Wabunge waliogongana Richmond warudishwe- Mzee Mwanakijiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waliogongana Richmond warudishwe- Mzee Mwanakijiji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Aug 4, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  M. M. Mwanakijiji

  JUZI Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipiga kura ili kuanza mchakato wa kujua ni kina nani watakuwa wagombea wa chama hicho kwenye nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge kwa kipindi kijacho cha miaka mitano.

  Hii ni hatua ya awali kabla ya majina ya washindi kufikishwa kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ambavyo vina uwezo wa kupindua matokeo kwa kadiri ya utashi wao.

  Mamia ya wana CCM watajitokeza kupiga kura ili kutoa mapendekezo yao katika utaratibu wa kura za maoni ambapo wanachama mbalimbali wamejitokeza kugombea wengine ikiwa ni marudio na wengine ikiwa ni mara ya kwanza.

  Tukiondoa taarifa za matokeo ambazo tumezisikia hasa wiki hii iliyopita, hasa mazingaombwe ya TAKUKURU na wale wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, masikio ya wachunguzi wengi wa kisiasa nchini yanabakia katika kundi la watu wachache ndani ya CCM ambao kwa takriban miaka miwili sasa limekuwa katika mgongano mkubwa.

  Tayari matokeo yanaonyesha kwamba baadhi wameanguka kama Lucas Selelii, James Lembeli, Alocy Kimaro na wengine. Hili kundi ambalo lilijikuta linakipasua Chama Cha Mapinduzi kufuatia sakatala la kashfa ya Richmond na masuala mengine ya ufisadi.

  Kufuatia sakata hilo la Richmond na baadaye suala la Rais mstaafu Mkapa na mgodi wa Kiwira wana CCM walijikuta wakigawanywa na kuwa na makundi makubwa mawili.

  Wale ambao wanaamini aliyekuwa waziri mkuu ambaye alijiuzulu kufuatia kuhusishwa na kashfa ya Richmond kuwa alionewa na wale ambao wanaamini kabisa kuwa Kamati Teule ilimwonea waziri huyo mkuu kwa kutompa nafasi ya "kujitetea".

  Mpasuko huo ukatiwa nguvu na mpasuko wa kundi la wabunge ambao waliamini kuwa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa alitumia madaraka vibaya pale alipodaiwa kujipatia mgodi wa Kiwira yeye, familia yake na watu wake wengine wa karibu.

  Suala hilo la kujipatia mgodi kinyemela liliwafanya baadhi ya wabunge kudai kuwa rais huyo mstaafu avuliwe kinga ili hatimaye aweze kulazimishwa kujibu mashitaka katika mahakama ya sheria.

  Kati ya masuala hayo mawili yakaibuka masuala mengine yatokanayo na hayo hasa pale ambapo vyombo mbalimbali vya habari vilipojikuta vinalazimishwa kuchukua upande, aidha kwa sababu za kiitikadi au vikiwa vinasukumwa na wamiliki wake au na watu wenye maslahi ya kifedha na vyombo hivyo, kiasi kwamba mgongano wa kisiasa ulivuka mipaka na kuwa mgongano wa binafsi katika ya makundi mbalimbali ya waandishi wa habari, wanasiasa, wafanyabiashara na kulazimisha jamii vile vile kuwa na pande mbili kuhusiana na masuala hayo.

  Kinyume na ambavyo ilitarajiwa kwamba hatimaye mpasuko huo wa kimaslahi ndani ya CCM ungesababisha kundi moja kujitoa hali halisi ni kuwa siku ya leo imefika huku makundi yote mawili yakiwa na mashabiki na wapambe wake yakiwa yameshikana pembe kama ng'ombe wagombanao na hakuna aliye tayari kumuachia mwingine.

  Ukiondoa kujiondoa kwa mmoja wa kundi hilo Fred Mpendazoe ambaye alijiunga na CCJ na baadaye CHADEMA, makundi yote mawili yameonekana kujitokeza kugombea tena nafasi za ubunge.

  Katika kipindi hiki kilichopita kundi moja lile linalojulikana kuwa la "wapiganaji CCM" limekuwa likilalamika kuwa kundi jingine la "mafisadi" limekuwa likijaribu likitumia mbinu mbalimbali ili kufanya wanachama hao wa kundi la kwanza kushindwa katika chaguzi za ndani za CCM na kuwa wasipate nafasi ya kuweza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.

