Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
Si huyu jamaa juzi Jumamosi alikuwa anasakata dansi na Miss sijui Kinondoni sijui Miss Dodoma. Watawala zetu hawawezi kutumia hata sixth sense - wewe ndiye una dhamana ya kuhakikisha taifa lina umeme, taifa liko gizani unakwenda kusakata rumba badala ya kuwa na vikao vya dharura (hata kama ni kuji-pritend) kutafuta suluhisho. Pambaf sana!!! Hii JF inatusaidia kumalizia hasira zetu hapa, vinginevyo mtu unaweza kujikuta uko dodoma unafyatua risasi.
 
Kwanza Mh. Pindi kakosea kitu kimoja. Kama waziri mkuu na subordinate raisi Jakaya Kikwete hakutakiwa kusema kwamba ingekua yeye angemfukuza kazi Jairo. Nasema hivyo kwa sababu je raisi akiamua kumbakisha Jairo Pinda atasema nini? Pinda yeye alitakiwa aseme tu kwamba taarifa hizi nitamfikishia raisi atakapo tua SA basi akaacha hilo jambo hapo. Sote tunajua mwenye uwezo wa kumuondoa Jairo ni JK kwa hiyo hatukuhitaji opinion ya Pindi ambae hawezi fanya chochote.

Cha pili ni kwamba kama Jairo ataondolewa basi na waziri husika i.e. Ngeleja anabidi aondoka. Nasema hivi kwa sababu haiingii akilini kwamba maamuzi ya kuchukua hizo milioni 50 toka kila taasisi/idara mpaka kutumia pesa hizo kutokea hongo kulifanyika pasipo waziri kujua. Kitendo cha pesa kutoka tu wizarani ina maanisha waziri alikua anajua. Sasa kusema Jairo aondolewe kwa kosa hilo halafu waseme Ngeleja is clean huo itakua kutufanya Watanzania wote ni watoto wadogo.

Kama mimi ningekua raisi ningemuandoa katibu mkuu, naibu waziri na waziri. Kwa sababu ni vigumu wao kuendelea na kazi zao chini ya wingo wa skendo hizi. In short ningekua raisi ninge reshuffle baraza zima na kuwatema baadhi ya watu kabisa. Maana ukweli ni kwamba kipindi cha pili cha JK kimekua kibaya zaidi kuliko cha kwanza.
Labda nam

Labada nami nisaidie kuongezea, kwa nini asubiriwe rais wakati makamo wake yupo?. Makamo anafanya kazi gani wakati rais hayupo yeye si ndiye anawajibika?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza Mh. Pindi kakosea kitu kimoja. Kama waziri mkuu na subordinate raisi Jakaya Kikwete hakutakiwa kusema kwamba ingekua yeye angemfukuza kazi Jairo. Nasema hivyo kwa sababu je raisi akiamua kumbakisha Jairo Pinda atasema nini? Pinda yeye alitakiwa aseme tu kwamba taarifa hizi nitamfikishia raisi atakapo tua SA basi akaacha hilo jambo hapo. Sote tunajua mwenye uwezo wa kumuondoa Jairo ni JK kwa hiyo hatukuhitaji opinion ya Pindi ambae hawezi fanya chochote.

Cha pili ni kwamba kama Jairo ataondolewa basi na waziri husika i.e. Ngeleja anabidi aondoka. Nasema hivi kwa sababu haiingii akilini kwamba maamuzi ya kuchukua hizo milioni 50 toka kila taasisi/idara mpaka kutumia pesa hizo kutokea hongo kulifanyika pasipo waziri kujua. Kitendo cha pesa kutoka tu wizarani ina maanisha waziri alikua anajua. Sasa kusema Jairo aondolewe kwa kosa hilo halafu waseme Ngeleja is clean huo itakua kutufanya Watanzania wote ni watoto wadogo.

