Wabunge wakataa maelezo ya BoT,wataka taarifa yote ya ukaguzi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
Je, hatimaye Wabunge waamka? Je, Lowassa atatoa onyo kwa Wabunge wa CCM kuishinikiza siri kali kutoa ripoti ya ukaguzi wa BoT hadharani?
Posted Date::1/29/2008
Wabunge wakataa maelezo ya BoT,wataka taarifa yote ya ukaguzi
Na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

WABUNGE wametaka kupokea taarifa ya serikeli kuhusu ukaguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, badala yake wametaka wapewe ripoti halisi ya ukaguzi ili waijadili kwa undani.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji kusoma muhtasari wa ripoti kuhusu matokeo ya yake na hatua zilizochukulia na serikali.

Mara baada ya Waziri wa Fedha, kuwasilisha ripoti hiyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) alisimama na kuomba muongozo wa Spika na kutaka ripoti yote ya ukaguzi ilepelekwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Simanjiro, (CCM) Christopher Ole-Sendeki na akisema kuwa kilichowasilishwa na Waziri ni muktasari tu hivyo ingekuwa vizuri kama Bunge lingeletewa taarifa kamili ili lipate kuijadili kwa kina.

Kutokana na ombi hilo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema kuwa ombi hilo amelipokea na kwamba yote yaliyosemwa yalikuwa katika mchakato wa ofisi yake na serikali ili kuona umuhimu kwa ripoti hiyo kuletwa bungeni hapo kwa ajili ya kujadiliwa.

Hata hivyo, Spika aliahidi kufanikisha ombi hilo na kuhaidi ndani ya wiki hii atapata maelezo kutoka serikalini na kuyawasilisha bungeni.

Spika alisema kuwa atajitahidi ripoti hiyo ifikishwe bungeni kwakuwa Bunge hilo lilishatoa ombi hilo katika kikao chake cha tisa.

Ombi bado lipo hai hata kama serikali haitataka kuleta ripoti hiyo mimi sina jinsi labda itokee kitu kingine kikubwa kinachotakiwa kujadiliwa badala ya ripoti hiyo, alisema Sitta.

Awali Waziri Megji alitoa muktasari wa ripoti hiyo jambo lilopingwa na wabunge hao kuwa haikuwa na jipya na ndipo walipotaka ripoti nzima iletwe kwa ajili ya kujadiliwa bila ya kificho.

Hivi karibuni Kampuni ya Ernst & Young iligundua ubadhirifu mkubwa wa jumla ya Sh133 bilioni kutoka katika akaunti hiyo jambo lililosababisha Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi aliyekuwa Gavana Mkuu wa BoT, Daud Ballali.

Katika ripoti hiyo, Meghji alisema kwamba serikali imeipa maagizo Mamlaka ya Mapato (TRA) kufanya uchuguzi wa kina kubaini mienendo ya ulipaji kodi kodi wa makampuni yote yaliousika na endapo yatakuwa hayajalipa kodi hatua kali zitachukuliwa.

Pia BoT imeagizwa kuchunguza kuona kama kuna benki zilizohusika kupokea fedha kutoka makapuni husika kwa ili kuona kama sheria na taratibu kuhusu udhibiti wa fedha haramu haukuzingatiwa.

Katika mhango wa Ole- Sendeki aliendelea kusisitiza kuundwa kwa Tume Teule ya Bunge kuchunguza ufisadi huo. Alisema kwamba ukaguzi uliofanywa hauzuii Bunge kuunda kamati.

Hata hivyo, mpaka sasa serikali imeshindwa kueleza wazi siku maalumu atakayorudi Gavana huyo ambaye anadaiwa kuwako nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya matibabu.

Ubadhirifu wa BoT uliibuliwa na Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Willibrod Slaa katika Bunge la Bajeti mwaka jana.
 
Hapa spika sasa kabanwa na amekalia Ncha ya mkuki .Wacha tuone sasa .
 
