Wabunge wahoji: Kwanini Mafisadi Tanzania Hawashughulikiwi?

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
218
Wabunge kadhaa, akiwemo Mbunge wa Lindi Mjini (CUF) Mh. Salim Barwany, wameihoji Serikali leo Bungeni ni kwanini haiwashughulikii mafisadi Tanzania wakati wengi wao wanajulikana?

Mh. Barwany alitoa changamoto kuwa anavyojua yeye Serikali inao uwezo wa kufanya hivyo ila anajiuliza ni nini kinachofanya iwe na kigugumizi? Alisema ni kwanini Serikali imegeuka kama vile "mbuzi anayepigiwa gitaa"?

Akawachekesha wabunge wenzake kwamba ukitaka kujua nguvu ya mlevi mwaga pombe yake--akimaanisha ukitaka kujua nguvu ya Serikali-tangaza maandamano ya nchi nzima!!
 
Binafsi nadhani serikali yenyewe haijaona tatizo kwa kuwa yale ambayo tunayaita ufisadi yanaonekana ni utaratibu wa kawaida wa maisha ya watendaji wetu. Hata malalamiko ya wananchi ambayo ni ya msingi sana kama huduma za jamii kama elimu na afya yanapofikishwa huenda yanachukuliwa kana kwamba wananchi siku hizi wanataka starehe kwa kudai "extraordinary social services"
 
Hao mafisadi ndio wauza pembe za Ndovu nani awaseme wakati wameiba kukaa madarakani?
 
Serikali iliyo madarakani haiwezi kuwashughulikia mafisadi kwani ni mafisadi hao hao walioweka hii serikali madarakani. Baba mwenye madhambi hawezi kupata nguvu za kuwakemea watoto wake wafanyapo dhambi kwani anajua watoto wake wanajua madhambi yake.
 
Viongozi waliomo serikalini aslimia 90% ni mafisadi,hivyo inakuwa vigumu kuwakamata mafisadi funika kombe mwanahalamu apite.
 
Bila chadema kuongoza hii nchi tusitegemee maendeleo tukingali tuko chini ya uongozi haramu wa CCM.
 
kwa serikari ya kifisadi kama hii sitegemei mafisadi kushughulikiwa
 
KANGI ameshauri pinda na Gasia watimuliwe.je akitimuliwa watu watapinga kama zzk
 
Serikali yeyote ya kifisadi inatakaleza sheria zake kibaguzi; kwanza inakuwa na sheria moja lakini inatumika kufuatana na nafasi ya mhusika katika jamii!! Nitatoa mfano wa sheria ya kubaka; kosa hili linajulikana kuwa ni la jinai lakini Juma Kapuya mbunge hata baada ya ushahidi wa kuridhisha lakini bado yuko huru wakati wengine waliotenda kosa kama hilo la kubaka wanatumikia kifungo!!! Serikali ya namna hiyo haina haki hata ya kuwafunga waiba kuku kwani wahalifu wengine inawafumbia macho.!!!
 
Back
Top Bottom