Kama mimi ningekua raisi ningemuandoa katibu mkuu, naibu waziri na waziri. Kwa sababu ni vigumu wao kuendelea na kazi zao chini ya wingo wa skendo hizi. In short ningekua raisi ninge reshuffle baraza zima na kuwatema baadhi ya watu kabisa. Maana ukweli ni kwamba kipindi cha pili cha JK kimekua kibaya zaidi kuliko cha kwanza.

Kutokana na waelezo ya waziri ina maana hawakutakiwa kuipitisha bajeti kuu, sasa CCM hawaoni wanakula matapishi yao? kama waliipitisha ile bajeti kwa asilimia mia na sasa wanatuambia bajeti nzima inatakiwa kurudiwa hivi tunawaelewa kweli au ndio na sie ni ma-mbumbu mbu?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kashfa hii lazima pia Ngeleja atimuliwe
Monday, 18 July 2011 21:21
Mwananchi

Muda mrefu kabla ya Wizara ya Nishati na Madini kuwasilisha bungeni makadirio ya matumizi yake kwa mwaka 2011/12 mwishoni mwa wiki iliyopita, gazeti hili lilipata habari kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya habari ndani na nje ya Bunge zilizosema kwamba, wizara hiyo ilikuwa imetenga mabilioni ya fedha kuwahonga wabunge kwa lengo la kuwashawishi wakubali kupitisha bajeti ya wizara hiyo.

Vyanzo vyetu hivyo vya habari vilituhakikishia kwamba, hakika fedha hizo tayari zilikuwa zinagawiwa kwa wabunge na kwamba kampuni mashuhuri inayohusika na masuala ya mahusiano yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, ambayo tunahifadhi jina lake kwa sasa, ilikuwa imepewa zabuni ya kusambaza fedha hizo za hongo.

Habari zilisema fedha hizo zilielekezwa kwa wabunge ambao wangekubali kupokea fedha hizo na kuisaidia wizara hiyo kupitisha bajeti yake ambayo ilikuwa imekamiwa na idadi kubwa ya wabunge wa CCM na wabunge wote wa upinzani kwa kutokuwa na mikakati yoyote ya kumaliza tatizo kubwa la umeme ambalo limekuwa linalikabili taifa kwa muda mrefu sasa.

Lakini katika kufuatilia kashfa hiyo, gazeti hili lilidokezwa kuwa, fedha hizo awali zilielekezwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba ambaye inasemekana alisimama kidete kuikataa bajeti hiyo ilipojadiliwa na kamati yake, huku baadhi ya wabunge wakiiunga mkono. Habari zilidai kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipokea fedha hizo zinazosemekana zilikuwa “nyingi”.

Pengine wasomaji wetu na wananchi kwa jumla watashangaa kwanini gazeti hili, pamoja na kupata dokezo hizo nzito, halikuchapisha habari za kashfa hiyo hadi zilipoibuliwa jana bungeni na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo na kuthibitishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda?

Tunakiri kabisa kwamba baadhi ya wananchi wanaweza kuibua dukuduku kuhusu suala hilo, ingawa tungependa waelewe kwamba kutochapisha habari hizo kulitokana na ukweli kwamba wizara husika ilikanusha tuhuma hizo na ndiyo maana gazeti hili lilizingatia weledi kwa kuendesha uchunguzi na kutafuta ushahidi ambao hatimaye ungewezesha kupatikana ukweli usiotiliwa shaka.

Ndiyo maana hatukushangazwa hata kidogo na Mbunge Shelukindo alipoibua kashfa hiyo bungeni na pia hatukushangazwa na kauli ya Waziri Mkuu Pinda alipokiri kuwa wizara hiyo ilitoa rushwa kwa baadhi ya wabunge na kusema Serikali ingemfukuza kazi Katibu Mkuu wa wizara hiyo, David Jairo ambaye ushahidi umeonyesha kwamba, hakika ndiye aliyechangisha fedha za kuwahonga wabunge ili bajeti ya wizara yake ipitishwe na Bunge.

