Wabunge wagomea posho ya laki 3, wasema ni ndogo

Labda tuweke mchanganuo rahisi hapa:
-Chakula @10,000x3 = 30,000/=
-Kulala per night = 40,000/=
-Kunywa per day = 20,000/=
-Miscellaneous = 30,000/=
JUMLA KWA SIKU MOJA =120,000/=

Haya, hapo nimechukulia maximum rates kabisa, ambapo kwa mtu anayejibana sana anaweza kuishi kwa nusu ya hiyo(60,000) tena kwa vizuri kabisa.
Hivi hawa wajumbe wana akili sawa kweli?....Dawa ni kuwaambia anayeona hailipi basi milango iko wazi!

JUMLA KWA SIKU MOJA =120,000/=
Uki-import Kidosho/Changu = 30,000/=
Vinywaji vya Changu kwa siku =30,000/=
Vinywaji kuzungusha raundi = 20,000/=
Nyama Choma (Mguu mmoja) = 10,000/=
Usiku Disco/Club = Tshs 10,000/=
GRAND TOTAL = Tshs 220,000/=
 
Labda tuweke mchanganuo rahisi hapa:
-Chakula @10,000x3 = 30,000/=
-Kulala per night = 40,000/=
-Kunywa per day = 20,000/=
-Miscellaneous = 30,000/=
JUMLA KWA SIKU MOJA =120,000/=

Haya, hapo nimechukulia maximum rates kabisa, ambapo kwa mtu anayejibana sana anaweza kuishi kwa nusu ya hiyo(60,000) tena kwa vizuri kabisa.
Hivi hawa wajumbe wana akili sawa kweli?....Dawa ni kuwaambia anayeona hailipi basi milango iko wazi!
PakaJimmy kwa hii serikali yetu unadhani yupo atakayediriki? sana sana usikute walikuwa wanasubiri wa kulianzisha kusudi ionekane limetoka kwa walengwa
 
Last edited by a moderator:
kiukweli!! sasa hivi UZALENDO Hakuna! wabunge waliochaguliwa na WANANCHI wamekuwa WANYAMA Kuliko UNYAMA wenyewe!! wachoyo! wabinafsi!! wazandiki!! Kimebaki kitambo kifupi TANZANIA Itachimbika!! POSHO YOTE HIYO eti haitoshi!! MUNGU Mvumilivu lakini nae anakaribia kuwachoka!!
 
Labda tuweke mchanganuo rahisi hapa:
-Chakula @10,000x3 = 30,000/=
-Kulala per night = 40,000/=
-Kunywa per day = 20,000/=
-Miscellaneous = 30,000/=
JUMLA KWA SIKU MOJA =120,000/=

Haya, hapo nimechukulia maximum rates kabisa, ambapo kwa mtu anayejibana sana anaweza kuishi kwa nusu ya hiyo(60,000) tena kwa vizuri kabisa.
Hivi hawa wajumbe wana akili sawa kweli?....Dawa ni kuwaambia anayeona hailipi basi milango iko wazi!
Hujaweka za kuhonga mkuu,ndio maana hesabu ya 220,000/=inakataa.
 
Kwanza naomba radhi kwa heading yangu yenye mtazamo wa kidni, lakini Imani yangu inabaki kuwa Mwl Nyerere huko aliko amashatangazwa 'mtakatifu' kwa sababu ya yale aliyoamini ukiachilia mbali aliyofanya hapa duniani. Maneno haya aliyasema miaka 52 iliyopita. Penye TANU weka CCM, "Ikiwa jitihada yetu itakuwa ni jitihada ya kupunguza tofauti iliyopo kati ya wale walio juu na wale walio chini, basi hapo hatuna haja kuwa na wasiwasi sana tunapowahimiza ndgu zetu kufanya kazi kwa bidii. Kwani tutakuwa hatuwahimizi wawafanyie kazi watu walio juu, bali tutakuwa tunawaomba wajifanyie kazi wenyewe. Lakini watu wa wasipojali tofauti iliyopo baina ya hali zao na hali za watu wa chini basi kuwahimiza watu wa Tanganyika kufanya kazi ni kuwahimiza wawafanyie kazi watu wa juu. Na serikali ya TANU (CCM?). ikikubali mambo hayo, basi haitakuwa na tofauti na serikali ya mkoloni. ......... Kama nilivyosema hapo juu, kila mtu hupenda fedha nyingi na hakuna mtu yeyote tangu waziri mpaka kibarua ambaye hapendi pato lake lizidi kuongezeka kila siku. Kwa hiyo ikiwa serikali ya TANU (CCM?) itachukua hatua hatua za kuzuia tofauti iliyopo sasa kati ya kati ya watu wa juu na watu wa chini, sina shaka watu walio juu hawatpenda. Hata mimi sitapenda, kwani hata mimi nataka kuwa tajiri. Bali ni vitendo ambavyo, ingawa tunajua kuwa vitawaudhi wachache, tunayo hakika kuwa ni vya manufaa kwa ndugu zetu walio wengi". Mods iache kwa muda hii thread ili watakapo kuwa wanasaini posho, wakumbuke huu ujumbe toka kwa mtakatifu mtarajiwa.
 
Eti kuna wajumbe wa bunge la KATIBA wanadai posho ya laki 3 kwa siku haitoshi..hivi hawajui kuna watu nchi hii hawana hata mia mbili ya kununulia panadol...walipoteuliwa kabla hawaenda Dodoma walijua watalipwa kiasi gani cha posho...kama waliona ndogo kwa nini walienda huko Dom? na kama hawakujua warudi makwao wakacheze na watoto zao au wake/waume zao..eeh waondoke Dom wakafanye yao,kwan wamelazimishwa kwenda Dodoma? jamani hzo hela ni kodi za watz na wengine wana maisha magumu kweli.,kuweni wazalendo kwa nchi yenu...JIULIZENI MMEIFANYIA NINI TZ KABLA YA KUFIKIRIA MATUMBO YENU.! ONENI AIBU.!
 
Deo Meck with Catherine Kahabi and 19 others
Mh. Rais, na sisi wapiga kura wako, wananchi wa kawaida kabisa, walipa kodi na wanyonge wa nchi hii, kwa huruma zako tunakuomba nasi walau tupate hata 20000 kwa wiki maana hali yetu huku ni mbaya sana Mh. Rais.

Pia kati yetu tupo wenye uwezo wa kutunga katiba mpya kwa posho ya Tshs. 50000 kwa siku, kuliko hao wahuni ambao toka waende Dodoma hawawazi juu ya katiba mpya bali wameunga genge ovu kwa ajili ya kudai posho, inamaanisha kuwa nia yao na shauku yao ni pesa tu na sio katiba bora.

Mh. Rais nashangaa hadi sasa hao wahuni, watu wazima ambao yaonekana wamebalehe viungo vya uzazi tu na sio akili na bongo zao. Mimi ningekuwa ndie Rais ningetinga Dodoma na mmoja mmoja apite mbele ili aseme juu ya posho, ambaye anasema haitoshi angechapwa viboko na aende kwake akamuonyeshe mkewe/mmewe maana ya kuwa mzalendo, na yule ambaye yuko na mkewe huko, waliopelekana kihuni huko waonyeshane huko huko.

Natamani hilo bunge la katiba lingekuwa TARIME ili hao wasaghane na walisya wanaosema posho hazitoshi tuwaonyeshe nidhamu na uzalendo maana wangechapwa viboko na waende kulima mashamba ya vijiji. Muna Tata amanto ghayo ghaoyoka too.

NAOMBA WAHUSIKA MKITAKA KUJENGA BUNGE JIPYA MJENGE TARIME NA HUKO TUWASIKIE WANAOMBA POSHO KUBWA KUBWA. With

 
Wabunge wa bunge maalum la katiba ni vema mkatambua kuwa shughuli iliyowapeleka huko n kujadili rasimu ya katiba na si kudai nyongeza ya posho. Ni kuso kujiona nyie ni maalum sana kuliko watanzania wengine. Laki 3 ndogo, wakat ndo mshahara wa wafanyakazi wengine kwa mwezi.
 
kiukweli!! sasa hivi UZALENDO Hakuna! wabunge waliochaguliwa na WANANCHI wamekuwa WANYAMA Kuliko UNYAMA wenyewe!! wachoyo! wabinafsi!! wazandiki!! Kimebaki kitambo kifupi TANZANIA Itachimbika!! POSHO YOTE HIYO eti haitoshi!! MUNGU Mvumilivu lakini nae anakaribia kuwachoka!!

wanatafuta za kutoa takrima 2015,cha msingi ni kuwakataa tu pindi uchaguzi utakopotia nanga,huwezi kudai laki 3 kwa siku ni ndogo kwa kazi ya kutengeneza katiba ya nchi itakayosaidia watanzania wote kusonga mbele.
kwa maana hiyo basi,wanadai hiyo pesa iongezeke kwa sababu katiba si yao? yaani ni kama tumewakodi kutufanyia kazi vile.
mimi nipo tayari kuifanya kazi hiyo,nachokiomba ni serikali kunilipia daladala hadi bungeni,sitaki hotel nitalala kwa jamaa yangu UDOM,na wanipe shilingi 20000 tu ya kulinda mfuko na pesa itakayobaki naomba itumike kununulia dawa mahospitalini
 
Hawa jamaa wamenekana ni limbukeni kwa sababu unaweza kuwa na digrii za saba but your still a fool or ignorance sababu madai yao hayana msingi kwani huko walienda kufanya biashara au kwenda kutengeneza katiba ambayo inawahusu sisi na wao wa watoto wetu watakokuja huko siku za usoni. Madai ya Ipad kwamba itapunguza gharama za karatasi. Ukiona kuwa tuliowapeleka huko ni mbulula kwanza gharama ya ipad 1 ni kuanzia laki 3 na kuendelea na unaweza ukakuta baadhi yao hawajui kuzitumia. hata hivyo ikiwa na ipad karatasi lazima itumike mana kunamambo mengina lazima uprint out document gharama ya karatasi lazima. Mbunge anasema kuwa hiyo pesa laki tatu ni ya kuwalipa vibarua wakulima kuna kibarua gani tz anayelipwa laki tatu kwa siku kama wenyewe wanavyotuambiaga tukiwa tunadai maslahi kwamba kama unaona mshahara mdogo acha kazi. Nasisi tunawaambia kama wanaona hiyo pesa ni ya vibarua waache waje wengine wenye uchungu na nchi. Mabwege hawa.
 
Hapa duniani watenda haki wanapigwa vita toka enzi ya adam, mzalendo kupata hiyo nafasi ni ndoto tu
 
Ni dhahiri shahiri kuwa kwenda kwao Dodoma si kwa ajili ya Taifa (KATIBA).Wanadhihirisha ni kwa jinsi gani suala la Katiba hawalipi UZITO!!.

Lengo lao kubwa ni Ulaji tu!.Na kwa namna hii hata katiba itakayopita itakuwa kinyume na matarajio ya Watanzania walio wengi hasa "Wanaharakati".

Oooh Tanzania,tutainuka lini?.......
 
Nasikia baadhi eti wanataka IPAD kama ni Rahisi kuipata hiyo IPAD kwanini wasingekwenda nazo kule bungeni
I pad...kama mtu hajawahii kuitumia au hatumii mara kwa mara mpaka aje awe na spid ya kuitumia na bunge la katiba litakua lishaisha
 
Paul Makonda ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa.
Ni kijana Makini sana na Hodari kwa kila afanyacho huitaji kufanya kwa Kiwango cha juu, Pia ni Kijana mwenye Misimamo yake Imara na Thabiti si Mtu wakuyumbishwa yumbishwa na kununuliwa kama vijana wengi wanunuliwavyo.
Kwani amekuwa akitamka na kufanya mambo mengi sana kwa ajili ya jamii na Chama pia, hii humfanya azidi kuwa mwanasiasa Mkomavu sana.

Leo hii Peter Dafi nimezungumza nae kuhusu Posho za Wabunge wakatiba, Tuimemtafuta kwakuwa Yeye ni Mmoja kati ya wabunge wa Bunge hili na Katiba na yuko Dodoma Tangu Tarehe 14 mwezi huu wa Pili hii nikuonyesha uhodari wa Jambo alilonalo mbele yake.

KUHUSU POSHO
Makonda anasema Laki tatu ni pesa ndogo kwa Posho za Wabunge hawa wanapokuwa Dodoma, kwani matumizi ni mengi sana kulinganisha namatumizi yao wanapokuwa Dodoma, Kwani.....
1 Laki tatu(300,000) haitoshi, na mimi nasimamia hilo hadi iongezwe hii kazi ni ngumu. watu wamekuja na wanasheria wasaidizi ili kuwasaidia na kuwashauri.
2. Malipo ya dereva na Posho pia chakula
3. Nyumba za wageni Dodoma na Hotel zote zimejaa na vyumba vimepanda bei si chini ya elfu (40,000Tsh). na kuendelea....
4. Mafuta ya Gari...
5. Mtu umeacha kazi zako na familia unakaa Dodoma kwa miezi miwili(2).
6. Unasomesha watoto Ada za Shule na Matumizi ya Familia na watoto, Hapo haijaja Dharula ya watoto Kuumwa nk...

Kwa hali hii Serikali lazima ilitizame swala hili vizuri apo ndo Watu watakaa vizuri Bungeni Dodoma na kufanya kazi hii vema kwa Moyo Mmoja wa Dhati.

Alisema Makonda Jioni hii ya Leo nilipozungumza nae kwa Simu.

Leo hii magazeti mengi sana yamechapisha habari za Posho kuwa ni Nyingi nk...

unaweza isoma pia habari kama hii MTIZAMO HURU.COM

 
Back
Top Bottom