Wasanii tuu hao na wataishia kuitwa chamber kuzibwa midomo kwa jina la nidhamu ya chama,wala usipoteze muda kufikiri watafanya chochote,na hao ambao wameambiwa wawashughulikie mafisadi katika ile report ya BOT ujue kesi ndio imeisha na hakuna hata mmoja atafikishwa mahakamani...hesabu maumivu hapo maana 133bn zimeenda na hazitarudi tena na hakuna mwizi maana zimeyeyuka katika mazingira ya kutatanisha(lugha ya mafisadi)
 
Hoja ya ufisadi moto

na Peter Nyanje, Kulwa Karedia na Ahmed Makongo
Tanzania Daima

HOJA ya ufisadi na ripoti ya ubadhirifu wa mamilioni ya fedha ndani ya Benki Kuu (BoT), imeendelea kugusa hisia za viongozi mbalimbali hapa nchini.
Ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo lilifunguliwa rasmi jana, hoja hiyo ndiyo iliyoonekana kuchukua nafasi ya kwanza miongoni mwa mambo mengine kadhaa.

Wabunge wawili, mmoja wa CCM na mwingine wa upinzani, walimtaka Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuitaka serikali iwasilishe bungeni ripoti kamili ya ukaguzi wa ubadhirifu katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT iliyoandaliwa na Kampuni ya kimataifa ya Ernst & Young.

Wabunge hao walitoa msimamo wao huo mara tu baada ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kumaliza kuwasilisha bungeni tamko la serikali kuhusu ripoti hiyo ya EPA iliyobaini ufujaji wa shilingi bilioni 133 katika mwaka wa fedha wa 2005/06.

Waliosimama na kutaka muongozo wa spika, wakitaka Bunge kupewa ripoti kamili ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) na mwenzake wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM).

Cheyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema ingawa taarifa ya Waziri Meghji ni nzuri, ilikuwa ni finyu mno ukilinganisha na ripoti kamili ya Ernst & Young.

Aidha, Cheyo alisema itakuwa ni vyema iwapo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2005/06 itawasilishwa bungeni na akataka ripoti hiyo, pamoja na taarifa ya Waziri Meghji, vyote vijadiliwe na wabunge kwa kina.

Kwa upande wake, Ole Sendeka aliposimama, alibainisha kuwa kilichowasilishwa na Waziri Meghji kilikuwa ni muhtasari tu.

Huku akimwelekea Spika, Ole Sendeka alisema: "Naomba kama itakubalika uielekeze serikali ilete taarifa kamili ya mkaguzi (Ernst & Young) na Bunge lipate fursa ya kuijadili kwa kina."

Aidha, Ole Sendeka alisema kuwa wakati alipokuwa akijadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka jana, aliomba kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza masuala kadhaa, likiwamo hilo.

"Nauliza iwapo taarifa hii (iliyowasilishwa na Meghji jana) inaathiri ombi hilo na uwezekano wa kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge?" alihoji.

Wakati Cheyo na Ole Sendeka wakizungumza wabunge wengine kadhaa walionekana wakipiga makofi kuashiria kuunga mkono mawazo hayo.

Akijibu maombi hayo, Spika Sitta alisema ingawa wabunge hao walikuwa wameshindwa kusema kanuni walizotumia kutoa hoja zao, alikuwa akikubaliana na mawazo yao.

Alisema alikubaliana na hoja hizo kwa sababu ni za msingi na kuwa wabunge bado hawajapatiwa nakala ya kanuni mpya, hivyo kuwa vigumu kujua wanapaswa kutumia kanuni ipi katika suala hilo.

"Lakini haya yote yalikuwa katika mchakato wa mashauriano baina ya Ofisi ya Spika na serikali. Bado tunaendelea kushauriana na ndani ya wiki hii nitatoa taarifa," alisema.

Aliwakumbusha watoa hoja na wabunge wengine kuwa tangu awali, alishakubaliana na hoja iliyowasilishwa na Lucy Mayenga (Viti Maalumu-CCM), aliyetaka ripoti ya hesabu za BoT za mwaka 2005/06 iwasilishwe bungeni na kujadiliwa na wabunge wote.