  Hapo awali kauli hizo zimekuwa zikipuuzwa na vyombo vya dola na hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kuonyesha ushahidi wowote kuwa kumekuwa na mchezo mchafu kwenye majimbo mbalimbali zaidi ya tuhuma tu.

  Hata pale ambapo baadhi ya watu wametuhumiwa kuwa wametumwa na mafisadi kugombea ukweli unabakia kuwa hakuna ushahidi wowote aidha wa maandishi, picha, sauti, au vielelezo vingine ambao umeweza kutolewa kushawishi jamii kuwa kumekuwa na mchezo mchafu.

  Japo hakuna ushahidi wa hilo haina maana jambo hilo halikuwepo. Tukichukulia taarifa za watu mbalimbali kukamatwa katika matukio mbalimbali yanayotajwa kuwa na mazingira ya rushwa wiki iliyopita ni wazi kuwa aidha kuna mtu anachezea akili za taifa zima au tuna vyombo vibovu kabisa vya kusimamia sheria.

  Inashangaza kuwa baada ya taarifa ya "kamata kamata" ya wiki iliyopita hadi leo siku ya uchaguzi hakuna mtu hata mm ambaye amefikishwa mahakamani kwa kosa lolote la kutoa au kupokea rushwa na wote wameachwa (hata wale tulioambiwa wamehojiwa usiku kucha) kushiriki uchaguzi.

  Hivyo basi, kama TAKUKURU, Polisi na wale wenye kuwaamuru wameona kuwa makosa yote ambayo yamefanyika hayakuwa na ushahidi mzito wa kumpeleka mtu yeyote mahakamani na hivyo kuwaacha wagombea wagombee na kupigiwa kura basi ni budi niseme kwamba jaribio lolote la kuleta mashtaka baada ya kura za maoni ni upotoshaji mkubwa wa demokrasia na ni kuchezea utawala wa sheria.

  Ninachosema ni kuwa TAKUKURU na Polisi wasiwachezee Watanzania kwa kujaribu kuvuruga mchakato wa kuwapata wagombea ndani ya CCM hasa kwa kutoa taarifa kwa kamati mbalimbali za CCM kuwa fulani na fulani alifanya hivi na vile wakati wa kura za maoni.

  Hilo likishaeleweka hatuna kukubali jambo jingine ambalo ni muhimu kuwa wale wabunge wote ambao waligongana Bungeni kwenye masuala ya Richmond, Mkapa na Kiwira wana CCM wataona ni bora wawarudishe tena bungeni.

  Ninaamini kabisa kuwa itakuwa ni makosa makubwa kwa wana CCM kutowarudisha wabunge hao wote kwani kwa kufanya hivyo kutawapa ushindi kundi moja nje ya Bunge.

  Binafsi sipendi ushindi wa mezani. Kwa vile CCM imeshindwa kutafuta suluhu ya makundi haya licha ya kuundwa kwa kamati ya Mzee Mwinyi, basi kujaribu kutafuta suluhu nje ya Bunge litakuwa ni kosa kubwa zaidi.

  Fikiria kwamba Bunge lijalo linakuja halafu Lembeli na Selelii wametupwa nje, huku Rostam na Lowassa wakiwa wameingia tena (kama inatokea) je, hawatotumia nafasi zao bungeni kuhakikisha "wabaya wao" wanashughulikiwa na hata kutumia mtindo wa Kamati Teule kuweza kujisafisha zaidi?

  Japo hilo ni jambo zuri kwa upande mmoja mimi ninaamini tusiyaachie haya makundi mawili yakwepane.

  Wana CCM wana jukumu la kuwarudisha wabunge wote waliohusika na masuala haya bungeni ili wakamalizane bungeni kwani hakuna atakayepewa ushindi wa chee.

  Kwa vile suala hili lilianzia bungeni ni lazima liishie bungeni na hakuna ujanja wa njia za mkato. Ninaamini wale wagombea wengine waliojitokeza katika majimbo ya wabunge hawa watakuwa ni wasindikizaji wazuri na wametoa changamoto nzuri lakini wana CCM watatambua kuwa kinachogombaniwa ni zaidi ya majimbo ya kisiasa.

  Wananchi katika majimbo yote yenye wabunge hawa wapambanaji na wale wenye kulaumiwa watatambua kuwa suala ambalo limelikabili taifa kwa miaka hii miwili ni kubwa mno kiasi kwamba kama ingekuwa ni mechi ya soka basi ningeweza kusema kilichopita ni kipindi cha kwanza tu. Katika kipindi hicho timu moja imefungwa magoli mawili.

