Wabunge Waliobebwa ni batili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Waliobebwa ni batili?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu wa Mungu, Nov 15, 2010.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Source: Na M. M. Mwanakijiji, gazeti la MWANAHALISI, Jumatano, Septemba 17,2010:

  Kwa muda sasa wanaJF wanakuwa wakichangia mawazo hoja ihusuyo wabunge waliopitishwa na kuhalalishwa na Tume ya Uchaguzi bila kuchaguliwa na waliojiandikisha na kushiriki katika uchaguzi mkuu wa tarehe 31.10.2010.
  Kwa mujibu wa mijadala ya wanaJF juu ya mada hii ni kwamba wabunge husika si wabunge halali, miongoni mwa sababu zinazotolewa kuwa:-
  1) Waliowachagua si wapigakura walio katika Daftari la Wapigakura; hawa walipatikana kutokana na chaguzi za kura za maoni ndani ya vyama husika.
  2) Kwa mujibu wa hoja za kisheria alizotoa mwandishi wa makala iliyotajwa juu-(Source), ni kwamba wabunge husika ni batili kwa sababu hawakupatikana kwa njia halali katika katiba ya JYMT.
  Kwa kuwahalalisha NEC imevunja katiba ya JYMT

  Baada ya ukweli huu kujulikana, hoja ya msingi ni je Hatua gani zichukuliwe (a) Ili kuwapa wawakilishi halali wapigakura wa majimbo yaliyoathirika; (b) NEC kwa kosa linalostahili kuitw uhaini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hao wabunge sio batili kwa sababu wametangazwa washindi na nec.
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Wamebebwa kama hivi au vipi?

  [​IMG]
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Minda inaonekana hata sheria inakupa shida. Unalozungumza ni kuhusu nafasi ya rais pekee ndiyo ikishatangazwa na tume huwezi kuhoji katika mahakama yo yote hapa nchini. Vinginevyo tusingeona kesi dhidi ya wabunge baada ya uchaguzi. Hebu cool down mwana kwetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. O

  Okinawa Senior Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbunge ambaye hajajachaguliwa na wananchi si Mbunge halali isipokuwa wanawake wanaoingia kwa viti maalum.

  NEC wamevunja katiba ya Jamhuri ya Muungano.
  Wananchi inabidi tuungane ili kuwakataa ili uchaguzi ufanyike kwenye majimbo hayo.
   
 6. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MwanaJF Safari ni Safari wlibebwa na Tume ya Uchaguzi na kuingizwa bungeni kupitia mlango wa nyuma maana wapigakura wa majimbo yaliyoathirika hawakupewa nafasi ya kuwachagua au kuwakataa kama msingi halisi wa demokrasia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  ni batili ndio..kwa mujibu wa katiba ya TZ sura y a 3, sehemu ya pili, ibara ya 66, kifungu cha 1 a-e, aina za wabunge ni zifuatazo:
  a) wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi
  b) wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka kuanzia asilimia 20 ya wabunge..itakayotajwa mara kwa mara na tume ya uchaguzi....
  c)wabunge 5 waliochaguliwa na baraza la wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake
  d)mwanasheria mkuu
  e)wabunge wasiozidi 10 walioteuliwa na rai kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67....

  Sasa hao waliopita bila kupingwa. nashindwa kuwaweka hapo juu!!!
  kweli wanatoka majimboni, ila
  hawakuchaguliwa na wananchi wote wa majimbo yao, bali walichaguliwa na WANACCM tu.
  Suluhisho: marekebisho ya katiba yanahitajika ili in case kwenye jimbo kunakua na mgombea wa chama kimoja, then kura za ndio na hapana ndio zitumike. Otherwise waliopita bila kupingwa ni BATILI.
  Naomba kuwakilisha.
   
 8. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naamini kuna wanaJF walio wanaharakayi wanaoweza kuchukua hoja hii kama uchkachuaji wa haki za wanadamu wapigakura wa majimbo yaliyoathirika kwa Tume ya Uchaguzi kupora haki na demokrasia kwa kuwalazimisha kuwakilishwa na watu wasiopita katika mchakato halali wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya nchi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Pipoooooooooooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! where are u???????????????????????.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mbunge anayepita bila kupingwa ina maana kuwa ballot paper ilikuwa na jina lake peke yake, kwa hiyo kura zozote anazopata zaidi ya moja ni ushindi kwake.


  Iwapo Tume haikutayarisha ballot paper zozote zenye majina ya wabunge hawa na kuzipeleka kwa wananchi siku ya uchaguzi wakiwa na imani kuwa wabunge hao wameshapita bila kupingwa, basi hao ni batili.
   
Loading...