Wabunge walalamikia ushuru wa magari utozwao bandarini...

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,238
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,238 2,000
Leo wabunge wawili akiwemo Halima Mdee wameshambulia waziri wa fedha kwa ushuru wa magari usioleweka..... Mbunge mmoja alifikia kuwaita TRA majambazi..

Ccha kushangaza wabunge hao wamemtaka waziri wa fedha, Mkulo awasaidie warudishiwe pesa ambazo wanadai wametozwa isivyo halali za ushuru wa kuingiza magari na kodi za TRA........

sasa hapa ndo ninaposhangaaa

1. Wakati sheria hizo mbovu mbovu za ushuru na kodi za kuingiza magari zinapitishwa bungeni, wao walikuwa wapi? Hawakuelewa au walifikiri hayawahusu?

2. Huu utaratibu wa kudai pesa warudishiwe, je na sisi wananchi tutarudishiwa vipi? Lini?

Hivi hakuna mtu anayeona kuwa kodi na ushuru wa magari bandarini ni wizi mtupu?

Mtu ananunua gari dola 2,000 akifika TRA anaambiwa alipe ushuru dola 8,000.... na gharama nyingine; gari linafika mpaka dola 15,000 au zaidi....

Je, hasara ni ya nani hapo? Wanunuzi wa magari wanapopungua, nani anapata hasara? Nchi haipotezi pesa kwa kuwa na wateja kidogo wa biashara ya magari na yote yanayoendana na biashara hiyo? Na madhara yake kiuchumi?

Je, wajanja wanaotumia loopholes za sheria hizi hawafaidiki?

Je, tunafanana na nchi gani kwa sheria hizi? Kenya? South Africa? Uganda? Zanzibar??????

Lakini, kama wabunge nao wanalalamika na kulia,na sisi tufanyaje?
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,239
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,239 1,500
IMO utaratibu ulowekwa kuweza komboa gari yako bandarini kwa kweli ni mbovu kupita maelezo… Wana process ndefu kupita maelezo… na Management mbovu kupita maelezo (thou hapa karibuni kidogo imekua nafuu hasa katika suala zima la uwizi wa mizigo inayokua imepakizwa katika gari na mhusika – na vipuri vya magari for insance battery, car radio na the like) Ni kweli kua ni vitengo vingi vina husika pale… kama TRA, (ambayo nayo ina makorombwezo kibao… e.g registration fee na VAT – to mention but a few) Vya kulipia ni viiingi mno… ukitoa gari pale hadi ile plate number temporary wametengeneza vibao pale vya kienyeji na walipia… lol

Na hizo processes naona ndio inafanya bei iwe kubwa kuliko hata gari ulonunua (kwa kuzingatia mwaka wa gari ilivotengenezwa) na pia naona ndio inawafanya wale madalali waweke ada kubwa mno za kusimamia utoaji wa magari wakijua wazi majority Tanzanians hawajui/hawawezi fuatilia sehemu husika – hasa ukizingatia kuna too many docs to fill…. Na hapo wa Tz ndo ujanja hutuishia… Hata hivo I would have to say saizi imekua nafuu kiasi… ndio pesa bado ni nyingi… But atleast hawakuweki pale makusudi ili tu ulipia ada ya mzigo kuwepo bandarini after one week expiry inayo ruhusiwa…

Upande wa wabunge… hao mpaka yawakute ndo huwauma… wakiwepo Bungeni ndio wanasikia mambo mbali mbali ambayo in ya kumuumiza mwanachi but hawavalii njuga kua wahakikishe kuweka system ya kumtemtea mwananchi wa kawaida… Na katika Vyombo vyoote vya serkali – hakuna inayo mnyonya mwananchi kama TRA…
 

Alwatan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Messages
409
Points
195

Alwatan

JF-Expert Member
Joined May 19, 2009
409 195
Mi kila siku nasema wabunge wa CCM na hata baadhi ya wapinzani wa sasa wengi wao(sio wote) ni makanjanja tu... mpaka yawakute wao binafsi ndio wanapaza sauti.

Sisi wananchi wa mtaani hatuna pa kukimbilia.

Tiba ni KATIBA MPYA KABISA itakayojenga STRONG INSTITUTIONS with proper checks and balances. Institutions zitakazoweza kudhibiti personalities regardless of how strong or powerful they are.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,471
Points
2,000

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,471 2,000
Ivi kwa nini isiwe kama Uganda wanacalculate kodi based on the CIF whether umeforge au halisi haiwahusu!
Sasa apa TZ wanafanya ujanja ujanja tuu!
Nchi ya kitu kidogoooo
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Mi kila siku nasema wabunge wa CCM na hata baadhi ya wapinzani wa sasa wengi wao(sio wote) ni makanjanja tu... mpaka yawakute wao binafsi ndio wanapaza sauti.

Sisi wananchi wa mtaani hatuna pa kukimbilia.

Tiba ni KATIBA MPYA KABISA itakayojenga STRONG INSTITUTIONS with proper checks and balances. Institutions zitakazoweza kudhibiti personalities regardless of how strong or powerful they are.

Mzee wabunge makanjanja wako CCM na CUF pekee lakini wengine hushindwa kwa ndiyoooooooooooo ila nia yao njema na husema wazi wazi .Fikiria wapinzani wakisha ona jambo wakasema si humezwa na uwingi wa ma CCM na Uchama kutawala bungeni badala ya Tanzania kwanza ? CCM laamna tupu na lawama lazima watabeba .
 

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,909
Points
1,225

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,909 1,225
tatizo hii nchi haina wabunge wanao ona mambo muhimu kama haya, hivi TRA
ina mamlaka gani ya kunyonya watanzania wanaojaribu kujikomboa kwa kujitafutia vijiusafiri huko serikali ina angalia?

hapa ndipo uwa najiuliza wale wabunge wetu mashuhuru kutetea jamii wako wapi?

kaka ZITTO ili ninakuhusu moja kwa moja kama waziri kivuli tunaomba tuweke kivulini vijana wataifa ila.
watu wakiwa na usafiri kuna faida kubwa sana hata huko vijijini watakwenda kufanya kazi na kuishi mijini.
kodi za gari ziwe sana bei lililonunuliwa, na nyingine zifutwa bana
 

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,909
Points
1,225

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,909 1,225
hii thread nitaikalia mpaka kieleweke, wakuu tuweke mawazo/fikra hapa usafiri ni muhimu kwa shughuli ndogo ndogo lakini zenye manufaa kiuchumi, kwa tanzania ya sasa mtu kama unakaa/fanyakazi dar uwezi kuwekeza morogoro kwa sababu ni ngumu kutegemea mabasi kwenye rudi kwa ratiba yako
TRA sasa basi imetosha
 

Dickson Mpemba

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2010
Messages
350
Points
225

Dickson Mpemba

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2010
350 225
Mimi nafikiri kuna tatizo katika mfumo mzima wa ulipaji kodi Hapa Tanzania sioni sababu ya kila mlipa kodi kutumia agent wakati Ana TIN yake na kwa ufupi mfumo mzima wa kutoza kodi pale TRA hauna uwazi na umejaa ukiritimba wa ajabu .
 

MWEEN

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2010
Messages
481
Points
225

MWEEN

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2010
481 225
Ivi kwa nini isiwe kama Uganda wanacalculate kodi based on the CIF whether umeforge au halisi haiwahusu!
Sasa apa TZ wanafanya ujanja ujanja tuu!
Nchi ya kitu kidogoooo
Wakuu,

Hili suala la unyanyasaji wa TRA dhidi ya wananchi wake ni moja kati ya mambo yanayowafanya raia wema washawishike kutoa rushwa (la sivyo ulipe kiasi kikubwa usichonacho) bila kupenda. Sheria zinapindishwa kwa makusudi kwa kujua kwamba, options zingine zozote utakazochukua zitakugharimu zaidi. Katika gharama zote zinazokatisha tamaa ni "MUDA". Kwamba inachukua muda mrefu sana kwa mtu kushughulikiwa suaa lake kiasi kwamba hata bidhaa yenyewe inapoteza thamani. Hatimaye itakapofahamika kuwa una haki, fidia yako ni neno "SAMAHANI" kama utaipata hiyo fidia.

