Wabunge wahoji Sh19bn kwa ajili ya chai, vitafunwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wahoji Sh19bn kwa ajili ya chai, vitafunwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by idumu, Jun 18, 2009.

 1. idumu

  idumu Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma
  WABUNGE wameendelea kuichambua Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2009/10, huku mbunge akihoji uamuzi wa serikali kutenga Sh19 bilioni kwa ajili ya chai na vitafunwa kwa wizara mbalimbali.

  Kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya chai na vitafunwa, kimewekwa katika kipindi ambacho nchi inapita katika wakati mgumu kiuchumi kufuatia mtikisiko wa uchumi duniani.

  Akichangia hotuba hiyo katika siku ya tatu ya mjadala wa hotuba bajeti, Mbunge wa Kojan, Salimu Yusuph Mohamed (CUF) alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa ikizingatiwa kwamba, Watanzania walio wengi wanaishi katika dimbwi la umaskini.

  “Tumeona bajeti ya safari za nje ni Sh34 bilioni na leo nimepitia bajeti hii naona kuna Sh19 bilioni ambazo zimetengwa kwa ajili ya bajeti ya chai kwa wizara mbalimbali, hii inashangaza sana. Iko wapi huruma ya serikali au ndiyo ile style (mbinu) ya mamba, ambaye anamuua na kumla binadamu huku machozi yakimtoka; utafikiri analia kumbe anafurahi. Kwa hiyo serikali nayo inafanya ‘style’ ya mamba kwa wananchi.”

  Akitoa mchanganuo huo kwa baadhi ya ya fungu la chai za wizara, alisema Wizara ya Fedha na Uchumi imetengewa Sh500 milioni huku wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikitengewa Sh 226.3 milioni.

  “Chai siyo mbaya, lakini tunapaswa kuangalia nchi yetu iko katika kipindi gani kwani sasa tuko katika wakati mgumu, hivyo kutenga kiasi hicho kwa ajili ya chai tu, nafikiri si sahihi,” alisisitiza mbunge huyo.

  Alikumbusha bunge kwamba, limepunguzwa muda kukutana ili kubana matumizi, hivyo hakuna sababu za kuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyo muhimu sana kwa taifa.

  Mbunge huyo alihoji: “Tumepunguza muda wa mkutano wa Bunge ili kubana matumizi, sasa haya mambo mengine ambayo tumeona kama safari za serikali kutengewa Sh34 bilioni yana maana gani?”

  Kwa ufafanuzi, alisema Watanzania walio wengi kwa sasa wanaishi katika hali ngumu ya umaskini kutokana na kuwa na kipato kidogo, ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya maisha.

  Mbunge huyo akisisitiza hilo, alisema hata takwimu za kimataifa (Malengo ya Maendeleo ya Milenia –MDGs) zinataka nchi zote duniani kupunguza idadi ya watu maskini wanaopata dola moja kwa siku.

  “Hata hapa ndani tulipo, hebu kwa mfano chukua Sh 2,000 umpe mtu, unafikiri ataishi vipi, ataigawa na kuitumia vipi fedha kama hiyo?” alihoji.

  Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Magharibi Profesa, Kilontsi Mporogomyi (CCM), aliwashambulia baadhi ya wabunge ambao wanaisifia serikali badala ya kukaa na kuikosoa kwa kuipa changamoto.

  “Hebu wabunge tuache utani hapa ndani, hatuko hapa kuisifia serikali ni kweli tunaangalia Progress (maendeleo), lakini hata Marekani wabunge wakiingia bungeni wanaiambia serikali fanyeni hivi,” alisema na kuongeza:

  “Sasa hapa, sisi tunataka kuisifia serikali, unaisifia serikali wakati baba na mama yako wanaishi kwa umaskini wa kutisha vijijini kule? Huu ni utani!”

  Profesa Mporogomyi ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri miaka ya nyuma, alisema kuna umuhimu wa kuwekwa miundombinu imara ya kiuchumi ili kuwaondolea Watanzania umaskini.

  Kuhusu bandari, alisema ni aibu kuzungumzia suala hilo kwani zipo nchi ambazo uchumi wake unaendeshwa kwa bandari tu.