"Hoja hii bado ni hai na taarifa iliyotolewa leo si kipingamizi. Naamini kuwa katika wakati huu wa uwazi na ukweli serikali imeshasikia hoja zenu na itazitafakari ipasavyo na bila shaka tutafikia mahali pazuri," alisema Spika Sitta.

Katika taarifa aliyoiwasilisha jana bungeni, pamoja na kubainisha yaliyogunduliwa na Ernst & Young katika ukaguzi wa EPA na hatua zilizochukuliwa na Rais, Waziri Meghji alisema kuwa wizara yake nayo imechukua hatua kadhaa.

Alisema kuwa baada ya kupata ripoti hiyo, Wizara ya Fedha imeiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kufanya uchunguzi wa kina kubaini mienendo ya ulipaji kodi wa makampuni yote yaliyohuska katika kashfa ya EPA.

Aidha, Meghji alisema kuwa iwapo itabainika kuwapo kwa ukwepaji wa kodi, TRA imetakiwa kuchukua hatua za kisheria.

Pia wizara yake imeielekeza BoT kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa serikalini kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa mabenki ya biashara yaliyohusika na kupokea fedha kutoka makampuni yaliyotajwa kuhusika katika kashfa ya EPA, iwapo sheria, taratibu na kanuni kuhusu udhibiti wa fedha haramu zilizingatiwa.

Aidha, akifafanua kuhusu hatua ya Rais Kikwete kuwaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kuchunguza zaidi suala hilo, alisema inalenga kupata ushahidi wa kisheria utakaowezesha kufunguliwa kwa mashitaka dhidi ya watu na kampuni zote zilizohusika katika kashfa ya EPA.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana ilipata kigugumizi ilipotakiwa kueleza kuhusu hoja ya Balozi wa Marekani hapa nchini, Mark Green, aliyesema nchi hiyo ilikuwa ikisubiri maelekezo ya serikali kuhusu kurejeshwa kwa Ballali anayeaminika angali nchini humo.

Kiongozi mmoja wa juu wizarani hapo aliieleza Tanzania Daima jana kwamba, wizara yake haikuwa na mamlaka ya kuagiza kurejeshwa kwa Ballali, kwa maelezo kuwa hakuwa mwajiriwa wake.

"Sisi kama wizara si mwajiri wa Dk. Ballali na wala hatuhusiki kabisa, anayehusika hapa kumleta nchini ni mwajiri wake ambaye ni Wizara ya Fedha," alisema kiongozi huyo wa juu aliyekataa kutaja jina akisema hakuwa msemaji rasmi wa wizara.

"Mimi si msemaji na kwa bahati mbaya hivi sasa Waziri wangu, Bernard Membe, yuko Ethiopia kikazi, angeweza kulizungumzia suala hili kwa undani zaidi, ingawa ukweli utabaki kwa Wizara ya Fedha," kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilisema kwamba kama gavana huyo anatakiwa kuletwa nchini, Wizara ya Fedha inapaswa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje kuandaa taratibu zote zinazotakiwa kurejeshwa kwa mtu aliyeko nje ya nchi.

Kutoka Bunda, Mara, Ahmed Makongo, anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo, Charles Makongoro Nyerere, amewapongeza Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa na mwenzake, Kabwe Zitto, wote wa CHADEMA, kwa kuibua hoja za ufisadi na mikataba mibovu ndani ya Bunge.

Katika hatua ambayo inaweza kuibua hoja, Makongoro alitoa pongezi hizo jana wilayani Bunda, wakati akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM wilayani humo, kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu mjini Bunda, ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea miaka 31 ya CCM.

Alisema kuwa yeye binafsi alikuwa hajui chochote kuhusu suala la BoT, na mikataba kama wa Buzwagi na kama si wabunge hao kupiga kelele bungeni na hata nje ya Bunge, asingefahamu.

