Wabunge waficha mali zao - Tume ya Maadili yawageuka, wamo pia mabalozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waficha mali zao - Tume ya Maadili yawageuka, wamo pia mabalozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]
  Mwandishi Wetu - Raia Mwema


  [​IMG]


  Baadhi ya wabunge kwenue kamati za Bunge


  Tume ya Maadili yawageuka, wamo pia mabalozi


  WABUNGE zaidi ya 30 wamevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayowataka kutoa maelezo ya mali wanazomiliki na kuwasilisha taarifa hiyo Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Raia Mwema ikidokeza kuwa, pamoja nao, wamo pia baadhi ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi mbalimbali za nje.


  Mbali na wabunge hao pamoja na baadhi ya mabalozi, wapo pia baadhi ya watumishi wa Mahakama za mwanzo nchini na madiwani. Wote hao sasa wanatakiwa kutoa utetezi wao kuhusu hatua yao ya kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995, iliyotungwa baada ya ‘kifo’ cha Azimio la Arusha mwaka la 1967 lililokuwa likibainisha kile kilichoelezwa kuwa “miiko ya uongozi.”

  Maofisa wa Sekretariati ya Maadili wamelithibitishia gazeti hili kwamba maadili wanayodaiwa kukiuka viongozi hao ni kutotii agizo la kuwasilisha tamko la maandishi katika hati rasmi kwa kuorodhesha mali au rasilimali anazomikili kila mmoja wao.


  Taarifa zaidi zinabainisha kuwa pamoja na kutakiwa Desemba 31, 2011 kuwa viongozi hao wawe wamekwishawasilisha tamko hilo, waliongezewa wiki moja zaidi hadi Januari 7, mwaka huu (2012) kukamilisha mchakato huo.


  Ally Mataula ambaye ni ofisa habari wa Sekretariati ya Maadili amelieleza gazeti hili kwamba pamoja na nyongeza ya wiki moja kwao, viongozi hawakutii agizo hilo.


  “Muda wa kisheria ulikuwa Desemba 31, mwaka jana, iliongezwa wiki moja nyingine hadi Januari 7, mwaka huu walitakiwa wawe wamekamilisha zoezi la urejeshaji wa fomu za tamko la mali. Lakini inasikitisha kusema kwamba pamoja na kuongezewa siku hizo, baadhi yao wamekuwa si watiifu” alisema Mashaula.


  Katika kuelezea hatua za awali dhidi ya viongozi hao, ofisa huyo alieleza kuwa watatakiwa kuwasilisha taarifa zao hizo za tamko la mali pamoja na maelezo ya kina juu ya kwa nini wameshindwa kutii maagizo waliyopewa kwa mujibu wa sheria.


  “Kuna sababu za kuchelewa baadhi ya viongozi wanaweza wakawa nje kimatibabu na wengine ni wakaidi, wanadharau au wengine hatuna taarifa kuhusu hali yao na inajitokeza tunapofuatilia inabainika wapo wanaoumwa au amefariki…kwa mfano vifo vya wabunge hivi karibuni,” alisema Mashaula .


  Naye Katibu wa Idara ya Viongozi wa umma katika Sekretariati hiyo, Tixon Nzunda, alisema tathimini ya urejeshaji wa fomu za tamko kwa mwaka 2011 inaonesha ongezeko kwa zaidi ya asilimia 22.5 kutoka wastani wa asilimia 60 za mwaka 2010 hadi asilimia 82.5 kwa mwaka 2011.


  “Tathimini ya urejeshaji wa tamko unaridhisha tofauti na miaka ya nyuma “alisema Nzunda na kuongeza; “Bado tunafuatilia kuhusu taarifa za mabalozi, kulingana na mazingira ya kazi zao inatuwia vigumu kupata taarifa zao kwa wakati lakini na wao watatakiwa wajieleze sababu za kuchelewa kurejesha fomu za tamko.”


  Hali kama hiyo ya viongozi kushindwa kuwasilisha tamko la mali kwa wakati liliwakumba baadhi ya viongozi, wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Miongoni mwa wabunge hao ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ambaye baada ya kuitwa kwenye Baraza la Tume ya Maadili lililokuwa likiongozwa na Jaji Damian Lubuva, alikiri kutowasilisha taarifa za mali anazomiliki na kujitetea alishindwa kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo, ambao chanzo chake ni kesi zilizokuwa zikimkabili na majukumu mengine ya kiuongozi.


  Wengine ni Mshauri wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa, Rajab Luhwavi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala. Wote pia walifikishwa mbele ya Baraza la Tume ya Maadili Aprili, mwaka jana na kujitetea.


  Kwa wakati huo Luhwavi alijitetea kuwa tangu aingie madarakani (msaidizi wa Rais) Februari 6, mwaka 2006 hajawahi kupata fomu hizo, licha ya juhudi zake za kuzifuatilia.


  Kwa upande wake, Profesa Mukandala alijitetea akidai kuwa, kila mwaka amekuwa akijaza fomu hizo na kuwasilisha kwa wakati ofisi za Tume ya Maadili.


  Kwa upande wake, Profesa Mukandala alidai tangu mwaka 2006 alipochaguliwa kuwa Makamu Mkuu wa UDSM amekuwa akijaza fomu hizo na kuziwasilisha zinakotakiwa.


  “Mwaka 2006/07/08 nimekuwa nikijaza fomu zangu na kuwasilisha kwenye mamlaka husika, mwaka 2009 maofisa wa Sekretarieti ya Maadili walifika ofisini kwangu kunihakiki, ndipo waliponiambia fomu zangu hazionekani na kunitaka nijaze upya,” alijitetea Profesa Mukandala kwa wakati huo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ilikuwaje wakati wa JK Nyerere iliwezekana na sasa hivi haiwezekani na viongozi ni walewale Mwinyi, Kikwete, Malecelela, Msuya, Mkapa yaani ni walewale lakini hakuna hata mmoja ajuaye mali zao? tunakimbilia za Mbunge wa Nzega tu ni mgeni huyo
   
 3. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama hiyo tume ingekuwa na maana yoyote, wote waliobainika kuhusika na rushwa ya rada kutoka BAE System ya Uingereza wangekuwa wamesahaulika katika nyanja za siasa za Tanzania.
  Cha ajabu wao ndio vinara wa siasa za nchi hii huku wakianzisha misemo maarufu (Vijisenti) na hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi yao pamoja na ushahidi na kurudishwa kwa pesa za ziada kwa nchi hii bado sio ushahidi wa kumtia mtu hatiani wala hata kumfungulia kesi!

  Sasa hiyo tume inafanya kazi gani, kwani hata itakapogundulika kuna mali zimepatikana bila uhalali zitakuwa na tofauti gani na vijisenti?
  Akili kichwani mwako.

  Hii ni bongo ya comedi kila idara.
   
 4. M

  MAMC Senior Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tanzania karibu kila jambo linatia hasira!!! Tazizo watu wanasubiri mabadiliko yatokee kwa wakati mmoja kila sehemu!

  Sioni hata hiyo kazi hiyo Sekretarieti wanayo ifanya! kazi kulindana!! na kutuongezea foleni tuu mabara barani na mashangingi kwa kodi zetu.

  Mana hata maelezo ya hao kina Prof, Mbowe, etc ni very weak sijui mtu kayakubali vp??
  i) ukijaza formu na kuwakilisha hau - tunzi copy ya "receipt evidence"??? ili kama wameipoteza uwape.
  ii) hao viongozi basi ni matajiri saana!! mama siamini kama mtu alijaza form mwaka jana mwaka huu atakuwa ame - pata mali nyingi sana mpaka imhitaji muda kukaa kitako na kujaza bila kuwa na msongo wa mawazo!

  Pia watu wanao takiwa jaza hizo fomu ni zaidi ya 1,200 na sijawahi sikia hata siku moja mtu kafikishwa Mahakamani au kafukuzwa kazi kwa kudanganya mali alizo taja! ina maana hii control - sheria inafanya kazi vizuri mno, au haifanyi kazi kabisa!!
   
Loading...