Wabunge ‘wailipua’ tena TICTS wadai inahujumu nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge ‘wailipua’ tena TICTS wadai inahujumu nchi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pdidy, May 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Wabunge ‘wailipua’ tena TICTS wadai inahujumu nchiNa Ramadhan Semtawa

  JINAMIZI la Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Service (TICTS), limezidi kutawala kufuatia hatua ya baadhi ya wabunge kuilipua tena wakidai kuwa inahujumu uchumi wa nchi kwa kudhoofisha utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam.

  Wabunge hao walisema hali hiyo imekuwa ikisababisha wafanyabiashara wenye shehena za mizigo,kukimbilia Mombasa, Kenya.

  Kitendo cha wabunge kuilipua tena TICTS kimekuja wakati serikali ikiwa imeongeza mkataba wa awamu ya pili kwa kampuni hiyo.

  Hata hivyo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesema mkataba huo umekiuka sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004.

  Wakichangia hoja katika Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jana, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha, walihoji nguvu za TICTS kiasi cha kuifanya TPA na serikali kushindwa kuichukulia hatua baada ya kushindwa kazi.

  Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Siraju Kaboyonga, alisema kama TPA na serikali wanaipenda TICTS iendelee, ni vema wakaondoa ukiritimba wa kampuni hiyo, ili wadau wengine watoe huduma.

  Kaboyonga ambaye kitaaluma ni mchumi, alisema bandari ni sawa na mgodi wa madini, lakini alionyesha masikitiko yake kuhusu namna inavyodhoofishwa na kupuuzwa kwa uwekezaji mkubwa.

  Huku akitoa mifano ya nchi za Singapore, Dubai, Msumbiji, Afrika Kusini na Kenya, ambazo bandari zake zina tija na ufanisi , Kaboyonga alisema ukiritimba wa TICTS, unaua Bandari ya Dar es Salaam.

  "Mimi nachukulia bandari kuwa sawa na mgodi, watu tunaangalia migodi ya madini, lakini bandari zetu kama ya Dar es Salaam kwa kuangalia kijiografia, ni mgodi tosha kutokana na kuzunguukwa na nchi zinazotuhitaji, " alisema.

  Mapema taarifa ya TPA iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Happines Senkoro, ilionyesha kuwa moja ya changamoto ni kushuka kwa tija ya kupakia na kupakua kontena katika TICTS.

  Senkora, alisema TICTS kwa sasa inafanya mizunguuko 18 ya upakuaji wakati mkataba unaitaka kufanya mizunguko 25.

  Ripoti hiyo, pia inaonyesha kuwa ukaaji wa makontena bandarini umeongezeka kutoka wiki moja hadi siku 25 kwa mizigo ya Tanzania na siku 14 kwa mizigo ya nchi jirani.

  Akichangia kuhusu kupungua kwa mzunguko wa kupakua makontena kutoka 25 hadi 18, Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM) Dk Omari Mzeru, alihoji, kama TICTS imeshindwa kukidhi masharti ya mkataba, kwanini wasichukuliwe hatua. "Kama TICTS wameshindwa kukidhi masharti ya mkataba, badala ya mizunguuko 25 wakafanya 18, TPA imefanya nini kuwachukulia hatua?" alihoji Dk Mzeru.
   
 2. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2017
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,438
  Likes Received: 12,607
  Trophy Points: 280
  Hii thread haina hata mchangiaji mmoja
   
 3. F

  Fofader JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Review ya mkataba na negotiations zimefanyika na sasa rental fee watakayolipa ni $14m badala ya $7m ya hapo awali. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya habari ITV leo.
   
 4. 10000

  10000 JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2017
  Joined: Oct 18, 2013
  Messages: 750
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 80
  thread ya 29/05/2009 bwana yule sasa anatumbua tumbua mpaka huko TICS tujisent wnacholipa serikali kimeongezwa
   
 5. jimmyfoxxgongo

  jimmyfoxxgongo JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2017
  Joined: Jan 23, 2013
  Messages: 3,219
  Likes Received: 4,823
  Trophy Points: 280
  Du hii thread ndo tunaijua umuhimu wake leo
   
 6. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2017
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,385
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Tutaelewana tu..
   
Loading...