  Wana CCM kwenye kura za maoni wamefanya makosa makubwa kuamua kuwaondoa wachezeaji uwanjani badala ya kuja na kumaliza kipindi cha pili ati kwa vile wameonewa na kufungwa mabao mawili.

  Timu yenye akili ni ile inayokuja kwenye kipindi cha pili kwa nguvu zaidi na mbinu mpya ili kujibu mashambulizi huku ile timu nyingine nayo ikijipanga vizuri zaidi kulinda magoli yao na ikibidi kuongeza mengine.

  Ni kwa sababu hiyo ninaamini wabunge wafuatao warudishwe bungeni ili wakamalizie mechi yao kwani katika Tanzania ya leo, hakuna ushindi wa chee au wa kubebwa.

  Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga), Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Lucas Selelii (Nzega), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Said Juma Nkumba (Sikonge). NEC ifanyie taifa hisani kwa kurudisha kundi hili zima bungeni ili wakamalizie mechi waliyoianzisha.

  Jaribio lolote la taratibu za kichama kumwengua yeyote hapo ni kujaribu kuipatia timu moja ushindi wa mezani. Tuwaache wote hawa warudi wakagongane tena huko bungeni au wakapatane. Ushindi wa chee hakuna.


  My take..
  Sikubaliani na hoja ya Mwanakijiji kwa sababu zifuatazo;

  1.Wapambanaji wa ufisadi wako wengi tu na wengine tunaingia hivi karibuni
  2.Kutoka kwa hawa waliotemwa kwenye kura za maoni ni firsa kwa CHADEMA kwenye majimbo husika
  3.Waliotoswa wanaweza kujiunga naCHADEMA na wakashinda kwenye majimbo yao ambapo wao wataonekana wana nguvu kuliko wagombea wa CHADEMA. Mfano kwa Selelii
  4.Ni Mwanakijiji huyu huyu aliyekuwa ameandika kuhusu CHADEMA toka hapa kwenda pale akisisitiza kuwa ili demokrasia iwe demokrasia basi kura za maoni lazima ziheshimiwe leo anataka NEC itende hisani,sikuelewi Mwanakijiji,Demokrasia uliyokuwa unaitaka iweje sasa ivunje kwakuwa unataka kina Kimaro warudi Bungeni?

  Inakuwaje mti mmoja unatoa maji matamu na machungu? Au sijakuelewa? Ndio maana mimi nilipingana sana na hoja zako nyingi kwamba zilikuwa hazitekelezeki.

  Ndugu endelea kuwa na msimamo wako wa kutetea kura za maoni za wananchi bila kuathiriwa na vikao vingine vya ngazi ya juu..

  Habari ndio hiyo..
   
 2. m

  mbarbaig Senior Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Acha reality iwe hivyo...nadhani utagundua nadharia zako zitabaki kuwa nadharia....Acha wenye ushawishi na wale ambao wanaheshimu kura za maoni waendelee...endelea na nadharia zako
   
 3. I

  IronLady Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh hii kali...
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wanapaswa kwa hali yeyote kurudi bungeni na hasa wale waliokua wanapambana na ufisadi. Sasa kosa lao ni moja, walikua wanapambana na serikali ya ccm hivyo wasitarajie huruma ya upendeleo kutoka kwa adui. Milango iko wazi kwa vyama pinzani kuwasimamisha katika majimbo yao, ila wasichelewe kuchangamkia hiyo fursa.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu MKJJ,

  Kwani si demokrasia imecukua njia yake, wameshindwa, kwa nini una-encourage CC/NEC wawaweke watu kwa matakwa yako? This might be an opportunity to opposition parties, the question is "are they well enough prepared for the battle?"
   
 6. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Sasa kwa mtindo huu wa kupendeleana, kwanini tuwalaumu vilaza kama Shamsa Mwangunga, Masha, na Sofia Simba? Aliyeshindwa akajaribu kwa tiketi nyingine kama ni jasiri kweli...
   
