Wabunge wakipitisha Bajeti ya Ngeleja leo, wakaombe Kura Wanakokujua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wakipitisha Bajeti ya Ngeleja leo, wakaombe Kura Wanakokujua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Jul 18, 2011.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Chonde chonde wabunge, hasa wa CCM.

  Tunawaasa msiipitishe budget ya Wizara ya nishati na madini, mkilogwa au kuhongwa mkaipitisha mtakuwa mmetangaza mgogoro kati ya wabunge wa CCM na wananchi.

  Kumbukeni yule mgiriki aliyesema serikali ya Tanzania iko mfukoni mwake enzi za Nyerere, lugha hiyo ilitafsirika kuwepo uwezekano wa hongo, simulizi za Nyerere zinabainisha kuwa japo hawakupata uthibitisho wa hongo, ilimgharimu mgiriki kufukuzwa nchini baada kuswekwa rumande, watu wengi walimuombea upatanisho bila mafanikio, alifukuzwa na kuonywa asikanyage tena afrika mashariki.

  Waziri ama chama cha CCM aki/kikiwalaghai mkaipitisha bajeti ambayo kwa mwendelezo wake kwa mfululizo wa miaka kadhaa sasa tunaelekea kuweka rekodi ya dunia ya kuwa taifa huru la kwanza tena lenye amani tele na utajiri wa maliasili nyingi lakini kuishi gizani totoro kwenye karne ya 21!!!

  Hatutawaelewa, mtakuwa mmehongwa, na hongo ya kwanza ni sitting allowance ambayo sisi wapiga kura hatukupeni bali bunge lawapa pasipo ridhaa yetu. OLE OLE WENU!!!
   
 2. k

  kiloni JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Toka lini ccm wamekuwa upande wa wananchi nipe siku na hoja moja tu!!
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wabunge wengi wa CCM wanaangalia maslahi ya chama na sio ya wananchi, kama mbunge anasema anaikubalia bajeti kwa asilimia 100 unategemea nini
   
 4. K

  KAMBOTA Senior Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Extracted from novakambota.com

  Watanzania wametoa wito kwa wabunge kuikataa vikali bajeti ya wizara ya nishati na madini inayoongozwa na William Ngeleja na badala yake wamshinikize kujiuzulu mara moja. Wananchi mbalimbali katika miji ya Dodoma na Dar es salaam waliozungumza na waandishi wa tovuti hii wametoa kauli za vitisho kwa wabunge huku wakisema "ole wake wabunge hawa wapitishe bajeti ya Ngeleja , watajua pa kwenda kuomba kura 2015″.Wananchi hao wamewataka wabunge wote kuweka itikadi zao za kisiasa pembeni na kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kuikataa bajeti hiyo na kumshinikiza waziri Ngeleja kujiuzulu.

  Hatua hii ya wananchi inakuja ikiwa leo jioni ni siku ambayo wabunge wataipitisha au kuipinga bajeti hiyo hata hivyo wabunge wengi waliotoa maoni yao wameonyeshwa kukerwa sana na mgao wa umeme na ubabaishaji katika wizara hiyo ambapo wamediriki kuweka wazi kuwa hawako tayari kuunga mkono hoja.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  mkuu, azimio lilounda kamati teule ya bunge ilikuwa chini ya mwenyekiti ndg. mwakyembe kuchunguza kashfa ya richmond ilikuwa kwa maslahi ya watanzania, na ikiwa tutadhani hawajawahi kuwa upande wa wananchi, basi waanze leo.
   
 6. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mimi mbunge wangu ni jirani yangu,nimeshamwambia akipitisha tu,atafute pa kwenda maana akirudi maskani patachimbika.
   
 7. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pagumu. Huu ni mtihani mkubwa kwa wabunge wa chama cha magamba. Hiyo kamati ya nishati na madini walitanguliziwa bahasha mapema na inasemekana bahasha nyingi ziliendelea kusambazwa kwa waheshimiwa wabunge wa magamba na wale wa upinzani ambao ni mapandikizi kama akina kibuda. Tutegemee nini sijui kwa sababu kuna shinikizo kubwa kutoka nguvu ya umma ya kuikataa bajeti hiyo na kumlazimisha ngeleja ajiuzulu. Ila jambo moja nina hakika nalo ni kwamba hiyo bajeti itapitishwa kwa kura nyingi za wabunge wa magamba ambao ndiyo wengi bungeni. Hawa watu unajua hawana hata haya na kwa sababu ya sera yao ya kuwajibika kwa pamoja ndiyo matokeo yake ni haya kuitumbukiza nchi shimoni. Mchana huu wanakaa wenyewe kama kamati. Utakayoyasikia kutoka midomoni kwao jioni ya leo hutaamini ni wale wale waliokuwa wanaongea asubuhi. Time will tell. Suluhisho hapa ni kwamba hata kama wataipitisha kwa kura zao nyingi bungeni basi wananchi nao waonyeshe kutokubaliana nao kwa kufanya maandamano ya amani nchini kote kuwapinga wabunge na kumtaka waziri na watu wake wajiuzulu na kuwaeleza wazi wabunge wa magamba kuwa wasitarajie kurudi humo mjengoni uchaguzi ujao.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Yafuatayo ndiyo yatakayowafanya/yaliyowafanya baadhi ya wabunge waunge mkono bajeti ya Ngeleja....
  1. Hakuna hata mbunge mmoja anayejuwa adha halisi ya kukatikiwa umeme............... wakati kwa mwananchi wa kawaida.... maji ndiyo ishu ya kwanza kumuumiza maana karibu wote tunachota maji kwa kununua kwa jirani mwenye pampu..... Almost wabunge wote wana standby genset of which runs and takes the load imeadiately. The only time they do not get power is between 3 to 7 minutes when the change over between TANESCO power and their gensets takes place.
  2. Kuna wabunge hawajawahi hata mara moja kukanyaga kwenye mgodi wowote TZ hii............ They do not know what underground looks like, hawajui madini yanaibwaje........... Ndiyo maana sikuona ajabu pale SUMAYE enzi akiwa PM aliposema KMCL wanasafirisha mchanga usio na kitu.......... MY GOD ............
  3. Vikao vya kulainisha misimamo ni vya kutishana........... HUKO WALIKO WANATISHWA NA KWA WOGA WAO LAZIMA wataachia baada ya kubana asubuhi ya leo.
  4............
   
Loading...