Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda inaonesha kuwa Wabunge waliotuhumiwa kwa rushwa ndani ya TANESCO hawana hatia na kumtaka Waziri wa Nishati na Madini na Katibu wake mkuu kuwaomba radhi wabunge hao.
Sote tunakumbuka kwamba wapo wabunge waliojitokeza wazi wazi na kuwashambulia wabunge waliotuhumiwa huku wakitamka kuwa wanaoushahidi wa kutosha kuwa walikula rushwa. Mmoja wa Wabunge hao ni TINDU LISSU, JOSEPH SELASINI na wengine. Katika ripoti hiyo ni JOSEPH SELASINI aliyetajwa kuwa alisema uongo huku kamati ikipendekeza apewe adhabu ya kukosa vikao 10 vya bunge, wakati huo ikishindwa kutaja hatua ya kumchukulia TINDU LISSU.
Lakini ni jambo la kushangaza kuwa Ripoti hiyo inawataka watendaji wa Serikali kuwaomba radhi Wabunge waliotuhumiwa badala ya kuanza na wabunge walichochea moto hadi kamati hiyo ikaundwa.
Lakini pia kuna jambo la kujiuliza hapa kama kweli kamati hiyo imekuja na matokeo yatakayowaridhisha watanzania na wasiamini kuwa Wabunge wanalindana, jambo ambalo linaweza kuibua mjadala hasa wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya, kwani kunaweza kuwa na haja ya kuwa na tume huru ya kuwachunguza Wabunge pale watakapotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.