 7. m

  mndebile Senior Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Safi Regia Mtema, kwa maoni yangu vyama vipo vingi si lazima wagombee kwa tiketi ya CCM tu, waje CHADEMA sie tunawakaribisha, binafisi Selelii na Kimaro wanawakubali kwa hoja zao wawapo bungeni, ila inawezekana waliwasahau sana wapiga kura wao au kama kuna mizengwe!! basi njia nyeupe wachangamke mapema kwenda kwenye chama kisichokuwa na mizengwe na Mungu atawasiadia wanaweza kushinda.
  Hawajachelewa!!!!!
   
 8. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  GS sikujua kama wewe wa 'njia moja'...hahhaaaaa karibu sana Utengule , mpanga! hahaaaaa
  mix with yours
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo ninapopata taabu sana kumwelewa Mwanakijiji na anavyoiangalia hatma ya Taifa la Tanzania ambalo kila dakika inazidi kutumbukia kwenye kwenye dimbwi la tope.

  • Mwanakijiji anadai kuwa kuna unfinished business kati ya mahasimu wawili ndani ya CCM na ingefaa kama wote wangerudishwa bungeni ili waweze eti this time kufanya kweli.
  • Mwanakijiji, kwa maandishi yake hapo juu, ni kama anataka kutuaminisha kuwa mafanikio yaweza kuletwa kwa business as usual kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwa usanii ule ule tulioushuhudia toka 2005.
  • Mwanakijiji yaonekana hawapi nafasi ya kufaulu wale wanaotaka kuona mabadiliko si katika uongozi tu bali katika mfumo ambao umetudumaza kwa miaka nenda rudi tangu uhuru.
  • Mwanakijiji amewahi kuwa na wasi wasi na wapinzani na yaonekana hawaoni watanzania wengine nje ya CCM kuwa wana uwezo wala vision ya kutosha ya kuliongoza taifa hili.
  • Mwisho kwa msimamo wake wa karibuni Mwanakijiji ametoa hoja mbali mbali za kutetea msimamo wake kuwa heri hao hao waliolifikisha taifa lilipo kuliko wageni wanaotafuta uongozi bila kujipanga vya kutosha.
  • Mwanakijiji bado anataka wabunge wale wale wanaopiga kele bungeni lakini wakati wa maamuzi muhimu ama wanakaa kimya au wanakuwa rubber stamp kwenye vikao vya CCM kama pia wanavyofanya kwenye hoja za serikali.

  Mwanakijiji Umma wa Watanzania unaanza kuamka na ningeomba usiturudishe kule kwenye siasa za kinafiki za wabunge wa CCM kwani hawana uzalendo au ujasiri, ni usanii tu kama wa bosi wao. Wakati wewe unawasikitikia na kuwaombea wapewe ushindi wa mezani kama kawaida ya CCM, wengine hata sura zao hatutaki kuziona zikikatiza kwenye viwanja vya bunge. Kama ni nafasi, walipewa na kwa miaka mitano hawana cha kuonyesha kwani Kagoda, Meremeta, Tangold, Dowans, Richmond, EPA n.k. ziko pale pale !! Hapana, muda wa kutuzugha umekwisha na sasa ngoja watafunane wenyewe halafu wachache wao watakaosalia, tutawatafuna ifikapo October 31 !
   
 10. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kula tano mkuu Regia
  Huyu mzee nilianza kumpunguzia alama za ufanisi tangu hoja za CCJ na utumbo wao alivyokuwa akiwatetea.
  Ukisoma kwa juu juu utaona kuna mantiki kidogo lakini ajiulize nini hatma ya upinzani ndani ya CCM, ikiwa imejisafisha (japo haiwezekani) ndo anataka vyama vingine vife? (Rejea hotuba ya mwalimu Nyerere kuhusu umuhimu wa siasa ya Vyama vingi. na iwapo watashindwa/ mabadiliko yakishindikana watafanyaje? Bila shaka wapiganaji watatoka ndani ya sisiemu na kurudi kujipanga nje ya huo mfumo, kwa kupenda au kwa kulazimishwa. mwana kiijeijei wakati huo ndio huu, huna haja ya kusononeka na yanayotokea ndani ya sisiemu, furahia hilo na ndio mwanzo wa mwisho wa dubwashika hili. Rudi kundini na ujiunge na wenzio ili kuimarisha nguvu na kusaidia kupunguza changamoto
   
 11. k

  kaka2002 Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Mwanakijiji hana mapenzi na CHADEMA. Alitamani kuona CCJ ikichukua madaraka ya nchi hii kwa muda mfupi wa chama hicho kuwepo duniani. Alikitetea kwa nguvu zake zote na kutaka kila mtu aamini umadhubuti wa chama hicho.

