Wabunge wacharuka! - Uwekezaji siyo kuuza nchi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Leo wabunge wameanza kuonesha makeke yao pale walipomcharukia mmoja wao aliyejitokeza kutetea kitendo cha Mwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Serengeti ambaye aliipiga "full stop" Kamati ya Bunge inayoongozwa na Mhe. Cheyo (UDP) ambayo ilifika huko mbugani kuangalia mambo yanavyoendelea.

Mwekezajji huyo aliwapiga wabunge full stop akidai kuwa wageni wamelala na hawataki kusumbuliwa. Wabunge hawakufurahishwa na hilo na leo Wizara husika imejaribu kutoa maelezo ambayo hayakuwaridhisha wabunge hata pale mmoja wa wabunge wakongwe (jina limenitoka) alipojaribu kuitetea serikali kuwa huyo mwekezaji amewekeza fedha nyingi sana kwa hiyo kitendo chake kinaeleweka, akiiashiria kwamba mwekezaji mwenye pesa nyingi hastahili "kusumbuliwa" na watu wadogo kama wabunge.

Lakini nyuma yake ni maneno ya Bw. Cheyo ambaye alinung'unika kuwa mtindo huu usipokoma basi kila Rais akitoka madarakani atakuwa anaandamwa na kashfa. Kuna tetesi ambazo zinadai kuna kauhisiano ka aina fulani kenye maslahi kati ya huyo mwekezaji na Rais kiasi kwamba yeye kama vile Sinclair anapata kiburi.

Wabunge wengi waliozungumza walionesha kukasirishwa na mwelekeo huo wa mawazo (kuwa wawekezaji wana special status) na Dr. Slaa alidai wazi kuwa hakuna bei katika hadhi na utu wetu na mwekezaji yeyote asijione kuwa kwa vile amewekeza mabilioni basi ana ka ujiko ka aina fulani hadi kuweza kuwapiga stop wawakilishi wa watu.

Hii ni siku ya pili tu ya kikao cha Bunge ambacho kinatarajiwa kuchukua karibu miezi miwili....
 
Masikini sijui Tanzania yetu imekuwaje? Hapa nahisi Mbuga imeisha chukuliwa. Yaani hata wabunge wanakimbizwa. Tumeisha uzwa tu.
 
Naona sasa wabunge wa upinzani watakosa mabomu ya kulipua bungeni.
Hongera ccm kwa kazi nzuri.
 
Ari mpya kazi za wizi mwelekeo wa kumalizia kuuza Nchi , masikini ngojen kura na vikofia , Wabunge teteeni Serikali mwisho wa mwaka mnachukua 20m .Hii inatisha sana sana .Yaani wabunge wanazuiliwa na mzungu aliyejenga mbugani ? No wonder ana jeshi lake mwenyewe na wakazi wa jirani wanajua adha na mambo makubwa yanayo wapata wakisogelea mpaka ama kuingia katika Nchi ya huyo mwekezaji aliyo pewa na CCM.
 
LUNYUNGU unatakiwa uelewe kuwa CCM imeweka miongozo/sera lakini wako baadhi ya viongozi wanakiuka maelekezo ya uongozi .
Aidha kwa bahati mbaya au kwa kutumwa ama kwa maksudi kwani watendaji wakuu wa serikari siyo wote CCM. Hao wanaofanya kazi ya kuandaa mikataba ni wasomi wetu tunaowatuma kufanya kazi kwa hiyo miongoni mwao wamo CCM CUF CHADEMA PONA n.k Hivyo wanaweza kabisa wakafanya kazi aidha kwa kuihujumu serikali ama kwa maksudi au kwa maslahi binafsi ili serikali ionekane haifanyi kazi zake vizuri.
 
Masikini sijui Tanzania yetu imekuwaje? Hapa nahisi Mbuga imeisha chukuliwa. Yaani hata wabunge wanakimbizwa. Tumeisha uzwa tu.

Kakindomaster,
Wewe endelea kuhisi tu. Mimi nina ndugu kule wananipa data kuwa mbuga zimeshachukuliwa. Kuna mahali nimesema mzalendo anafukuzwa na "walinzi" wa mwekezaji katika mbuga zetu wenyewe za Serengeti. Si umeona wabunge walipigwa stop eti wageni wa mwekezaji wamepumzika?
 
Naona sasa wabunge wa upinzani watakosa mabomu ya kulipua bungeni.
Hongera ccm kwa kazi nzuri.

Masaka,
Kama unafikiri wapinzani wamekosa mabomu ya kuripua bungeni nakushauri---stay tuned. CCM yako ni bomu.
 
Kakindomaster,
Wewe endelea kuhisi tu. Mimi nina ndugu kule wananipa data kuwa mbuga zimeshachukuliwa. Kuna mahali nimesema mzalendo anafukuzwa na "walinzi" wa mwekezaji katika mbuga zetu wenyewe za Serengeti. Si umeona wabunge walipigwa stop eti wageni wa mwekezaji wamepumzika?

Mkuu kama hiko hivyo basi inatisha. Tunapoelekea kwa kweli hakujulikani. Hili ni balaa. Watu tunakuja kutawaliwa ukubwani? Enzi hizi wakati tuna akiri zetu?
 
Kakindomaster,
Wewe endelea kuhisi tu. Mimi nina ndugu kule wananipa data kuwa mbuga zimeshachukuliwa. Kuna mahali nimesema mzalendo anafukuzwa na "walinzi" wa mwekezaji katika mbuga zetu wenyewe za Serengeti. Si umeona wabunge walipigwa stop eti wageni wa mwekezaji wamepumzika?

Hawa wabunge kwa nini hawakutumia power zao?...ndio maana nasema sisi watanaznia ni makondoo imagine wangekuwa wabunge wa kenya....mnakumbuka issue ya Artur Brothers huko Kenya miaka ya 2006 ni wananchi walifanya jamaa wakawa deported.

Ndio maana majirani zetu hutuita sisi ni WASWAHILI (filimbi nyingi tu)
 
LUNYUNGU unatakiwa uelewe kuwa CCM imeweka miongozo/sera lakini wako baadhi ya viongozi wanakiuka maelekezo ya uongozi .
Aidha kwa bahati mbaya au kwa kutumwa ama kwa maksudi kwani watendaji wakuu wa serikari siyo wote CCM. Hao wanaofanya kazi ya kuandaa mikataba ni wasomi wetu tunaowatuma kufanya kazi kwa hiyo miongoni mwao wamo CCM CUF CHADEMA PONA n.k Hivyo wanaweza kabisa wakafanya kazi aidha kwa kuihujumu serikali ama kwa maksudi au kwa maslahi binafsi ili serikali ionekane haifanyi kazi zake vizuri.

Ipole
Umesoma bandiko langu hukulielewa kabisa naomba rudia kusoma then kasome maneno ya Cheyo kama ulivyo shauriwa .Ipole watendaji wasio kuwa wana Siasa kwa Nchi kama Tanzana lazima wasikie maneno nahata kufanya matakwa ya wana siasa .Lini utaweza kusema JK kasimama kama Rais na si kama mwenyekiti wa CCM ? Ukijibu hili nitakupa maelezo zaidi .Siasa mpaka michezoni hata kwenye starehe CCM inataka kufika na kusema imeleta starehe leo unasemaje ? Wataalam wanafanya kazi kwenye serikali ipi ? Ya Chapa kipi ? Je wanafuata miongozo yao ?
 
Mutu akishawekeza ni private matter ,hamuwezi kwa kuwa ni wabunge tu mtoke na makoti yenu hata hayajapigwa pasi mtokako mkaingilie sehemu ambayo mtu amewekeza kwa fedha yake ,kuna kitu ni private na kama hiyo ni hoteli basi muwekezaji atakuwa yupo katika mstari na pengine hata nyie mnaotaka kwenda huko akiwemo Raisi hamtoweza kwenda bila ya mipango maalumu,kwani jukumu la usalama na amani ni la huyo muwekezaji ,mpeni taarifa mnaedna saa ngapi,mtakuwepo huko kwa muda gani ,je mtataka muandaliwe chakula mtalipa ,mtalipiwa au muandaliwe free.
Haiwezekani kabisa na si sheria na mnaweza kuitia serikali hasara ikiwa muwekazaji atakuwa na wanasheria wajanja ambao uzembe kama huo uliofanywa na kina Cheo na wenzake kujipeleka kichwa kichwa wanaweza wakautumia na kuomba walipwe fidia.
Katika suite kama hizi ambazo zinakuwa well secured si sehemu za kwenda tu kwa kuwa wewe au nyinyi ni wabunge mukusanyane huko eti mnaenda kuangalia shughuli zinaendeleaji ,hizi si shughuli zenu mmeshakatiwa chenu kaeni pembeni mnataka kwenda pelekeni taarifa msubiri majibu yaani mlifikiri mnaenda kutembelea soko la kariakoo ,hivi atoke mlala hoi na kulekea kwenye jengo la bunge mtamruhusu ? maana hao wabunge amewachagua yeye na wanamuwakilisha yeye na kinachojadiliwa hapo ni kwa ajili yake ,hivi atapata ruhusa ya kuingia ndani na kuangalia shughuli za bunge na wabunge wanavyojadiliana.
Nafikiri hawa wabunge wanahitaji elimu juu ya nini maana uwekezaji naamini kabisa hata Raisi hawezi kwenda hapo bila ya taarifa seuze hawa wabunge masikini za Mungu wanaotoka vijijini hawakuelewa kama kuna mipaka ya kazi zao na sio kuenda popote tu kwa kuwa yeye ni mbunge ,haiwezekani hilo wamefanya ni kosa,na nyie mnaolalamika kuwa wazalendo wanatimuliwa ni lazima watimuliwe kwani hilo eneo limeshakodishwa sasa wao wadai feza inayopatikana huko,mikataba ilitiwa saini huko , wenyewe wanasema na kuandika ,NO TRACE PASSING. yaani mtu akishaweka kibao hicho basi ana haki hata ya kukupiga risasi ujinga ni wako kwa nini hukuenda shule ,waelimisheni wenzenu huko vijijini sio mnakimbilia kuwekeza tu ,halafu mnataka mkate mbuga ,mbona ukikatiza kwenye kambi za jeshi unapelkwa mchura ,naona kuna elimu inahitajika.
Kuna mmoja nimemshangaa amesema kwa nini hawa wabunge hawakutumia power zao ,mbona mimi sijaziona hizo power zao toka liundwe hili Bunge la Tanzania ,nasikia wanaweza kuweka shilingi mbona sijaona na miswada mibovu inapita kila siku tusidanganyane power zao labda kwa mimi mlala hoi wanaweza wakaniitia polisi na kunifunga lakini sio hapo ,huyo mzungu yupo juu ya sheria na wangelijidai kutumia nguvu basi ungesikia jamaa anadai bilioni nyingine anaidai serikali ,serikali itabidi ilipe na fungu jingine anapewa Cheyo.
 
Hizo pesa za kuwekeza zimewekwa kwenye mifuko ya JK na serikali yake na kundi la MAFISADI, muda waja tena tutawakurupusha kama ngedere. Mark my words haitachukua hata miaka mitano.
 
Masikini sijui Tanzania yetu imekuwaje? Hapa nahisi Mbuga imeisha chukuliwa. Yaani hata wabunge wanakimbizwa. Tumeisha uzwa tu.

Sio kuhisi bali ni ukweli imeshachukuliwa angalia hata jina lake inapotangazwa ni hii hapa chini sio serengeti au bongo

paul-tudor-jones_72886911.jpg
The Paul Tudor Jones Sabora Plains Park, Grumeti Game Reserve

....the billionaire commodities trader Paul Tudor Jones embarked upon one of the most ambitious conservation projects in Africa when he leased 340,000 acres of Tanzania’s western Serengeti—along with every wildebeest, zebra, and gazelle within its borders. Since then, two lavish lodges and a tented camp, under the design and management of South Africa’s pioneering Singita tourism group, have opened in the eco-reserve, offering 54 guests 21st-century service in a sumptuous bush-chic setting.......All-inclusive rates per person begin at $850 for Sabora and Faru Faru, $1,500 for Sasakwa per person per night

Kilichobaki sisi ni kulia tu na kupiga duru UWIIIIIIIIII
 
Naona sasa wabunge wa upinzani watakosa mabomu ya kulipua bungeni.
Hongera ccm kwa kazi nzuri.

Kazi nzuri ipi? :confused::confused::confused:
Wangekuwa wanafanya kazi nzuri haya ya Wabunge kutimuliwa na 'mchukuaji' yasingetokea! Ebo!!!
 
mbuga, madini, ufukwe (walichomolewa).. but not too long msishangae hata Coco Beach mkajikuta kapewa mwekezaji.. Kwanini wasiamua kutugawia kila mtu kipande chake cha ardhi ili tujue mbele kwa mbele...
 
Nakumbuka kule nyuma kuna mtu alisema ameiweka serikali mkononi enzi ya Mwalimu Nyerere kweli hakuna rangi aliacha kuona,alishughulikiwa kwelikweli,je nini tukifanye ili turudishe heshima yetu tuliyokuwanayo?
 
Leo wabunge wameanza kuonesha makeke yao pale walipomcharukia mmoja wao aliyejitokeza kutetea kitendo cha Mwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Serengeti ambaye aliipiga "full stop" Kamati ya Bunge inayoongozwa na Mhe. Cheyo (UDP) ambayo ilifika huko mbugani kuangalia mambo yanavyoendelea.

Mwekezajji huyo aliwapiga wabunge full stop akidai kuwa wageni wamelala na hawataki kusumbuliwa. Wabunge hawakufurahishwa na hilo na leo Wizara husika imejaribu kutoa maelezo ambayo hayakuwaridhisha wabunge hata pale mmoja wa wabunge wakongwe (jina limenitoka) alipojaribu kuitetea serikali kuwa huyo mwekezaji amewekeza fedha nyingi sana kwa hiyo kitendo chake kinaeleweka, akiiashiria kwamba mwekezaji mwenye pesa nyingi hastahili "kusumbuliwa" na watu wadogo kama wabunge.

Lakini nyuma yake ni maneno ya Bw. Cheyo ambaye alinung'unika kuwa mtindo huu usipokoma basi kila Rais akitoka madarakani atakuwa anaandamwa na kashfa. Kuna tetesi ambazo zinadai kuna kauhisiano ka aina fulani kenye maslahi kati ya huyo mwekezaji na Rais kiasi kwamba yeye kama vile Sinclair anapata kiburi.

Wabunge wengi waliozungumza walionesha kukasirishwa na mwelekeo huo wa mawazo (kuwa wawekezaji wana special status) na Dr. Slaa alidai wazi kuwa hakuna bei katika hadhi na utu wetu na mwekezaji yeyote asijione kuwa kwa vile amewekeza mabilioni basi ana ka ujiko ka aina fulani hadi kuweza kuwapiga stop wawakilishi wa watu.

Hii ni siku ya pili tu ya kikao cha Bunge ambacho kinatarajiwa kuchukua karibu miezi miwili....

Wabunge ndio waliochemsha. Wamejisahau. Mbele ya raia (na mkazi halali) yeyote wao ni watu wadogo. Wamebweteka na huko kujiita waheshimiwa na kusahau kuwa wao kazi yao ni kutumikia na sio kutumikisha!

Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuingia kila mahali bila kibali cha mhusika, full stop. anayetaka kufanya hivyo kuna utaratibu wa kwenda mahakamani na kueleza bayana sababu za kutaka kuvamia eneo la mwingine. Kwenye utawala wa sheria, private property ni sacrosant. Wao wanategemea mfanya biashara aache shughuli zake zote aende kuwatetemekea hao waheshimiwa? In their dreams. Kwa mtindo huu, ndio mashirika mengi ya umma yalianguka maana badala ya kujali uendeshaji yalitanguliza kuwakirimu waheshimiwa kila wakijisikia kutembelea! Kama kweli walitaka kufanya ukaguzi katika biashara ya mwingine kwa nini wasiende incognito? wapange vyumba na kujilipia gharama zote kama wateja wengine? Wao wanataka walale bure, wanywe bure na wakiondoka wapewe vibahasha! Hii haiwezekani hata siku moja. wafanye hivi kwenye mashirika ya umma lakini si kwenye miradi ya watu binafsi.

Kwa nini hatuwasikii wakienda kukagua gesti huko ambako hakuna hata barabara? Au wenye gesti sio wawekezaji?

Hawa waheshimiwa wakati maeneo yanakuwa privatised wanakuwa kimya. Haya ndiyo matokeo ya privatisation. Tukishayauza hatuna haki tena. Ni ya mwenye mali. Kama kweli wana uchungu na nchi hii wangedai kufanya huo uchunguzi kabla ya hiyo privatisation. Wameangalia Serengeti, Ngorongoro, Lake Natron halafu leo kwenye kulamba ndio wanataka sympathy yetu? No way.

The free ride is over! No more free lunches!

Amandla!
 
Imefika mahala hata watunga sheria ( wabunge ) hawajui sheria!

Hao wageni "waliompumzika" ni stahiki yao kwani wamelipia huduma hiyo kwa mapesa kibao kutoka kwao mpaka hapa Bongo na huyo so called mwekezaji ana haki ya kulinda haki ya wateja wake kupata huduma kwa pesa zao.

Upo wapi utawala bora ikiwa mtu mwenye hadhi ya Mbunge ana vamia tu maeneo ya watu wakiwa wameji mpumzisha kisa eti yeye Mheshimiwa, mbona huko Bungeni tunaingia kwa utaratibu maalum wao wanataka kuvamia tu this is really low from waheshimiwa.
 
Back
Top Bottom