Pamoja na ukweli kuwa kashfa hiyo ni nzito na ni moja ya kashfa za aina yake tangu nchi yetu ipate uhuru, bado tunampongeza Waziri Mkuu Pinda kwa kuwasikiliza wabunge waliotaka kiongozi huyo mtoa rushwa afukuzwe kazi. Kama ambavyo tumekuwa tukisema na kusisitiza mara kwa mara kupitia safu hii, unyenyekevu na usikivu wa kiongozi huyo siku zote umeepusha shari na kuleta maridhiano miongoni mwa makundi katika nchi yetu, likiwamo Bunge.

Tunachokisisitiza hapa ni kwamba, Serikali isiishie tu kumtoa kafara Katibu Mkuu huyo pekee wakati ukweli usiopingika unajulikana, kwa maana kwamba mtoa rushwa huyo asingeweza kutenda kosa kubwa kama hilo pasipo kupata maelekezo na baraka za bosi wake, Waziri William Ngeleja. Ni aibu iliyoje kwa Serikali iliyo madarakani kwamba wizara inaweza kuziamuru taasisi zote zilizo chini yake zichange fedha za kutoa hongo ya kupitisha bajeti yake bungeni.

Sisi tumefadhaishwa na kusikitishwa na kashfa hiyo ambayo bila shaka imethibitisha kwamba, hakika ufisadi na rushwa vimejikita ndani ya Serikali. Tunamshauri Rais Jakaya Kikwete afanye maamuzi magumu kwa kuvunja Baraza la Mawaziri na kuwafukuza kazi Waziri Ngeleja na Katibu Mkuu wake, David Jairo. Tunadhani pia kwamba sasa Takukuru haitakuwa na kisingizio cha kutowafungulia mashtaka wote waliohusika na kashfa hii, wakiwamo baadhi ya wabunge na watendaji wengine serikalini.
 
Kwanza Mh. Pindi kakosea kitu kimoja. Kama waziri mkuu na subordinate raisi Jakaya Kikwete hakutakiwa kusema kwamba ingekua yeye angemfukuza kazi Jairo. Nasema hivyo kwa sababu je raisi akiamua kumbakisha Jairo Pinda atasema nini? Pinda yeye alitakiwa aseme tu kwamba taarifa hizi nitamfikishia raisi atakapo tua SA basi akaacha hilo jambo hapo. Sote tunajua mwenye uwezo wa kumuondoa Jairo ni JK kwa hiyo hatukuhitaji opinion ya Pindi ambae hawezi fanya chochote.

Cha pili ni kwamba kama Jairo ataondolewa basi na waziri husika i.e. Ngeleja anabidi aondoka. Nasema hivi kwa sababu haiingii akilini kwamba maamuzi ya kuchukua hizo milioni 50 toka kila taasisi/idara mpaka kutumia pesa hizo kutokea hongo kulifanyika pasipo waziri kujua. Kitendo cha pesa kutoka tu wizarani ina maanisha waziri alikua anajua. Sasa kusema Jairo aondolewe kwa kosa hilo halafu waseme Ngeleja is clean huo itakua kutufanya Watanzania wote ni watoto wadogo.

Kama mimi ningekua raisi ningemuandoa katibu mkuu, naibu waziri na waziri. Kwa sababu ni vigumu wao kuendelea na kazi zao chini ya wingo wa skendo hizi. In short ningekua raisi ninge reshuffle baraza zima na kuwatema baadhi ya watu kabisa. Maana ukweli ni kwamba kipindi cha pili cha JK kimekua kibaya zaidi kuliko cha kwanza.

...labda huyu Ngeleja anaogopwa kutemwa kwa sababu Rostam anamkingia kifua na hivyo Kikwete kishapewa onyo asimguse kabisa huyu pamoja na kushindwa katika kuiongoza Wizara ya Nishati. Kama utakumbuka Ngeleja alikuwa mstari wa mbele kupigia debe mitambo ya Dowans inunuliwe na Serikali.
 
