhusiano wa JKT na uzalendo? Steven Wassira ambae nadhani amesoma enzi za JKT alimhoji Esther Bulaya kwa nini amekataa kuunga mkono budget.

  Je, kuunga mkono budget hata kama haina masilahi kwa taifa ndio uzalendo? na kati ya hawa wawili nani mzalendo?

  Nadhani kama kuna vipaumbele vingine vyenye tija kwa taifa tungepeleka hizo hela tunazotaka kuzitumia kwa kuwapeleka watu JKT, uzalendo hauwezi kuletwa na JKT kama matumizi mabaya ya mali ya umma bila vipaumbele yataachwa yaendelee.
   
 2. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi mkuu!
   
 3. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  well said;
  1.JKT ya miezi 6/mwaka mmoja haiwezi kuleta uzalendo kwa vijana;mfano wote waliohusika na ufisadi wa nchi hii wamepitia JKT na wamesomeshwa bure.
  2.Malezi mazuri kuanzia utotoni kutoka kwa wazazi,walimu,jamii na serikali ndio inaweza kuleta uzalendo.
   
Loading...