Wabunge waliokataa "kutoka" wafukuzwe/waonywe na Chadema kwa msimamo wake?

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
0
Samahani wanaJF Heading imebadilishwa ambayo haiendani na maudhui niliyokusudia sitaki kuonekana mbabaishaji post nimeifuta.
 
Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
1,195
Nashukuru Facts 1 kwa kuanzisha suala hili, binafsi muda mrefu nimeuangalia mwenendo wa Zito Kabwe ulibadilika tangu alipoteuliwa wakati ule na Kikwete kama mjumbe wa kamati ya madini. Zito Kabwe sio yule tena tuliyemfahamu alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza, ambaye hata wakati mwingine alisimamishwa kwa muda akisimamia anachoamini, akitetea haki ya wanyonge bila kutetereka.

Zito tuliyemfahamu alikuwa kweli mtetezi wawanyonge, mtetezi wa tz kwa ujumla.

Ila Zito anayejitokeza, aliyejitokeza siku za karibuni ni tofauti, kuna kitu kinaendelea.

Kama kuna mtu wa kwanza atakayeivuruga Chadema na harakati za ukombozi wa watanzania nisingesita kusema atakuwa Zito Zuberi Kabwe. Matukio mbali mbali yanadhihirisha hilo.

Alikuwa mpiganaji hodari wa wananchi, lakini sijui ameingiwa na nini. Yuko kiccm ccm vile.
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,229
2,000
HAPANA mm naona yeye ni mkweli kuliko wale walionyamaza na hawakuhudhuria tukio la kutoisikiliza hotuba wafanyweje? kama Shibuda, Mnyika, Mdee, Ndesamburo na mkwewe pia na bintiye na wengine.
ZITTO Bunge lililopita ameitetea Nchi sana yeye na Wangwe na Dr Slaa licha ya kupinga Posho na Mishahara alisimamia tume za urekebishaji Madini, hesabu za Umma n.k. kijana abaki ni kawaida ya Waha na Wamanyema bila yeye ....................
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,721
2,000
Nadhani hili ni swala la wao wenyewe kwa wenyewe huko CHADEMA. Unajua kumfukuza mwanachama usiyekubaliana naye siyo jawabu kabisa kisiasa kwa sababu unajikosesha advantage ya kujua upande wa pili wa mtazamo wako, jawabu sahihi ni kwa CHADEMA kujenga utaratibu wa kuwa wawazi na kuondoa kuwepo kwa kitu kama "taarifa za siri." Vile vile chama kijijenga kumu-accommodate kila mwanachama. Siku zote uwepo wa taarifa za siri unaweza unasababisha mgawanyiko ndani ya chama kwa vile inawezekana wengine wasizione taarifa hizo kama ni siri.
 
Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
0
Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".
MKJJ nakubaliana na wewe kuwa katika kujenga demokrasia lazima kuwe na uhuru wa kutofautiana kimawazo hasa ndani ya chama, lakini uhuru bila mipaka ni fujo. Sikatai Zitto kutofautiana kimawazo lakini yeye kama kiongozi hata kama si kiongozi hawezi kuwa anatoa siri za chama nje bila kuwasiliana na viongozi wenzake. Ningekuwa mimi nimesema kuwa kuliwa na kutofautiana kwenye maamuzi hata kama ni kweli uzito hauwezi kulingana wa kiongozi kama yeye hasa ukizingati swala tete kama hili.
 
Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
0
MODS heading uliyoiweka haiendani kabisa na maudhui niliyokusudia, mtu akisoma heading na kukuta kitu tofauti wa kupuuzwa ni mimi siyo wewe MODS. Ningeshauri kama haiwezekani kurudisha heading ya mwanzo jaribu kuangalia heading nyingine iendane na maudhui yaliyopo au kama haiwezekani kabisa bora ifute thread nzima, kwa sababu lengo la heading uliyoiweka ni kunigombanisha na watu wengi wakati si lengo langu. Asante. Heading yangu ilisomeka
Petition Zitto afukuzwe Chadema

Ninazo sababu;

Ingawa yeye na baadhi ya watu wanamtetea kuwa hizo ni njama za CCM lakini kuna matukio anayoyasababisha yeye mwenye ama kwa makusudi au kwa kutokujua ambayo huwezi kuisingizia CCM.

Hizi ni baadhi ya sababu zilizonifanya nifikie uamuzi huu mgumu:

Kwenye sakata la ama kununuliwa au kutonunuliwa kwa mitambo ya Dowans Zitto alitofautiana na msimamo wa viongozi wake na msimamo wa Chadema kwa ujumla.

