wabunge wahoji jeshi kumtumia j. patel kuingiza matrekta kilimokwanza;utapeli huu nani anahusika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wabunge wahoji jeshi kumtumia j. patel kuingiza matrekta kilimokwanza;utapeli huu nani anahusika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 14, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,109
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wahoji jeshi kutumika katika kilimo Kwanza [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 13 July 2011 20:48 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Hussein Issa
  KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeuponda mpango wa Kilimo Kwanza na kuitaka serikali ieleze sababu za kumtumia mtuhumiwa wa ufisadi, Jayantillal Kumar Patel, kuingiza matrekta ya mpango huo nchini.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Msemaji wa kambi hiyo, Joseph Selasini, alipokuwa akitoa maoni ya kambi kuhusu hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT), katika mwaka wa fedha wa 2011/12.

  Alisema mpango huo una hurufu ya rushwa inayolishirikisha jeshi.Selasini alihoji mantiki ya kumtumia Patel anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mabilioni ya shilingi mahakamani.Selasini alisema tatizo lingine katika mpango huo ni kuliingiza jeshi katika biashara wakati halipaswi kufanya hivyo.

  Alisema kama jeshi limeamua kujiingiza katika biashara hiyo, makamanda wake na wizara, wanapaswa kueleza kiasi cha fedha, ambazo chombo hicho imezipataka kwa kuingia katika biashara hiyo.


  Selasini ambaye pia ni Mbunge wa Rombo kupitia tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, alisema kiasi cha Sh1.23 zimetumika kuingiza matrekata hayo hapa nchini kupitia mgongo wa Patel anayekabiliwa na kesi mahakamani.Katika hatua nyingine, Selesini alisema serikali inapaswa kuwatumia wananchi wenye vipaji, kutengeneza magobori badala ya kuwakamata na kuwaadhibu.


  Alisema kugundua kitu kama hicho ni jambo jema na kwamba ni vizuri wagunduzi wakathaminiwa na kuendelezwa.Msemaji huyo wa kambi ya upinzani pia alisema kitendo cha wanajeshi kupiga wananchi bila sababu za msingi na hasa katika maeneo ya vijijni ni cha kinyama.

  Alisema wananchi wanapaswa kuheshima na kushirikishwa kama wadau wa usalama badala ya kuwatesa kwa kuwapiga.Hali kadhalika aliohoji sababu za serikali kuagiza kutoka nje ya nchi, dawa wakati jeshi lina kiwanda cha kutengeza.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...