  Huku akionekana kuchukizwa na utendaji mbovu wa bandari, alishauri iwepo wizara itakayohusika na bandari kwani wizara ya sasa ya Miundombinu imeshindwa kazi.

  Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega (CCM), alisema ni vema serikali ikaangalia upya kodi katika vinywaji baridi kwani kitendo cha kupandisha kodi kitapunguza wanywaji tofauti na serikali inavyofikiria.

  “Nafikiri uamuzi huu wa serikali kupandisha kodi katika vinywaji baridi unaweza kupunguza idadi ya wanywaji, maana kama ni soda zitanywewa kwenye harusi na misiba tu au mtu akilazwa hospitali,” alifafanua.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa napata picha ya kwa nini bajeti ya maendeleo kila mara huwa ni ndogo kuliko ile ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditure). Kwa mfano bajeti ya mwaka huu inaonyesha maendeleo yamepangiwa 2.6 Trillion wakati matumizi ya kawaida yamepewa 6. something trillion!

  Dah ni kweli wafanyakazi wanahitaji chai.....lkn sio kwa extend yakupewa 19 billion chai tu.....???? hii ni chai ya aina gani wandugu...na je, fungu la allowances mbalimbali litakuwa limekaaje?

  Wabunge wetu if they mean business wahakikishe bajeti wanaichambua vizuri na kwa umakini kujua in and out ya kila kitu!
   
 3. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hivi hawa wanaotusaidia wanajuwa kwamba bil 19 zimetengwa kwa ajili ya chai?
   
 4. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani serikali yetu haiko serious vya kutosha. Kwani hiyo chai ina manufaa gani kwa ujenzi wa Taifa? Kwani kuna tathmini gani inayoonyesha kuwa wasipokunywa chai utekelezaji wa majukumu yao utapungua? Kwanini kama wana njaa ya chai kiasi hicho wasibebe chupa za chai kutoka majumbani kwao? Hivi wanajua kuwa kuna watu hawajui hata watakula nini kwa siku wakati wao wakijimiminia chai walizowakata kodi?

  Nadhani umefika wakati kuweka misingi ya matumizi ya pesa za umma. Haiwezekani kuwa walipa kodi waambiwe barabara hazijajengwa, eti kwasababu billioni zaidi ya 50 zilitumika kutengenezea watu chai maofisini. Billioni hizo kwanini zisitumike kununulia mitambo ya umeme, kujengea barabara, kulipa walimu (shule na vyuo) mishahara, kuimarisha jeshi la polisi (naamini kuwa bajeti ya Polisi haifikii hii ya chai na safari), kuweka vifaa vizuri zaidi mashuleni na hata kujenga kiwanda kimoja tu cha saruji, mbolea au zana za kilimo?

  Wanajipongeza kwa kipi walichokifanya vizuri? Hivi kweli tunajua tunachokifanya? Mimi huwa najisikia kupata kichaa kwa jinsi serikali hii inavyofanya maamuzi yake. Chai kweli? Duh.
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jamani, tuandamane! Hii imevuka mpaka! Yani pesa yote hiyo katika chai kwa mwaka mzima? Does it really add up? Sidhani kama hii hela inaenda huko. Hela zinamegwa ki-design hapa. This is not accountability....ni wizi!!!
  Alafu na wabunge nao wasidhani tumesahau ya kwao pia!
   
 6. Marlenevdc

  Marlenevdc Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi maji ya kutengenezea chai zote hizo wanatoa wapi!?! Ikiwa chai inanywewa kwa milioni 1,5 kila siku inakuwaje wakati wa mgao? Wanapika kwa kuni? Na kama hawanywi siku kama hizo (za mgao) na J2, ina maana zinazobaki wanahamishia kwenye lunch?
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  duuuh hiii kiboko.bil 19 ya chai na vitafunwa? inamana hizi wizara zote wafanyakazi wao hawawezi kutumia sehemu ya mshahara wao kunywa chai hio hili kuweza kuokoa hio bil 19? ama kweli tanzania ina viongozi mbumbu.jamaa hawana huruma kabisa na nchi hii na nakubaliana na huyo mbunge wa cuf kwamba serikali ni kama mamba tu.
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  labda tuwaombe viongozi wadini wawapigie kelel tena labda watabadilisha mawazo tena.
   
Loading...