Wabunge ‘wala’ rushwa marufuku kuingia China; Ikithibitika majina yao yatatumwa Beijing | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge ‘wala’ rushwa marufuku kuingia China; Ikithibitika majina yao yatatumwa Beijing

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, AGOSTI 06, 2012 05:49 NA ARODIA PETER

  *Lengo ni kudhibiti vitendo vya jinai
  *Ikithibitika majina yao yatatumwa Beijing
  *Kamati ya Makinda yasubiriwa kwa hamu
  *Viongozi wa dini watishia kwenda majimboni

  TUHUMA za rushwa zinazoendelea kuwaandama wabunge, zimechukua sura mpya, baada ya Serikali ya China kujiandaa kupiga marufuku wabunge wote wanaotuhumiwa kujihusisha na rushwa kuingia nchini humo.

  Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata kutoka ubalozi wa China hapa nchini, zinasema umepokea taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wakuu wa China, wafuatilie kwa karibu wabunge wote wanaotuhumiwa kwa rushwa, kisha watume taarifa ili wakibainika wasiingie kwenye nchi hiyo.

  "Tumeletewa taarifa na viongozi wetu wa ngazi za juu, kuwa tufuatilie kwa kina wabunge wote ambao wanatuhumiwa na wakibainika majina yao yatumwe China, ili wazuiliwe kuingia kule,

  …unajua taifa letu ni taifa ambao halina mchezo na mtu anayepokea rushwa ovyo ovyo na ni kosa la jina. kwa kiongozi kama hawa wabunge kujihusisha na siasa,

  "Kwa kipindi chote hiki, kama wabunge hawa wangekuwa China leo hii, tungekuwa tunazungumza mambo mengine, wangekuwa wamechukuliwa hatua kali,

  "Tunashangaa kuona kwa nini hapa kwenu, bado wanaendelea kuruhusiwa kuingia bungeni… au wanasubiri majibu ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizi," kilihoji chanzo chetu.

  Chanzo hicho, kilisema ubalozi wa China hapa nchini, umetuma maofisa wake mjini Dodoma kwa ajili ya kupata mwenendo wa wabunge wote wanatuhumiwa.

  "Hivi sasa hapa Dodoma kuna maofisa wa ubalozi wa China, wanaendesha uchunguzi kuhusu tuhuma hizi, ikibainika ni za kweli baada ya majina ya wabunge ‘wala rushwa' kutajwa, watachukua picha zao kwa ajili ya kuzituma China, ambako hawataruhusiwa kukanyaga kwa sababu kwao rushwa ni kosa la jinai," kilisema chanzo chetu.

  Naye Mratibu wa maombi yanayoendeshwa na Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania, mjini Dodoma Mchungaji William Mwamalanga alisema kwa kauli moja viongozi wa dini, wamesikitishwa na tuhuma hizo.

  Alisema viongozi wa dini ambao wamepiga kambi mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuliombea taifa, wamewataka wabunge wote waliotajwa wajiuzulu mara moja.

  "Viongozi wa madhehebu mbalimbali tupo hapa Dodoma, kwa ajili ya kuliombea taifa, lakini moja ya jambo kubwa ambalo tumekubaliana kupita katika majimbo yao, kueleza waumini wetu matatizo haya ya rushwa… tunataka wajiuzulu kwa ajili ya kulinda heshima zao,

  …viongozi wa dini wamekerwa na tabia ya wabunge kuhusishwa na rushwa, wao wana neno moja tu, wanataka Bunge livunjwe kwa sababu nje ya nchi tunachekwa mno.

  Katika mahojiano kwa njia ya simu na MTANZANIA jana, Mchungaji alisema, viongozi wote waliotajwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kusababisha nchi kuingia katika mgao wa umeme bandia, wanapaswa kujiuzulu, ili kulinda heshima zao, na kamwe wasisubiri kuwajibishwa na kamati iliyoundwa ya Spika wa Bunge Anne Makinda.

  Alisema si jambo jema kwa wabunge kusubiri kuchunguzwa na Kamati ndogo inayoongozwa na Brigedia Jenerali, Hassan Ngwilizi iwaumbue.

  "Dawa ya wala rushwa si kuunda kamati kuwachunguza, vitendo hivi vinafanywa kwa siri kubwa, wabunge wetu wafike mahali wabadilike, kiongozi akituhumiwa, lazima jambo hilo lipo, kama halipo basi linakuja."

  "Vitendo vya rushwa ni kama vile mtu kukamatwa ugoni na mke au mume wa mtu, ukikuta vinafanywa mchana kweupe hicho ni kiwango cha ukichaa, rushwa katika nchi yetu imefikia kiwango cha ukichaa."

  "Wanaotuhumiwa wasingoje kamati ya Spika, tutawaona ni wakweli wakijiuzulu, hata kama hawajatenda, wanapaswa kuwa mfano maana hizo ni tuhuma nzito kwao."

  "Wakumbuke aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa alipoamua kujiuzulu si kwamba alikuwa na makosa ya moja kwa moja, bali alitaka kulinda heshima ya chama chake na taifa lake,

  "Wito wetu kwa hao waliotuhumiwa watambue taifa letu lipo katika wakati mgumu sana, rushwa ilikofikia inaweza kuangusha nchi wakati wowote kwa kiwango kisichotarajiwa, hivyo wataonekana waungwana na hekima ya hali ya juu kama wakijiuzulu nafasi zao na kuwapisha wengine" alisema Mchungaji Mwamalanga.

  Alisema hivi sasa, Watanzania wamefika mahali hawamwamini mtu yeyote, si kamati za Bunge wala vyama vya upinzani, kwa sababu baadhi yao wametajwa katika kashfa za aina hiyo.

  Mchungaji huyo alikwenda mbali zaidi na kuonya kuwa, kama watagoma kujiuzulu, basi kwa kutumia umoja wao wa dini watakwenda katika majimbo yao na kuwataka wananchi wasiwape tena nafasi katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

  "Sisi kwa umoja wetu, tumekubaliana kuombea taifa kwa miezi mitatu mfululizo, kiongozi mwenye kujihusisha na rushwa tutamtaja hadharani na katika jimbo lake la uchaguzi,

  "Tunao ushahidi wa kutosha, mgao wa umeme kwa miaka yote hii, ilikuwa hujuma kwa umma, viongozi wote waliohusika wamelidhalilisha taifa kwa ukimya wao, wabunge wa upinzani hawakupaswa kuwemo katika kashfa hii …wao ndiyo walikuwa tumaini la Watanzania."

  "Mathalani tamko la aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo William Ngeleja kwamba, mgao wa umeme nchini ungekuwa historia, ilikuwa ni ghiliba tu, kwani Watanzania waliendelea na mgao huo bila kuwepo na dalili ya kuisha, kibaya zaidi watendaji waliendelea kumdanganya Rais kwamba, mambo yako safi, haya hayavumiliki" alisema Mchungaji Mwamalanga.

  Kuhusu uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, alisema ni kiongozi mzuri, isipokuwa watu wanatumia upole wake kujinufaisha binafsi na kuliacha taifa.

  "Rais Kikwete ni mpole na muungwana sana, tatizo watumishi badala ya kutumia mwanya huo kujenga nchi, wanautumia vibaya kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.

  "Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi mwenye hekima na busara, alijua si kila ovu linaweza kuundiwa na kujadiliwa katika vikao, alikuwa na ujasiri wa kukemea hadharani bila woga na viongozi wenzake walimtii kwa hilo."

  "Ni bahati mbaya watumishi na watendaji wa Serikali hawana huo woga tena, wanafanya watakavyo kwa kisingizio kwamba hadi mahakama iwatie hatiani," alisema.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Oh Yes... Kwanini USA na EUROPE wasifanye hivyo pia?
   
 3. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  bora , au waweke sheria, wakiingia wanawatait na kuwapiga kitanzi huko huko, hatutaki kuwaona wakirudi tz
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  gazeti hili ni udaku tupu just look a mere cooked story
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa wachina sound tuu makampuni yao kibao yanatoa rushwa kupata miladi ya barabara no wonder barabara zao nyingi zinakuwa sub standard bse ela nyingi hutumia kuhonga
  Ndo maana wale wa CHiCo wameambiwa warudie kipande cha sekenke
   
 6. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  OLE Sendeka jina lake litangulie mengine yatafuata
   
Loading...