Huku akijua kuchukua form na kugombea uenyekiti kungesababisha mgogoro mkubwa wakati wa uchaguzi wa ndani wa Mwenyekiti, Zitto alionyesha waziwazi mbele ya vyombo vya habari kutoridhishwa na uamzi wa wazee wa chama kuombwa kujitoa kiasi cha kusababisha kuzaliwa kwa makundi mawili ndani ya chama.

Kutofanyika kwa chaguzi za ndani za Baraza la vijana BAVICHA na Baraza la wanawake BAWACHA inasemekana mkono wa Zitto pia ulihusika kiasi cha kuleta makundi na chaguzi kusimamishwa.

Wakati chama kikiendelea na kampeni mwaka huu Zitto alisikika akisema uchaguzi ujao atagombea urais huku akijua kitendo hicho kingetumiwa na wapinzani kuwagombanisha na wapiga kura.

Zitto amekuwa akipinga maamuzi mengi ya chama waziwazi kiasi cha kuleta minong'ono ndani na nje ya chama. Ingawa ana uhuru na utashi wake lakini yeye kama kiongozi anatakiwa atoe ubinafsi na kuweka chama mbele, mfano kupinga uamuzi wa chama kuwasimamisha kina Kafulila na wenzake.

Zitto amekuwa akiongea habari za chama zingine za siri kwenye vyombo mbalimbali vya habari mfano kutumia FACEBOOK bila kujali utaratibu uliowekwa na chama.

Leo ameongea siri za chama kuhusu upigaji kura wa ama kususia hotuba ya rais au la bila kuangalia athari zitakazosababishwa na kitendo chake hicho.

Kwa sababu hizi na zingine ambazo ni siri ya chama; ili kukinusuru chama na mgawanyiko unaoweza kutokea naomba kupendekeza yafuatayo:

1. Chama kimuonye Mh. Zitto aache tabia yake hiyo inayokishushia heshima chama. AMA
2. Zitto anyang'anywe vyeo vyake vya juu vya chama hadi hapo atakapojirekebisha(kukomaa). AU
3. Ili kukilinda chama kisigawanyike kabla ya uchaguzi mkuu ujao chama kichukue uamuzi mgumu (mapema) wa kumsimamisha Zitto uanachama. Ni bora kupoteza jimbo moja kuliko kupoteza chama kizima kinachotegemewa kuleta mapinduzi Tanzania.

Naomba kutoa hoja.
 
mambomengi

JF-Expert Member
May 16, 2009
829
250
Huyu bwana anang'ata na kupuliza. Nilifikiri angeweza kuwa Rais wangu, hakika ni mganga njaa kama wengine. Muda utatueleza amesimamia nini. Samahani.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
681
500
Jamani Zitto yuko sahihi kama amefanya mambo yale kwa utashi binafsi ingawa kuongea hadharani hajakitendea chama chake haki na watajuana huko kwa mujibu wa kanuni na katiba za chama. Ila ombi langu kwake asije akawafanya watu wa Kigoma kama alivyofanya Dr. Amani Kaburu ambaye amekufa kisiasa tayari, Akifanya mchezo ccm wanaajua kununua na kuua kisiasa kama alivyokwisha Masumbuka Lamwai na wengine kibao mnawajua.
 
zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,299
2,000
sioni sababu ya yeye kupewa muda, asimamishwe tu ndo itakuwa muarobaini wa mgawanyiko ndani ya CHADEMA, sitashangaa kusikia zitto kateuliwa kuwa waziri ndani ya serikali ya JK km ishara ya JK kushirikisha upinzani kwenye serikali yake.
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,862
0
Kwa wasiofahamu ccm imefikia kuwa chama cha kidikteta kwa sababu ya kuzuia sauti yenye msimamo kinzani ndani ya chama. Mimi nilikuwa mwanachama wa ccm na nilikitumikia kwa moyo wangu wote. Lakini mwaka 2006 niliwarejeshea kadi yao baada ya kubaini udikteta mkubwa ndani ya chama hicho. Kwa ufupi, kwenye vikao vya ccm ukitofautiana na msimamo wa wakubwa basi wewe unatazamwa kama muasi na unaweza kuanza kuandamwa kama adui.

Bado sijajiunga na chama chochote cha siasa lakini kwa utafiti wangu binafsi naelekea kushawishika kujiunga na CDM. Ninaamini ndani ya CDM kuna demokrasia ambapo mojawapo ya ishara zake ni kuruhusu mawazo kinzani. Naamini kuwa CDM inaheshimu wanachama wenye mawazo tofauti na haiwachukulii kuwa ni maadui. Na kama haifanyi hivyo, basi nitumie fursa hii kuwashauri waanze mara moja. Kama mhe. Zitto Kabwe amekuwa akitofautiana sana na viongozi wengine kwenye vikao vya chama, basi wachukulie kuwa hiyo ndiyo demokrasia. Muhimu hapa ni kuheshimu maamuzi ya chama kupitia vikao vyake halali. Hata kama wanachama kadhaa wanapinga suala fulani lakini kura zikipigwa na kuonekana wengi wanaunga mkono, basi huo unachukuliwa kuwa ndiyo msimamo wa chama na ndiyo unaopaswa kuheshimiwa na wanachama wote.
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
14,827
2,000
Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".

Ukubwa dawa!! na maneno yanapotoka kwa gulu kama wewe yanafurahisha zaidi! kitu ambacho hakitakwi ccm, kinakaribishwa chadema!!! eti wanachama millioni 5 wa ccm wote walisema na kukubaliana JK pekee ndiye achukue form ya kugombea urais! what a shame! demokrasia ni pamoja na hayo! kuanzia nyumbani unamulika mpaka nje!

Kwa wasiofahamu ccm imefikia kuwa chama cha kidikteta kwa sababu ya kuzuia sauti yenye msimamo kinzani ndani ya chama. Mimi nilikuwa mwanachama wa ccm na nilikitumikia kwa moyo wangu wote. Lakini mwaka 2006 niliwarejeshea kadi yao baada ya kubaini udikteta mkubwa ndani ya chama hicho. Kwa ufupi, kwenye vikao vya ccm ukitofautiana na msimamo wa wakubwa basi wewe unatazamwa kama muasi na unaweza kuanza kuandamwa kama adui.

Bado sijajiunga na chama chochote cha siasa lakini kwa utafiti wangu binafsi naelekea kushawishika kujiunga na CDM. Ninaamini ndani ya CDM kuna demokrasia ambapo mojawapo ya ishara zake ni kuruhusu mawazo kinzani. Naamini kuwa CDM inaheshimu wanachama wenye mawazo tofauti na haiwachukulii kuwa ni maadui. Na kama haifanyi hivyo, basi nitumie fursa hii kuwashauri waanze mara moja. Kama mhe. Zitto Kabwe amekuwa akitofautiana sana na viongozi wengine kwenye vikao vya chama, basi wachukulie kuwa hiyo ndiyo demokrasia. Muhimu hapa ni kuheshimu maamuzi ya chama kupitia vikao vyake halali. Hata kama wanachama kadhaa wanapinga suala fulani lakini kura zikipigwa na kuonekana wengi wanaunga mkono, basi huo unachukuliwa kuwa ndiyo msimamo wa chama na ndiyo unaopaswa kuheshimiwa na wanachama wote.

well said! niliwahi kuwaambia watu Zitto anaishi miaka 50 mbele zaidi! mtu anatoa mawazo asimamishwe bila kujua position ya zito ni hipi, na mpaka anasema yeye si mtoto! aliwaza yote haya ya kusema kuwa ni mnafiki, kanunuliwa n.k.......

CHADEMA members kwa mawazo yenu haya mnajishushia hadhi bila kujua, bado chadema ina makovu mengi ya kuibaka demokrasia within chama, hili liangaliwe sana tena kwa vitendo!!!

tunahitaji katiba mpya na tume huru, kama Zitto yuko kinyume na hili, then fanyeni mnayotaka, lakini kama tu nikutofautiana jinsi ya kupata hizi changes then needs deper discussion, wengi wana chadema pia hawajasupport kwa chadema kutoka bungeni! zitto naye ni mmojawapo, mnataka sauti zao zisikike wapi??

leadership maturity ni ku-aacomodate watu wa aina hii, na kama uongozi wa chadema umemuelewa zitto pas kufanya any damaging move, then they are matured, I believe they have been like that!

msiwasikilize hawa members ambao kwa kauli zenu wanaweza wakawa sisimizi tu!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
...Kuhusu uamuzi wa baadhi ya wabunge wa Chadema kutokutoka na wenzao ninaamini ni haki yao kabisa - kwani mimi ninaamini katika dissent ya wananchi bila kumlamizisha mtu afuate au asimamie kile dhamira yake inapinga. Lakini naamini ni msimamo wa makosa; kwa kutokuungana na chama chao wabunge hao wanasema kuwa matokeo ya Urais hayakuwa na tatizo lolote na hivyo kwa vile ni rasmi basi ni lazima yakubaliwe, lakini vile vile ni wa makosa kwa sababu kama habari ni kweli kwamba ilipigwa kura na wengi wakashinda basi wale walioshindwa walitakiwa wakubali uamuzi wa wenzao na kuusimamia.

