Wabunge waibua ufisadi wa mabilioni D’Salaam

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
mremar.jpg
Mwenyekiti wa LAAC, Augustine Mrema

Patricia Kimelemeta na Ramadhan Semtawa
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeibua tuhuma za ufisadi wa Sh2.7 bilioni katika mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Gongo la Mboto, Dares Salaam uliopaswa kufanywa na Kampuni ya East Africa

Meat (EAMC).Mradi huo ulipaswa kutekelezwa kati ya mwaka 2005/06 kwa ushirikiano wa jiji na Manispaa tatu za Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye kikao kati ya kamati yake na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwenyekiti wa LAAC, Augustine Mrema alisema kampuni hiyo ya Malaysia ndiyo iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa machinjio hayo.

Mrema alisema katika mradi huo, Halmashauri ya Jiji iliingia mkataba wa kughushi na EAMC, huku wakiwashawishi watendaji kushiriki kwenye ujenzi wa machinjio hayo yanayodaiwa kuwa ya kisasa.

Alisema kutokana na hali hiyo Halmashauri ya Kinondoni ilitoa Sh229milioni wakati ya Ilala ilitoa Sh364miloni, Temeke ilitoa Sh224milioni huku jiji likitoa Sh1.2bilioni.

Alisema kutokana na hali hiyo, fedha hizo zimepelekwa kwenye miradi huo ambao mpaka sasa haujatekelezeka jambo ambalo linaonyesha kuwa kuna baadhi ya wajanja ambao wamechukua fedha hizo.
"Tunajua kabisa kuwa kuna baadhi ya vigogo wameshiriki kuwarubuni watendaji wa halmashauri kwa ajili ya

kutekeleza miradi hewa, hatutakubali na kila aliyeshiriki atachukuliwa hatua za kisheria," alisema Mrema.
Alisema mbali na hilo, baadhi ya vigogo hao ndiyo walioshiriki kwenye kashfa ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambalo ripoti yake bado inasubiriwa ikabidhiwe serikalini kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mrema alisema kutokana na hali hiyo, LAAC itawasilisha taarifa hizo kwa watendaji wakuu ili waweze kuangalia hatua stahiki za kurudishwa kwa fedha hizo katika halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wahusika walioshiriki kwenye utapeli huo.

"Haiwezekani hata kidogo watu wachache wanufaike na rasilimali za taifa kwa manufaa yao, jambo ambalo limesababisha kuingia mikataba feki ambayo wanajua kabisa kuwa haiwanufaishi wananchi. Lazima fedha hizi zirudi," alisema.
Meya: Kampuni imefilisika

Hata hivyo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi alisema kampuni hiyo imefilisika na kwamba hakuna mtu atakayeweza kulipa deni hilo. Kutokana na hali hiyo, alisema watakaa na halmashauri za manispaa ili kuangalia jinsi ya kutatua matatizo hayo.

"Kampuni yenyewe imefilisika, nani atalipa deni hilo? Hakuna kwa sababu hata jiji ni miongoni mwa watu waliotapeliwa japo tulikuwa tumeingia ubia lakini kilichofanyika ni kwamba mradi huo haujatekelezeka," alisema Dk Masaburi.
Alisema machinjio hayo yalitakiwa kujengwa mwaka 2006, lakini mpaka sasa hayajengwa na wala hakuna eneo la ujenzi.

Meya Masaburi alisema halmashauri hizo zilitoa fedha hizo na kudaiwa kuwa zimetumika kwenye upembuzi yakinifu na kuongeza kwamba, ilipofika mwaka 2009, madiwani wa jiji na manispaa walitaka ufafanuzi kuhusu suala hilo na kuitaka jiji kujiondoa kwenye mkataba huo jambo ambalo lilisababisha halmashauri hizo kudai fedha zao ambazo mpaka sasa hazijalipwa.

Alisema wakati hayo yakiendelea, tayari kampuni hiyo ilikuwa imefilisika na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuendelea na mkataba au kurudisha fedha.

"Meneja wa kampuni hiyo ambaye ni raia wa Zimbabwe aliyejulikana kwa jina la Benjamin Chipazi ni miongoni mwa watu waliotapeliwa, anadai mafao yake ya zaidi ya Dola za Marekani 150,000, lakini ameshindwa kulipwa kwa sababu hakuna mtu aliyerithi madeni hayo," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, jiji haliwezi kurithi madeni ya kampuni hiyo na kwamba kila mmoja anapaswa kutambua kuwa katika mkataba huo wametapeliwa.
Iddi Simba Mwenyekiti

Alipoulizwa jana, Mwenyekiti wa EACM, Iddi Simba alikiri kuwa kampuni hiyo na ilikuwa ijenge mradi huo.
Alisema EACM ilikuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa kuhusisha jiji na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam wakati huo alikuwa akiingia kwenye vikao akiwa mjumbe.