  Mi nadhani umefika wakati wa kujiimarisha kwa kuunganisha nguvu na kila mtu anayelitakia mema taifa hili. Tunahitaji viongozi wasiohujumu jitihada za kuwaletea watanzania maendeleo. Awe na uchungu na mali za nchi hii, asiwe fisadi, asiwe rafiki wa mafisadi (ndege wa aina moja huruka pamoja), asiwe ombaomba, awatie moyo watu wake kufanya kazi kwa bii pasipo kuwakatisha tamaa eti watanzania wavivu mara ooh hawajui kiingereza, mara hawana nidhamu n.k.

  Kiongozi mzuri ni mwenye kuongoza kwa kutenda na watu wake wakahamasika na kumfuata. Shime watanzania wakati wa mabadiliko ni sasa. NDIO TUNAWEZA. KILA MMOJA ATIMIZE WAJIBU WAKE. KILA MMOJA ANATAKIWA AWE SEHEMU YA MABADILIKO TUNAYOYATAKA.

  MUNGU ATUSHINDIE. AFICHUE HILA ZOTE WANAZOFANYA KUZUIA MABADILIKO.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji anajua hawa hawawezi kurudi. Mtu kama Selelii alitaka kumweka pabaya Lowasa siku ileile na pengine kuiangusha serikali ya JK. Wengi mlimwona Mwakyembe kama shujaa kwenye kamati ile lakini mimi shujaa wangu alikuwa Selelii.
  Wapambanaji hawa watafute majukwaa mengine kama NGOs, vyama vingine vya siasa au waje humu JF.
   
 13. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama ni wavivu na hawana nidhamu je wazungumziwaje! ndio yale yale ya kuwalaumu wazungu wanaosema africa ni maskini na ina maambukizi makubwa ya VVU....halafu waafrika wanasema kuwa wazungu wana ekzagireti matatizo yetu! SI KWELI .....UKWELI UNABAKI KUWA NI KWELI AFRIKA INA MATATIZO HAYOO
  mix with yours
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji mwenyewe kaingia mitini.Uko wapi njooo ujibu hoja...
   
 15. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu ndiye Mwanakijiji bana....
   
 16. n

  nkaki Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Jamani sisi tunataka wabunge watakao wawakilisha Watanzania bungeni. Yaani matatazo yote tulionao Watanzania yakapatatiwe ufumbuzi kupitia rasilimali zetu tulinazo ambazo zinatosha na kusaza.

  Mwanakijiji sitakuelewa endapo utataka waliotemwa warudi kwa msamaha wa NEC ili wakatengeneze mambo yao. Angali matatizo walionao Watanzania Maji, Barabara, hospitali, shule etc. Angalia wakulima wanavyoteseka (wanaoishi vijijini). Wakati mwingine mgongana husababishwa na kuzikana. Hakuna aliyemsafi wote wamepungukiwa la msingi wasome nyakati.:
   
 17. K

  Kiganja Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I have only this to say on Lowassa: "He is as rotten a human being as can be found anywhere under their "flag"; he is a shame to the Masai People and to the nation, and no one who has helped him to send him to the Parliament / Prime Minister's office who did not know that, his proper place was the penitentiary, with a chain and ball on his legs." Period
   
 18. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhhhhhh
  mix with yours
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mtu akisoma hiyo topic bila background kidogo inatoa impression kuwa nataka watu wabebwe na NEC. Hapo nitakuwa najipinga misimamo yangu and I don't like kujipinga. Makala hii niliituma ili itoke siku ya Jumapili (August 1, 2010) siku ya kura za maoni. Lakini Mhariri kaamua kuitoa kwenye makala yangu ya kawaida ya Jumatano; kwa hivyo inasomwa ikiwa siku nne baada ya tukio iliyotakiwa kuzungumzia. So, isome ukifikiria unaisoma Jumapili siku ya kura za maoni. M. M.
   
 20. N

  Ngala Senior Member

  #20
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kula tano mzee mwenzangu maana ulinichanganya sana nikadhani kuna mtu anatumia jina lako vibaya lkn sikuona ukikanusha. kutuweka vizuri zaidi ebu tujazie makala ya lula wa ndaliwamunzila raia mwema toleo no 145 mii sina utaalamu huo. asante sana in advansi
   
Loading...