Wabunge walimtisha Spika kura ya kutokuwa na imani

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Inaelezwa kuwa Tume ya Bunge wakishilikiana na wabunge walimwekea Spika Makinda shinikizo kubwa wakitaka posho mpya na kama angeshindwa, walimtisha kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na hivyo, kumng’oa madarakani.

Kutokana na azimio hilo kupitishwa, Spika alilazimika kutetea posho hizo kwenye vyombo vya habari na wajumbe wa Tume hiyo kwa kushirikiana na Spika, walimtaka pia Katibu Dk. Kashilila kuanza kuwalipa katika mkutano uliopita wa Bunge lakini alikataa.
 
tupe data na sio habari za kusadikika,
wabunge wangapi walimtisha kupiga kura ya kutokuwa na imani nae kwa lipi hasa?
tunajua mama ni kilaza wa sheria sawa lakini sidhani kama angeweza kutishwa bila kushtaki kwa waliomweka madarakani.
 
Wabunge gani hao ???? Hawa Hawa wa CCM waliokosa msimamos juu ya kung'oa magamba wataweza kung'oa spika anayefukuzia mshiko wa matumbo yao
 
Hakuna cha kutishwa wala nini, ni yeye tu hazimtoshi. Kwa hiyo kauza nchi kwa ujira wa kiti chake sio? Yaani ameona afadhali watanzania wakawaida wafe njaa, kuliko yeye kukosa kiti hicho? Kama habari hiyo ni kweli basi Kikwete amekosea sana kumweka kwenye kiti hiyo muuaji mkubwa huyo.
Ebu fikiria kwa kuruhusu posho ya laki 2, ni watanzania wangapi wanakufa njaa bila hata kupata 500 kwa siku? Kwanza posho ya nini? Yaani kukaa tu bungeni na kusinzia wanahitaji kodi ya wananchi iwalipe? Mbona wafanyakazi wengi wakawaida tena wanaofanya kazi mazingira magumu hawana hivyo miposho. Ebu wafie zao huko, ni kutafuta tu kupata hela ya kwenda kuenezea ukimwi hawana lolote hao
 
Bado kuna wanaopiga debe rais 2015 awe mwanamke. Hatari sana sio nawadharau waheshimiwa kina mama bali bado wakati wa mwanamke kuwa rais hapa Tz.
 
kama alitishiwa na akakubali kufuata matakwa ya waliomtisha hiyo inaashilia kuwa yako mengi ambayo yanamfanya yeye afanye kwa matakwa ya watu furani,ilimradi tu kurinda kitumbua chake,kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama yeye hakutakiwa kufuata matakwa ya watu furani kwani anaongozwa kwa taratibu,sheria na kanuni

kwahiyo sio wabunge tu kutokuwa na imani nae sasa hivi hata wapigakura wake hawana tena imani nae
 
Bado kuna wanaopiga debe rais 2015 awe mwanamke. Hatari sana sio nawadharau waheshimiwa kina mama bali bado wakati wa mwanamke kuwa rais hapa Tz.

Hawa watu ni dhaifu sana ndio maana hata Nyerere hakutaka hawa watu wawe viongozi.
 
kama alitishiwa na akakubali kufuata matakwa ya waliomtisha hiyo inaashilia kuwa yako mengi ambayo yanamfanya yeye afanye kwa matakwa ya watu furani,ilimradi tu kurinda kitumbua chake,kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama yeye hakutakiwa kufuata matakwa ya watu furani kwani anaongozwa kwa taratibu,sheria na kanuni

kwahiyo sio wabunge tu kutokuwa na imani nae sasa hivi hata wapigakura wake hawana tena imani nae
Kwani Makinda alipigiwa kura na nani, yeye ni kati ya waliopata ubunge wa sandakalawe, na ukiangalia viongozi wakuu karibu wote ni wale waliopita bila kupingwa, Waziri Mkuu Pinda, Waziri wa mambo ya nje Membe na Spika wa bunge Makinda, kwa trend hii utaona hata urais wa JK unaweza kuwa wa sandakalawe.
 
Angetolewa kwa kutokuwa na imani nae akakubali kutoka angekuwa shujaa wa karne......angebakia kuwa mbunge milele kwa heshima!!kama anakubali kusaliti uma wote wa walalahoi ajili maslahi binafsi,ukweli utakuja kumtoa pale maaana hana sababu kuwepo pale
 
Back
Top Bottom