''Mambo haya alikuwa ayaseme Pius Msekwa ambaye ndiye aliyekuwa amealikwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu, na mimi nayasema kwa niaba yake na hata mimi ufisadi unanikera sana na hivyo nayasema kwa machungu kabisa na nitaongeza na ya kwangu," alisema Makongoro aliyemwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Alisema kuwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM, kuufahamu ubadhirifu wa BoT mapema, lakini walikuwa wakimya, hadi hapo Slaa alipolivalia njuga na kuweka wazi ukweli wa mambo, hali ambayo ilibainika kuwa ni kweli, baada ya wachunguzi wa ukaguzi wa mahaesabu walipogundua ufisadi huo wa sh bilioni 133.

''Mimi mwenyewe nililipata hilo kupitia kwa Slaa, wabunge wetu wa CCM walikuwa nalo lakini hawakulisema, hata lile la kuhusu Richmond, pia nililipata kwa Zito Kabwe...mimi nilikuwa nimelala tu kumbe wenzetu wanatumaliza......," alisema Makongoro.




 
katika mchakato wa ofisi yake na serikali ili kuona umuhimu kwa ripoti hiyo kuletwa bungeni hapo kwa ajili ya kujadiliwa.

Si dhani kama serikali inaona ni muhimu kwa hiyo ripoti kwenda huko bungeni au kuwekwa wazi, nafikiri ingeshafanya kitambo.
 
Nauliza iwapo taarifa hii (iliyowasilishwa na Meghji jana) inaathiri ombi hilo na uwezekano wa kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge?" alihoji.
Hizi tume mimi kwa kweli zinanikera, hakuna njia nyingine yakufatilia mambo hadi kuwe na tume?

''Mimi mwenyewe nililipata hilo kupitia kwa Slaa, wabunge wetu wa CCM walikuwa nalo lakini hawakulisema, hata lile la kuhusu Richmond, pia nililipata kwa Zito Kabwe...mimi nilikuwa nimelala tu kumbe wenzetu wanatumaliza......," alisema Makongoro.
Kuwa chama cha upinzani haimaanishi ni kuwa adui wa chama tawala, huu mtazamo unachangia kudidimiza uchumi wetu.
Watu wamekuwa wakiogopa kutetea au kujenga hoja, kuhofia kuimaliza CCM!
 
Kwa uzoefu wangu vitaletwa visingizio na spika atakuwa anatetea mnooooo!
 
Nakubaliana na wabunge kutaka taarifa kamili ifikishwe bungeni!Lakini bado naona kuna spin ya hali ya juu!
Namshangaa Mama Meghji kwa kudai eti kampuni hizo zichunguzwe kama zimelipa kodi!Nani anajali kama wanalipa kodi wakati pesa walizotumia kwenye biashara ni za wizi?Pesa za wananchi!
Ni wazi kwamba hizo pesa zilitolewa kwa kupitia taratibu zote..sasa TUNATAKA HAO WALIOIDHINISHA MALIPO HAYO KUTUAMBIA NI VIGEZO GANI VILITUMIKA KUZITOA!NI PESA NYINGI SANA!HATA AUDITOR WA SERIKALI ANATAKIWA NAYE ATOE MAELEZO!Ila pesa zilipitia taratibu zoote..ila uchunguzi wa kwamba zilikuwa zinakwenda wapi ndio swali walilotakiwa kujiuliza..anyways assume walikuwa wanajua!Je si ni wazi kuwa pesa hizo zilikuwa kwenye akaunti ya madeni ya nje?Kwanini zilitolewa huko kwenye hiyo akaunti?Ama madeni ya nje ndio serikali na hayo makampuni?Huwezi kuona kwamba kwasababu akaunti ya madeni ya nje ni rahisi kutofatiliwa kwasababu wanaamini kuwa everyone knows pesa hizo zitaishia kulipa madeni ya nje?Maswali ni mengi na yanahitaji serious responding zaid ya kuawahoji watanzania peke yake na kudai kuwa Balali hajahusika!Kwani walikuwa hawaoni kuwa hizo pesa zinaenda kwenye makampuni badala ya madeni ya nje?We unafikiri kwanini Mama Meghji aliandika barua na kudai kuwa sheria a nchi zimefuatwa?si alijua wazi kuwa allocation ya hizo funding ni tofauti na lengo lake halisi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom