Wabunge, Wafanyabiashara, Baadhi ya Mawaziri, watumiwa na wauza unga kumhujumu Kitwanga na Magufuli

1974hrs

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
741
536
Wabunge wa upinzani na kumuhujumu magufuli linawezekana hili.

Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini ACT Wazalendo,Peter Msigwa mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA, Mbunge wa Mwibala Kangi Lugola na Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa kuongoza harakati. Vilevile wamo Wafanyabiashara wakubwa wa Mafuta na Sukari . Wamo pia Mawaziri wa awamu ya Tano kwenye Serikali ya Rais MAgufuli.

Vilevile kuna njama za mtandao wa madawa ya kulevya, zenye lengo la kumuonda Waziri wa mambo ya Ndani Charles Kitwanga kwa sababu amewanyima raha sana wauzaji wa Dawa za kulevya hadi wengine wamekimbilia nje ya nchi.

Hatimaye sasa rasmi taswira ya CHADEMA mpya chini ya Lowasa inavaa gamba kwa kasi baada ya kucheza ngoma wasioijuwa. Kama inavyojulikana Mh.Charles Kitwanga tokea ateuliwe kuwa Waziri wa mambo ya ndani tumeshuhudia wauza unga wakubwa kwa wadogo wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hili limekuwa pigo lililodhihiri kuwaumiza wazungu wa unga wakiwamo waliofadhili harakati za UKAWA ili kumuwezesha mamvi kuikalia ikulu.

Hii ni kutokana na umbumbu na hasa kumuhusisha Mh.Kitwanga ambaye hakuwahi kuhudumu wizara ya mambo ya ndani kipindi mkataba baina ya Lugumi na jeshi la polisi ukisainiwa na kutekelezwa.Ieleweke tu madudu ya mkataba huo yamegunduliwa na CAG na ripoti imekabidhiwa kamati ya mambo ya nje na usalama ili ijadiliwe kama sheria na kanuni za bunge zinavyotaka.

Ushauri:CHADEMA kabla ya kufanya kazi za genge la 4UM lililochini "raisi ya mioyo yenu"..mjiridhishe kwanza na sio kutumika kulenga kivuli badala ya ndege.

NB:Naunga mkono wote wanaotaka kujua ukweli wa Lugumi kwa maslahi ya taifa.

Nawasilisha.
 
Wabunge wengi bongo wanaishi kwa "imprest" za mafisadi ili kuendesha maisha,sio wa CCM wala upinzani.Nchii hii mafisadi hawana chama wako pande zote....wakwepa kodi,wavusha makontena nk..ni vyama vyote.Ili serikali ilete maendeleo ijitenganishe na wezi ndani ya bunge.
 
Wabunge wa upinzani na kumuhujumu magufuli linawezekana hili
Kwahiyo mnataka mtuaminishe kuwa Kuna watu hawakosei au kufanya mipango ya wizi? Tena kwenye awamu hii ya tano. Kama amehusika na ufisadi awajibishwe tu. Sheria ni msumeno. Eti kisa anapambana na wauza madawa, basi aonekane lulu akikosea asiwajibishwe. Piga chini wote wezi.

Kuhusu zanzibar, Suala lipo wazi. Msitake kujisafisha ili muonekane ni watu mbele za wananchi. Mliwanyima haki yao wazanzbibar kwa kubaka katiba. Leo mnarudi kwa wananchi eti watu wanampango. Acheni zenu. Nyie ccm ndo majizi makubwa
 
Hatimaye sasa rasmi taswira ya CHADEMA mpya chini ya Lowasa inavaa gamba kwa kasi baada ya kucheza ngoma wasioijuwa. Kama inavyojulikana Mh.Charles Kitwanga tokea ateuliwe kuwa Waziri wa mambo ya ndani tumeshuhudia wauza unga wakubwa kwa wadogo wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hili limekuwa pigo lililodhihiri kuwaumiza wazungu wa unga wakiwamo waliofadhili harakati za UKAWA ili kumuwezesha mamvi kuikalia ikulu.

Hii ni kutokana na umbumbu na hasa kumuhusisha Mh.Kitwanga ambaye hakuwahi kuhudumu wizara ya mambo ya ndani kipindi mkataba baina ya Lugumi na jeshi la polisi ukisainiwa na kutekelezwa.Ieleweke tu madudu ya mkataba huo yamegunduliwa na CAG na ripoti imekabidhiwa kamati ya mambo ya nje na usalama ili ijadiliwe kama sheria na kanuni za bunge zinavyotaka.

