Wabunge waibua ufisadi Sh25 bilioni Maliasili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waibua ufisadi Sh25 bilioni Maliasili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo (Kushoto) akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii walipokuwa wakiwasilisha taarifa za Wizara hiyo katika Osifi ndogo za Bunge jijini Dar ES Salaam jana.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Zainab Vullu.Picha na Venance Nestory​

  Patricia Kimelemeta
  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) imebaini utata wa matumizi ya zaidi ya Sh25 bilioni katika Wizara ya Maliasili na Utalii, huku watendaji wa wizara hiyo wakikosa takwimu za idadi ya wanyamapori na vitalu vya uwindaji.

  Kashfa hiyo imezidi kuitikisa wizara hiyo kwani hivi karibuni ilikumbwa na kashfa nyingine ya utoroshaji nje twiga wakiwa hai, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

  Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo alisema fedha hizo zinatokana na mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya wizara hiyo.

  PAC kwa muda wa wiki nzima imekuwa ikipokea taarifa za wizara mbalimbali za Serikali, ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambako iliibua ukata katika balozi za Tanzania nje na juzi, ilikutana na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kubaini utata wa matumizi ya Sh1.5 bilioni za mafuriko ya Kilosa.

  Cheyo alisema kamati yake katika Wizara ya Maliasili na Utalii pia ilibaini watendaji wa wizara hiyo kutokuwa na takwimu za wanyama, vitalu vya uwindaji, takwimu za watalii wanaoingia na kutoka pamoja na rasilimali mbalimbali zinazoweza kuiingizia nchi mapato, jambo ambalo limesababisha kupata hati chafu kwa miaka mitatu mfululizo.

  “Nashindwa kujua mnafanyaje kazi wakati hamna hata takwimu za wanyama wala watalii wanaoingia nchini, jambo hili linaisababishia Serikali kushindwa kuingiza mapato na kuweka mianya ya wizi, kutokana na hali hiyo mnapaswa kubadilika na kufanya kazi zenu kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na nchi,”alisema na kuongeza.


  “Kutokana na ripoti iliyowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini kuwa zaidi ya Sh25 bilioni zimetumika kinyume na taratibu katika kipindi cha mwaka jana, na kwamba matumizi hayo hayako kwenye vitabu vya Serikali wala hazina,” alisema Cheyo.

  Alisema hilo ni kosa kwani watendaji walipaswa kuwasilisha fedha hizo hazina ikiwa ni pamoja na kuandika mchanganuo wa matumizi ili taarifa zake ziwekwe kwenye vitabu vya Serikali.

  Lakini, Cheyo alisema kilichofanyika ni kuchukua uamuzi mkononi wakati wakijua kuwa wanachokifanya ni kinyume na sheria.

  “Huwezi kuchukua fedha za Serikali bila ya kutoa maelezo, fedha zinazoingia kwenye wizara zinapaswa kuwasilishwa hazina ili ziweze kuhakikiwa ndipo ziweze kurudishwa kwenye wizara husika kwa ajili ya matumizi husika. Lakini, kilichofanyika wizara hii ni kuchukua mgawo wao mapema huku wakijua wanachokifanya ni kosa,”alibainisha.

  Alisema kutokana na hali hiyo, mapato ya wizara hiyo yamekuwa yakishuka kila mwaka kutokana na watendaji wake kutokuwa makini, hali ambayo inaonyesha wazi kuwa, wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

  Kwa mujibu wa Cheyo, makadirio ya ukusanyaji wa mapato ya wizara hiyo kwa mwaka 2010 yalikuwa ni Sh1.7trilioni, lakini walikusanya Sh79bilioni, mwaka 2011 mapato yalishuka na kufikia 52bilioni na sasa hawana hata shilingi.

  Alisema idadi ya watalii wanaoingia nchini ni kubwa, lakini fedha zinazowasilishwa serikalini ni ndogo ambazo hazilingani na idadi hiyo, hali ambayo inaonyesha wazi fedha hizo zinapotea kinyume na taratibu.

  Alisema idadi ya watalii wanaolala kwenye hoteli za hapa nchini ni kubwa, lakini fedha zinazowasilishwa serikalini ni ndogo na hazilingani na idadi hiyo ya watalii, jambo ambalo linaonyesha wazi kuna wajanja wanatumia nafasi hiyo kuiba mapato ya Serikali.

  Cheyo aliongeza kwamba wizara hiyo ni nyeti kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali, lakini watendaji wake wanashindwa kuwajibika ipasavyo jambo ambalo limesabababisha fedha nyingi kutumika kinyume na utaratibu.

  Alifafanua kwamba kutokana na hali hiyo, watendaji hao wa wizara wanapaswa kuweka mifumo ya uwazi ya ukusanyaji wa mapato ili kila mtu aweze kubaini kiasi kilichoingia, kilichotoka na matumizi yake na si kuweka usiri ambao unasababisha mianya ya wizi.

  Kamati hiyo imewaagiza watendaji hao kukaa na hazina ili waweze kuhakiki mapato na kuwasilisha taarifa hizo kwenye vitabu ya Serikali.

  Mbali na hilo, pia PAC imewataka watendaji wa wizara hiyo kuweka utaratibu wa kuwataka watalii wanaoingia nchini kulipa fedha za Kitanzania na si kutumia fedha za kigeni kama ilivyo sasa.

  Kauli ya Katibu Mkuu
  Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi alikiri kuwepo kwa wafanyabiashara wajanja wa hoteli wanaokwepa kulipa kodi na kusababisha wizara hiyo kukusanya kiasi kidogo cha fedha kila mwaka.

  “Ni kweli, kuna baadhi ya wafanyabiashara wa hoteli kuwa wajanja na kushindwa kodi stahiki, lakini sasa hivi tunabadili mfumo na kuwepo mfumo wa kielectronic ili tuweze kujua idadi ya watalii walioingia nchini,”alisema Tarishi.

  chanzo.
  Wabunge waibua ufisadi Sh25 bilioni Maliasili
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi wabunge ndio huwa wanaibua au huwa utata/matumizi mabaya yamebainishwa kwenye taarifa ya Makaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali?
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hapana wao huwa ni wasemaji tu mana sio wakaguzi.
   
 4. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wakishaibua then wanachukua hatua gani???
   
 5. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizi stori kila siku tu tunazisikia, mi nadhani ni jinsi tu ya kuhalalisha posho zao tu, maana baada ya hapo hutasikia chochote kimefanyika!
  hivi ile ishu ya TCRA imeishia wapi? Impact ya hizi kamati za bunge mia bado kuiona kabisa
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tuliisha wahi kuandika hapa kuwa huko wizara ya maliasili na vitengo vyake kama TANAPA na vingine matumizi ya fedha za umma zimekuwa kama zao!!!! Tulimuomba Mheshimiwa Lema afutile kwa maana hilo ni eneo, kujua vyanzo vya mapato mkoa wa ARUSHA North Tourist Zone !!!! Hiyo itakuwa ni kidogo miaka yote ni fedha ngapi zilizo potea kwa njia hiyo?????

   
 7. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni CCM!
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua wabunge siyo executive ila wakati mwingine huwa wanataka kuwa executive. wanachotakiwa si kutoa tu maneno ya sijui hela zatafunwa sijui nini na makelele mengine kibao bila matendo. Mimi naona ni kama usanii tu; wanatakiwa wawabane wanasiasa (mawaziri) ndani y bunge hadi wapate maelezo ya kutosha juu ya tuhuma wanaziona kwenye repoti za wakaguzi. Lakini hizi kauli za naunga mkono kwa asilimia mia hututafika kokote!
   
 9. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Nashukuru Mh Spika kwa kunipa nafasi hii adimu. Najua pesa zimeliwa lakini naunga mkono kwa asilimia mia. Ahsante. Magamba style!!
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Lema akaja na jibu gani?
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yes ndo zimwi linalokula Tz
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tanzania ya kesho itajengwa leo na hasa vijana tuchukue hatua ya vitendo na si maneno matupu
   
 13. K

  Kilete New Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli haya mambo sasa yametosha!Wizara hii inaonekana ina mabo kweli,kwani ni wizara ni miongoni mwa wizara chache zisizo na naibu waziri!Pia mwisho mwa mwaka jana Mh.waziri( Maige) alitamba kwamba huko jimboni mwake amechangia shughuli za kimaendeleo zenye dhamani ya karibu shilingi za Kitanzania milioni mia tano(5M),je hizi alizipata wapi?Je mshahara na marupurupu yake vina hiyo dhamani?Nafikiri hapo ndipo tume inatakiwa ianzie kufanya uchunguzi wake ktk kutafuta ukweli wa mambo!
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Bunge na kamati zisizokua na meno!! Hao wezi ndio wameshikiria uchumi wa nchi,wakikamatwa uchumi utayumba bwana,bora waendelee kuiba!
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kamati inaenda kumchunguza sugu na mnyika hahaaaa kazi kweli kweli,kina chenga,lowassa,shimbo,kikwete,legal ofisa(rz1) etc wanadunda tuuuu kweli tz shamba la bibi,hii nchi haitakomboka mpaka kiongozi(fisadi) apigwe risasi adharani na mwananchi hili iwe fundisho!
   
 16. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mh ukistaajabu hili hujui lile! Nchi hii tajiri bwana haiwezi kwisha wiki hujasikia billions of money zimegundulika kuibiwa then hakuna kinachofata. Toka saa hii siwezi ita Tanzania maskini, ni tajiri mjinga, wenyewe mnasema babu jinga kaa ufikiri mali zako zinaliwa.
   
 17. D

  Davie Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ivi kila siku hii kamati inaibua utata juu ya matumizi ya mabaya ya fedha za umma...na hakuna kitu kinafanyika...
  maana cjawahi sikia taarifa ya kuwa waliosababisha hiyo hasara wamechukuliwa hatua wala nini..
  kila sku ni taarifa ya ''TUMEIBUA UFISADI".......ETC..
  Then what next...
   
Loading...