Mh. Lisu alipokuwa anajadili mabadiliko ya sheria ya TRA mwanzoni mwa kikao cha 4 cha bunge la 10, alitaka kipengele kiongezwe, kuwa kama mteja akikosea anapigwa faini, basi ni haki kuwa TRA wakikosea nao wapigwe faini. Bahati mbaya mazezeta ya CCM yakapinga. Hii ingewaadabisha TRA wawe makini ili wasimuonee mteja. Ungeshangaa ni watu wangapi wangepinga udhalimu huu wa TRA.

sambamba na hili, polisi nao wange kuwa wanawajibika kwa kila tuhuma itakayothibitika kuwa sio ya kweli. Aliyetendewa udhalimu alipwe fidia ya kutosha nafasi na kipato ambacho kadhia hiyo ya uwongo imemsababishia. Hii ndiyo dawa ya kesi za kubambikiziwa, kukamatwa bila sababu, kuwekwa mahabusu kwa ridhaa ya askari, mkuu wa wilaya, Mkoa na hata Rais.

Nawakilisha
 

Mr.Mak

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2011
Messages
2,801
Points
2,000

Mr.Mak

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2011
2,801 2,000
mie naona wale watengeneza ile formula wanafanya makusudi ili watu wawaletee magari hadi bongo kisha washindwe kulipia kisha wao wanayanunua kwenye mnada, tar 1/9 kutakuwa na mnada kaoneni magari ya watu wanavyoyauza bila hata huruma ya kumfikilia aliyeyaagiza toka nje mpaka hapa kama katumia dola nyingi sana. Ivi kwanza naomba mnijuze nini malengo ya TRA kutoza kodi kubwa kuliko bei halisi ya kitu chenyewe? naomba wanijuze ni biashara gani nyingine inayotoka nje ya nchi ambayo kodi yake huwa ni zaid ya thamani ya hicho kitu? Hakika mimi sioni mantiki ya TRA ya kufanya hivo wanavotufanyia. TRA kama chombo cha serikali basi kinaipa sifa mbaya serikali yake kwa unyama huo wanaotufanyia sisi watanzania.
Niulize ivi soko la africa mashariki likianza ni ipi bandari ya africa mashariki ili atleast litumie formula hizo za uganda. Kumbe magari japani hayana bei sana ila sisi wenyewe ndio tunajichanganya. Condition ngumu kama hizo TRA walitakiwa kuziweka kama serikali yetu ingekuwa na kiwanda cha magari. sasa kiwanda huna na bado hutaki wanunue magari?!!!!!
 

sem2708

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
3,818
Points
2,000

sem2708

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
3,818 2,000
nchi imekosa ubunifu,njia pekee wanayoona ya kupata mapato ni kodi za magari na wafanyakazi huku wakiachia makampuni ya simu,madini n.k yakitesa.
 

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,238
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,238 2,000
Ivi kwa nini isiwe kama Uganda wanacalculate kodi based on the CIF whether umeforge au halisi haiwahusu!
Sasa apa TZ wanafanya ujanja ujanja tuu!
Nchi ya kitu kidogoooo
sasa unaona?
ina maana mfanyabiashara wa uganda ana advantage kubwa mno kulinganisha
na wa tz
halafu tunasema watanzania wamezubaa na eac
 

Forum statistics

Threads 1,358,227
Members 519,261
Posts 33,162,850
Top