Ukiangalia ndicho hicho hicho wanachotaka Watanzania wakubali "uamuzi wa wengi" kwenye uchaguzi wa Rais sivyo? Si wanasema JK kashinda kwa asilimia 61 hivi na kuwa uamuzi huo wa wengi uheshimiwe na watu wasiupinge? Sasa iweje wao baada ya kupiga kura na wengi wameshinda wao wenyewe wakageuka na kupinga uamuzi wa wengi katika jambo ambalo wenzao wanapinga uamuzi wa wengi vile vile? Nadhani ni mtego kwa wabunge hao! kwani kama kweli walikuwa hawakubaliani na chama chao (ambayo ni haki yao) wangeenda Bungeni wakati wenzao wananyanyuka wao wangekaa chini na kumpigia makofi Rais na hivyo kuonesha kuwa wanamtambua, wanakubali matokeo yalivyotokea na hawana tatizo na mfumo uliopo. Lakini kama wana matatizo na mfumo uliopo na matokeo ya Kura yalivyofanyika kwenye nafasi ya urais, walikuwa na uchaguzi mmoja tu ambao ulikubaliwa na chama. (Kutoka Facebook yangu)
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,966
2,000
Mods kubadilisha Heading ni udikteta.
Na mbaya zaidi mwanzisha mada mwenyewe hakubaliani na heading uliyoiweka.
Kama vp Mod si ungeanzisha thread yako yenye heading unayoitaka wewe!

Sioni maana ya ile slogan "...we are dare to talk openly"
 
Deo

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
1,218
1,250
icon1.gif
Re: Petition Zitto afukuzwe Chadema

Afukuzwe
 
nsami

Senior Member
Jun 11, 2010
175
0
MKJJ nakubaliana na wewe kuwa katika kujenga demokrasia lazima kuwe na uhuru wa kutofautiana kimawazo hasa ndani ya chama, lakini uhuru bila mipaka ni fujo. Sikatai Zitto kutofautiana kimawazo lakini yeye kama kiongozi hata kama si kiongozi hawezi kuwa anatoa siri za chama nje bila kuwasiliana na viongozi wenzake. Ningekuwa mimi nimesema kuwa kuliwa na kutofautiana kwenye maamuzi hata kama ni kweli uzito hauwezi kulingana wa kiongozi kama yeye hasa ukizingati swala tete kama hili.

Fact 1, tuko pamoja ktk hili!
Bado zito hawezi kukwepa lawama za usaliti katika hili. Zito ni kiongozi ktk chama na suala hili naamini halikuanzia na kufikia muafaka dk chache tu walizokuwa bungeni.

Zito alikuwa na nafasi nzuri ya kulipinga kwa mtizamo wake ndani ya vikao vya chama wakati suala hilo likiwa under discussion!

Ama alifanya hivyo akashindwa na wengi waliokubaliana nalo au hakufanya hivyo sijui, ila kama suala limeshafikia uamuzi hata kama unatofautiana na mawazo yake binafsi alipaswa kuachana na individual difference azungumzie msimamo wa chama. Lolote nje ya hilo ni FUJO na kujiona ni maarufu kuliko CHAMA.
 
kipipili

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
1,590
1,250
mbona wabunge wote wa chadema waliokuwepo bungeni walitoka. ambao hawakuwepo hakuna cha kuwafanya ndiyo demokrasia hiyo. wangekuwepo then wasitoke hiyo ingekuwa issus nyingine.kalas
 
engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
tuwape mda watatuwe mambo yao tusiwe na haraka(没问题)
mapinduziiiiiiii daimaaaaaaaaa
 
Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,945
2,000
MODS heading uliyoiweka haiendani kabisa na maudhui niliyokusudia, mtu akisoma heading na kukuta kitu tofauti wa kupuuzwa ni mimi siyo wewe MODS. Ningeshauri kama haiwezekani kurudisha heading ya mwanzo jaribu kuangalia heading nyingine iendane na maudhui yaliyopo au kama haiwezekani kabisa bora ifute thread nzima, kwa sababu lengo la heading uliyoiweka ni kunigombanisha na watu wengi wakati si lengo langu. Asante. Heading yangu ilisomeka

Nakupa big up?
Heading ya mwanzo ndiyo yenye kuwakilishwa yaliyomo kwenye hoja.Mods kabda ya kubadili heading labda ingekuwa bora kufanya consultation na mweye thread!
Yote ni yote message sent.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom