Wabunge wahoji uhalali wa Magufuli kuhamamisha fedha za Muungano, kujengea barabara Mwanza

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Baadhi ya Wabunge wamehoji uhalali wa kisheria wa Rais John Magufuli kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wabunge hao walihoji hilo wakati wa semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini hapa Dar es Salaam, iliyoendeshwa na Dk Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali alihoji juu ya mamlaka ya Rais katika kutumia fedha ambazo zilishapangiwa bajeti na Bunge na kuzipeleka kwenye maeneo mengine.

Alihoji pia juu ya nidhamu ya Serikali katika usimamizi wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Mbunge huyo alisema dhana ya mgawanyo wa madaraka haipo kwa sababu Serikali ina nguvu kuliko Bunge na Mahakama hivi sasa.

Alisisitiza kuwa nguvu hiyo ndiyo inayomfanya Rais afanye kitu chochote anachotaka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.

Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.

“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.

Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.

Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.

“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo. Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.

Pia, Sungusia alisema, “Fedha ambazo Rais hawezi kuziingilia ni zile zilizo kwenye consolidated fund (mfuko hodhi), nje ya hapo anaweza kufanya lolote,” alisema mwanasheria huyo.

Source: Mwananchi
 
Kuna Bomu linapikwa na wahafidhina hapa, tusijeshangaa bajeti kukwama, na bunge kuvunjwa, na uchaguzi kuitishwa na chama flani kikateuwa mgombea mwingine.
 
Hao wabunge hawana jipya kabisa. Kwa miaka yote ni lini bajeti imeheshimiwa? Mara zote wanaruhusu pesa inatumiwa kwenye vifungu vya hovyo. Miaka iliyopita bajeti ilichotwa kwa ajili ya safari na hakuna mbunge aliyerefusha mdomo.

Kwa sasa pesa inapelekwa kwenye matumizi ya maana wao wanahoji. Hiyo pesa ingeongezea posho zao wangeuliza?
 
Hiki ni kipindi cha cheap politics. Baadhi ya wabunge, kwa ukosefu aidha wa elimu au simple logic, wana jitokeza tu na hoja za hovyo angalao tu waonekane jimboni kwao au ndani ya vyama vyao kwamba nao wanasema kitu. Hata akina Lugola walivaa kofia za kininja bungeni kuwa pumbaza wananchi kwamba wao ndo wapiganaji dhidi ya rushwa na ufisadi.
 
Ila ukweli, Mh. Anaendesha nchi kama anaendesha familia yake, kilichopatikana mda huo huo kinapangiwa matumizi, hamna plan wala nini, sikosoi utendaji wake, hakika tumepata raisi, ila tunataka mpango madhubuti wa mda mrefu

Majipu endelea kuyatumbua baba, ila mambo ya fedha na mengineyo pia jaribu kuachia wahusika, kila mtu awajibike panapostahili, mkono wako unagusa kila mahali sidhani kama kuna ambaye ataenda kinyume au tofauti na inavyokusudiwa
 
Kuna Bomu linapikwa na wahafidhina hapa, tusijeshangaa bajeti kukwama, na bunge kuvunjwa, na uchaguzi kuitishwa na chama flani kikateuwa mgombea mwingine.

nakuelewa awe na tahadhari hiyo mana chama chake ndo kinapiga lapa kwenda mahakamani.
 
Sasa kama Zanzibar inachangia kwenye mfuko wa pamoja wa Muungano,tena inachangia zaidi kuliko hako kaasilimia 3 anakopewaga..
inakuwaje hela zinazohusu Muungano ziishie bara,kama yalivyoishia mabilioni ya Zanzibar yaliyokuwepo kwenye bank ya East Afrika,yaliyoishia huko BOTanganyika na hela nyengine kutoka FIFA,UN n.k. eti hata foreign exchange,utalii,ushuru wa bandari ya zanzibar,makusanyo yote kuishia bara..
zamani wabara walienda zanzibar kuchukua vitu..
mtanganyika kaenda mbali zaidi kwa kuigomea zanzibar isijiunge na OIC ili ikose mikopo isio riba na bidhaa muhimu kama matrekta..
Mtanganyika tunaelewa kwa nini unalilia Muungano..
 
Alipohamisha za sherehe ya Uhuru kujenga barabara za Dar hao wabunge walikaa kimya, leo kahamishia Mwanza maneno kibao. Hii nchi ni yetu sote acha JPM agawe keki ya taifa maeneo yote sio kila mtu akimbilie Dar
 
Kuna Bomu linapikwa na wahafidhina hapa, tusijeshangaa bajeti kukwama, na bunge kuvunjwa, na uchaguzi kuitishwa na chama flani kikateuwa mgombea mwingine.
......hio itakuwa tekiniko misteki, kwa wabunge wa chama changu wengi hawatarudi kwa sababu tumegundua ni wala rushwa, afu ndo mtajua taasisi ya uraisi nguvu yake ikoje, hayo maneno yenu ya kwenye gahawa tu
 
Hao wabunge hawana jipya kabisa. Kwa miaka yote ni lini bajeti imeheshimiwa? Mara zote wanaruhusu pesa inatumiwa kwenye vifungu vya hovyo. Miaka iliyopita bajeti ilichotwa kwa ajili ya safari na hakuna mbunge aliyerefusha mdomo.
Hao wabunge hawana jipya kabisa. Kwa miaka yote ni lini bajeti imeheshimiwa? Mara zote wanaruhusu pesa inatumiwa kwenye vifungu vya hovyo. Miaka iliyopita bajeti ilichotwa kwa ajili ya safari na hakuna mbunge aliyerefusha mdomo.

Kwa sasa pesa inapelekwa kwenye matumizi ya maana wao wanahoji. Hiyo pesa ingeongezea posho zao wangeuliza?

Kama huko nyuma kulitokea makosa na wabunge hawakuhoji matumizi ya fedha haina maana hawana haki ya kuhoji maamuzi ya rais hivi sasa. Mimi namsifu rais Magufuli kwa kazi anayoifanya mpaka sasa lakini haina maana asifuate sheria kwenye maamuzi yake. Sina uhakika kama amevunja sheria au la, lakini nategemea yeye kama rais atakuwa na wataalam wa kumshauri kisheria.
 
Hii button ya "LIKE" ingekuwa ina ukubwa mbalimbali ningekupa ile kuuubwaaa kabisa
 
Alipohamisha za sherehe ya Uhuru kujenga barabara za Dar hao wabunge walikaa kimya, leo kahamishia Mwanza maneno kibao. Hii nchi ni yetu sote acha JPM agawe keki ya taifa maeneo yote sio kila mtu akimbilie Dar

Kumbuka kuwa Mwanza ni jiji kama Dar es salaam tu.
Usichukulie kama ni eneo la watu fulani. Majiji au miji hua haina mwenyewe.

Na pia ukumbuke hizo ni hela za Muungano.
Rais wa Zanzibar alitakiwa ashirikishwe.
Fedha nyingine zilipaswa zipelekwe Zanzibar sio Tanganyika peke yake.
 
Kama huko nyuma kulitokea makosa na wabunge hawakuhoji matumizi ya fedha haina maana hawana haki ya kuhoji maamuzi ya rais hivi sasa. Mimi namsifu rais Magufuli kwa kazi anayoifanya mpaka sasa lakini haina maana asifuate sheria kwenye maamuzi yake. Sina uhakika kama amevunja sheria au la, lakini nategemea yeye kama rais atakuwa na wataalam wa kumshauri kisheria.
Nimeuliza wakati bajeti za hovyo zinapitishwa walikuwa wapi? Kila mwaka bajeti inayopitishwa siyo hiyo inayotumika. Kila mbunge anaelewa na hakuna aliyewahi hoji matumizi ya hovyo na misururu ya safari za US pesa ilikuwa inatoka wapi.

Kwa wema wa magufuli leo hii eti mbunge anauliza juu ya maamuzi ya Rais. Wakati wa Kikwete hakuna aliyeuliza na hata jina lake kutajwa Bungeni ilikuwa marufuku kwa kanuni za Bunge. Lukuvi alikuwa pale kila siku kuzuia jina la rais kutajwa.
 
Nyerere aliwahi kusema Katiba hii rais anaweza kuitumia kuwa dictator. Naona magufuli kaamua kuitumia hivyo
 
Alipohamisha za sherehe ya Uhuru kujenga barabara za Dar hao wabunge walikaa kimya, leo kahamishia Mwanza maneno kibao. Hii nchi ni yetu sote acha JPM agawe keki ya taifa maeneo yote sio kila mtu akimbilie Dar
hiyo kweli mwanakwetu
 
Kumbuka kuwa Mwanza ni jiji kama Dar es salaam tu.
Usichukulie kama ni eneo la watu fulani. Majiji au miji hua haina mwenyewe.

Na pia ukumbuke hizo ni hela za Muungano.
Rais wa Zanzibar alitakiwa ashirikishwe.
Fedha nyingine zilipaswa zipelekwe Zanzibar sio Tanganyika peke yake.
haya mambo JPM anafanya kwa zamu ukitaka afanye kila kitu leo haiwezekani mpeni muda hata huko michenzani patajengwa tu
 
Back
Top Bottom