Last edited by a moderator:
hawa gazeti la mwananchi hawa nao ni wazushi sana.....waitaje hiyo kampuni kam kweli ana uhakika na hicho wanachokisema ....na waseme kwa nini pesa zitumwe huko GST na sio huko kwenye kampuni hiyo inayosambaza pesa kwa walengwa?!!!

ushauri wao ni mzuri japo japo hautazingatiwa maana jk hataki ngereja aondoke
 
Kelele za Peoples' Power, Peoples' Power, Peoples' Power, Peoples' Power! It was nice.

Wabunge Chadema wanataka credit utadhani wao ndio wamekwamisha makadirio ya wizara! Cheap popularity kwa kila kitu hata pale ambapo hawahusiki kweli?
 
Wabunge Chadema wanataka credit utadhani wao ndio wamekwamisha makadirio ya wizara! Cheap popularity kwa kila kitu hata pale ambapo hawahusiki kweli?

wapi ulipoona wabunge wa chadema wanatafuta chepa popularity?
 
...labda huyu Ngeleja anaogopwa kutemwa kwa sababu Rostam anamkingia kifua na hivyo Kikwete kishapewa onyo asimguse kabisa huyu pamoja na kushindwa katika kuiongoza Wizara ya Nishati. Kama utakumbuka Ngeleja alikuwa mstari wa mbele kupigia debe mitambo ya Dowans inunuliwe na Serikali.

wala rostam hausiki na hii kitu........jk mwenyewe ana mkono wake hapo kwa 100%....
 
Wabunge Chadema wanataka credit utadhani wao ndio wamekwamisha makadirio ya wizara! Cheap popularity kwa kila kitu hata pale ambapo hawahusiki kweli?
We kweli unaumwa: unataka kusema wabunge wa CCM waliounga mkono hoja kwa 100% kuwa ndiyo waliohusika kuibua mambo!!, sasa subiri mmojammoja kuwekwa kitanzini. Kila mara wabunge wa CCM wamezoea kuhongwa kisha kuunga mkono kwa kishindo sasa Arobaini zao zimefika.
 
Habari za kuaminika 100% kutoka vyanzo vyetu dodoma vinasema kwamba, Mh. Ngeleja pamoja na David Jairo wamekaangwa na kijana mmoja ambaye pia ni mbunge kupitia Chama Tawala, kijana ambaye uelewano kati yake na hao watendaji wawili ulikuwa ZERO. Bifu ya kichinichini ya muda mrefu sana.

Kupitia mtandao wao uliokuwa ukiongozwa na Rostam Aziz, kijana huyo ambaye amekuwa mzungumzaji mkuu wa TANESCO na Wizara ya nishati na Madini, ndiye aliyesuka mpango mzima, kutumia watu ndani ya wizara kumsihi Bw. Jairo achangishe hizo fedha. Baada ya kufanikiwa, kutumia hao wafanyakazi , aliwaomba nyaraka ambazo zilisahiniwa na Jairo ambazo ndio sasa zinawakaanga wakina Ngeleja.

Ni huyu kijana mbunge ndiye Aliyempelekea mama Shelukindo barua kutoka kwa Jairo ikiomba Idara zote kuchangia 50milion. Vile vile kijana huyo alimpelekea Waziri mkuu barua ya kuibua Rushwa. Haya yote yalikuwa ni mpango mzima wa kuonyesha kwenye Ngeleja na mwenyewe Jairo hawafai kuongoza wizara hiyo. Bifu kati ya huyu kijana na Jairo imetokea Ikulu. Mwisho wake ndo hapa.

Ukisikia siasa chafu, subiri muone sasa mpira ukichezwa kwenye uwanja wa Siasa. Ngeleja nje.

Habari ndo hiyo toka Dodoma.............