Alisema awali, jiji na manispaa zake tatu lilibuni mradi huo wa kujenga machinjio ya kisasa katika kiwanja chake cha Gongo la Mboto kilichokuwa na thamani ya Sh bilioni moja ambacho kilitumika kama sehemu ya mchango wa fedha katika hisa zake.

Alisema katika mkataba huo, Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni kila moja ilipaswa kutoa Dola 500 za Marekani ikiwa ni mchango kwa hisa zake hivyo kufanya tahamani ya mtaji kufikia Dola 2.5milioni.
"Lakini, kilichotokea ni kwamba, fedha hizo za manispaa hazikutolewa katika kipindi ambacho mradi ulipaswa

kuanza. Hivyo, kampuni ikafilisika kwa sababu hata watu wengine waliotaka kuwekeza fedha zao walisita baada ya kuona manispaa hizo zinasuasua," alisema.

Alisema kampuni iliyofanya upembuzi yakinifu ilikuwa ya mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina tunalihifadhi kwa kuwa hakupatikana kujibu madai hayo jana).
Simba alisema hakuna fedha ambayo imeliwa na EACM kwani hata kiwanja hicho ambacho ni mali ya halmashauri ya jiji, bado kiliachwa mikononi mwa mamlaka hiyo.

Kuhusu ni kiasi gani cha fedha ambacho manispaa hizo tatu zilitoa hadi kampuni hiyo ilipokuwa ikikaribia kufilisika, Simba alijibu, "Sijui. Wewe umenikurupusha tu hapa sina nyaraka zozote."
Lakini alisisitiza kwamba EACM haikuwahi kuuza kiwanja hicho kwani bado kiliachwa mikononi mwa jiji hilo hadi kampuni ilipofilisika.
Wabunge waibua ufisadi wa mabilioni D
 
hizi kamati za bunge zimeshanichosha,kazi kuibua ufisadi tu lakini kuiwajibisha serikali hawawezi!!!
 
Nimechoka na hizi habari, kila siku vumbua vumbua, utafikiri akina sir Isaac Newton.
Hizi kamati hazina hata meno ya kumung'unya nyama zilizosagwa zinamaliza tu rasilimali kwa miposho wanayolipana.
Wanakuwa kama mbwa ambao hawana meno ya kung'ata, wao kubweka tuu!!
Mbona hatuwaoni wale watuhumiwa kwa pilato??
Eti mtu kaiba bil 6 halafu anapewa adhabu ya kukatwa asilimia 15 ya mshahara wake (say Tshs 1,500,000) hivi hii ni akili au tope?
Badilisheni nyimbo hizi, aaaaaaggghhhhhh!!!
 
Hii ndio tanzania yetu! Mwizi anaweza kukufanga wewe unayedai haki!! Jamani tunakwenda wapi!! Huyu iddi simba kila alipogusa ameharibu na bado anapeta!! Huyu mtu anahitaji kufilisiwa!! Ninasikitika hata kwenye mkutano wa wazee wa dar alikuwa msemaji!! What a shame is this!!!
 
kama kwenye UDA wamemshindwa kuwashughulikia Masaburi na Simba sijui kwenye hili sababu kwenye hiyo kamati ya mzee wa kiraracha wanajitahidi kweli kukamata mchwa lakini sijawahi kusikia wamefikishwa mahakamani labda kwa hili tuvute muda tuone move itaishaje
 
Hii ndio tanzania yetu! Mwizi anaweza kukufanga wewe unayedai haki!! Jamani tunakwenda wapi!! Huyu iddi simba kila alipogusa ameharibu na bado anapeta!! Huyu mtu anahitaji kufilisiwa!! Ninasikitika hata kwenye mkutano wa wazee wa dar alikuwa msemaji!! What a shame is this!!!
Tanzania nchi yetu inahitaji total overhaul, utawala uliopo haufai kabisa ni wa kijizi tuu, wezi hawachukuliwi hatua zozote wanapeta tuu!!!!!!!!

 
Aisee hii nchi tulete management ya wazungu,tuweke serikali pembeni wakae wazungu kama 10. Mmoja wizara miundombinu, mmoja afya, mmoja fedha, mmoja madini, mmoja nk halafu wote wawe wanawajibika bungeni.wa Canada wazuri sana kwa hizo kazi.
 
Back
Top Bottom