Ushauri:CHADEMA kabla ya kufanya kazi za genge la 4UM lililochini "raisi ya mioyo yenu"..mjiridhishe kwanza na sio kutumika kulenga kivuli badala ya ndege.

NB:Naunga mkono wote wanaotaka kujua ukweli wa Lugumi kwa maslahi ya taifa.

Nawasilisha.
 
Msigwa siku ya pili tu baada ya magufuli kuapishwa na kutembelea wizara ya fedha yeye kwa makusudi alipost picha ya zamani inamuonyesha anakagua daftari la mizani halafu akasema Rais anakagua maudhurio hii ni poor governance. Tangu hapo simsikilizi Msigwa
 
Hatimaye sasa rasmi taswira ya chadema mpya chini ya Luwasa inavaa gamba kwa kasi baada ya kucheza ngoma wasioijuwa.Kama inavyojulikana Mh.Charles Kitwanga tokea ateuliwe kuwa Waziri wa mambo ya ndani tumeshuhudia wauza unga wakubwa kwa wadogo wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hili limekuwa pigo lililodhihiri kuwaumiza wazungu wa unga wakiwamo waliofadhili harakati za ukawa ili kumuwezesha mamvi kuikalia ikulu.

Hii ni kutokana na umbumbu na hasa kumuhusisha Mh.Kitwanga ambaye hakuwahi kuhudumu wizara ya mambo ya ndani kipindi mkataba baina ya Lugumi na jeshi la polisi ukisainiwa na kutekelezwa.Ieleweke tu madudu ya mkataba huo yamegunduliwa na CAG na ripoti imekabidhiwa kamati ya mambo ya nje na usalama ili ijadiliwe kama sheria na kanuni za bunge zinavyotaka.

Ushauri:Chadema kabla ya kufanya kazi za genge la 4UM lililochini "raisi ya mioyo yenu"..mjiridhishe kwanza na sio kutumika kulenga kivuli badala ya ndege.

NB:Naunga mkono wote wanaotaka kujua ukweli wa Lugumi kwa maslahi ya taifa.

Nawasilisha.

Acheni porojo. Kitwanga atuambie juu ya uhusika wa Infosys kwenye ufisadi wa pesa za umma sio blaablaa za nani mchawi aliye mchongea kwa umma.
 
Acheni porojo. Kitwanga atuambie juu ya uhusika wa Infosys kwenye ufisadi wa pesa za umma sio blaablaa za nani mchawi aliye mchongea kwa umma.
Mara Lugumi,mara Infosys...hamna msimamo...hadi majambazi yamejaa humu JF!
 
Kama ni kweli haipendezi Na sipendelei kabisa

Kama ni uongo ajiandae kukabiliana nae Na kuburazana mahakamani mana list ya watu aliowataja hao mm kazi ipo

Lakini tusisahau Na wale wezi wa pesa za LUGUMI
 
Hivi chadema Na mambo ya PAC wapi Na wapi waliomwandama huyo bosi wako ni PAC mkiona mambo yanawachachia mnasema chadema ccm ni Ile Ile mafisadi nyinyi wezi nyinyi watumbua majipu nyinyi wasifiaji nyinyi awamu ya nne mliipongeza nyinyi Na sasa mnaitukana nyinyi
 
Mpuuzi akiongea upuuzi against watu wenye mtizamo tofauti na serikali ni mtu mwema,ila mtu mwema akiongea kasoro kuhusu serikali anakuwa mtu mbaya...huyu bwana ni mpuuzi tu na anastahili kuburuzwa mahakamani kwa kosa la kuleta mifarakano kwenye jamii!

Hakuna sheria inayomhukumu mtu kwa kufuata hisia za mpuuzi mmoja,ikiwa yeye ni mwana mwema alistahili kupeleka duku duku lake mahakamani ama kwenye vyombo vinavyohusika...
 
Kuna ukweli fulani na mimi jana niliahidi kuweka humu mkakati wa mawaziri na mipango ya hujuma. Lakini video hii imekosa ukweli walipomweka Msigwa na Maalim Seifu.
 
Back
Top Bottom