Pengine Kijana sasa JK atampa wizara baada ya familia yake kuombolewa pale aliponyimwa wizara hasa baada ya baba yake kutangaza kwamba mwanae lazima awe waziri

Nice try! Haiingii akilini kabisa hii hoja. Nyie ndio wale wale mnaodai kwamba Ngeleja, Jairo na January wote ni watu wa Rostam. Leo hii unaleta hoja kwamba January (bila ya kumtaja jina jinsi ukionyesha woga wako, lakini ni wazi ni nani unamuongelea hapa) kwamba yeye amewa set-up wenzake kwa kumtuma Jairo atengeneze hiyo barua. Kwanza Jairo kama ni mtu mwenye akilli timamu au maadili unaweza kushawishika na yeyote kufanya jambo kama hilo kweli? Ikumbukwe kwamba Jairo ameandika hii barua baada ya Kamati ya Makamba kupitisha makadirio ya Bajeti. Jairo alitaka pesa za kwenda kufacilitate kupitisha mbele ya Bunge zima, sio mbele ya Kamati. Ikumbukwe pia kwamba Wizara ilishajaribu kuwapa bahasha wajumbe wa Kamati kabla ya kupitisha makadirio, na hili lilikemewa na Mwenyekiti wa Kamati. Sasa baada ya Wizara kupatwa na msukusuko huo ambao uliandikwa magazetini wiki iliyopita, jiulize iweje ikaendelea kutafuta pesa za kusaidia kupitisha makadirio mbele ya Bunge zima?

Hii ni chuki tu na roho ya kwanini. Huyu kijana anafanya kazi, tatizo haters wengi hampendi kwamba anapanda chati mbele ya wananchi, kutwa kila siku kumchafua hapa JF kwa kumzushia scandals. Mnaishi na wasiwasi mkitetea makuwadi wenu wenye ndoto za Urais badala ya kuwashauri na wao kuchapa kazi na kujituma kama January.
 
Tuseme mathlan unachosema ni kweli, kama Jairo angepokea hizo fedha angeweza vipi kuzigawa kwa wabunge?.. ebu tupe jinsi ambavyo angeingia bungeni na kuzigawa nani angehusika na ugawaji wa vibahasha na visionekane baada ya sheria kupita na waliohusika mwanzo kupewa warning!..Huyu Jairo alikuwa na kiburi gani ama nguvu gani ya ushawishi ambayo leo wabunge woote wameshituka, halafu yeye alitaka kufanya kitu ambacho wabunge hawakutegemea wala kudhania kinaweza kufanyika.. basi kama ndio hivyo, huyu Jairo ni jinga la wajinga wote!
 
MEN LIE , WOMEN LIE...NUMBERS DONT LIE

MALAYSIA:

POPULATION: 28 million
ELECTRICITY CAPACITY (AVAILABLE) : 21,000 MEGAWATTS

TANZANIA:

POPULATION: 45 million

ELECTRICITY CAPACITY:(AVAILABLE)
630 MEGAWATTS
CCM..NGELEJA..JAIRO..mnahusika
 
Mkandara

Barua aliyoandika Jairo imevuja, sasa unaniuliza mimi kama madai kwenye barua ni ya kweli? Binafsi sidhani kwamba Jairo alikuwa anania ya kugawa hizo pesa. Pengine ni kisingizio tu ili abaki nazo, na agawane yeye na wachache.

Tusubiri tujue ni kiasi gani kilitumwa kwenye akaunti na pesa zipo wapi sasa hivi.
 
Ni wakati mzuri kwa waziri Ngeleja kung'atuka kwani ameonesha wazi hana umakini katika kazi ya kusimamia na kuiongoza wizara nyeti kama ile.
 
Pia naomba niulize kuwa je hatuna sheria ambayo itaweza kumsota rumande, huyu Jairo aliesaini barua ya kuwezesha utoaji wa rushwa ili bajeti yao dhaifu ipite, kwa muda ambao uchunguzi wa kashfa hii unafanyika?
 
mkuu wangu ni ngumu sana maana syndicate iliyohusika ni kubwa mno...ndio maana mpaka sasa hivi mkuu wa nchi amekuwa mbishi sana
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom