Wabunge wa Znz na bunge la Jamhuri ya muungano Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Znz na bunge la Jamhuri ya muungano Tz

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by muchetz, Nov 12, 2010.

 1. m

  muchetz JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Mbunge anayetoka zanzibar anaingia kwenye bunge la jamhuri ya muungano kujadili mambo yanayo husu muungano tu? na kama ndivyo inapofika kwenye masuala ya Tanzania bara kuna mpaka gani unaowazuia kujadili au kushiriki katika masuala yasiyo kwenye muungano??
  hii huwa siielewi kabisa maana naona kuna uwezekano mkubwa wa bara kuamuliwa mambo yasiyo ya muungano na znz.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu Muchetz inaelekea una hoja ya maana lakini umeshindwa kunishawishi ebu nitajie kifungu cha katiba mbunge wa Zanzibar anapokatazwa kujadili masuala ya Tanzania bara.Tuanzie hapo mjandala utakuwa umewasaidia wengi nikiwemo mimi.
   
 3. m

  muchetz JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Kama umesoma vizuri post nimeuliza maswali na sikutoa conclusion ili lijadiliwe na kutolewa maoni!!
   
 4. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #4
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  ngongo

  Hivi ni kwanini kuna baraza la wakilishi zanzibar na hakuna baraza la wawakilishi Tanganyika?
   
 5. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si mnaspika wenu mabere marando kwanini msimuulize hili swali?
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawaulizi kwa nini hii bendera ya CUF inapepea humu JF ? :israel::israel::israel:
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama huna jibu siyo lazima ujibu utumbo....
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Crap
   
 9. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hoja yako ni ya msingi sana ila naona wachangiaji wanataka kuleta upotoshaji na malumbano bila kujibu hoja.

  Kwenye muungano wetu kuna masuala yanayohusu muungano (mfano ulinzi, mambo ya ndani, elimu ya juu, etc) na yasiyohusu muungano (mfano elimu ya msingi, ardhi, uchumi na biashara).

  Kwenye masuala ya muungano ni sahihi kabisa kwa pande zote kukutana na kuamua kwa pamoja, lakini yakija masuala ambayo hayahusu muungano nadhani hapa ndipo kuna tatizo kwani Zanzibar ina wabunge takribani 70 kwenye bunge la muungano na hawa wanaweza kuwa na maamuzi yasiyo na manufaa kwa watu wa bara kama wakitumiwa na kundi fulani, mfano kama kundi la wabunge 120 wa bara wakawa wanataka jambo lenye manufaa kwao na wakawashawishi hawa 70 wa Znz (wanaweza hata kupewa rushwa) hivyo wanakuwa 190 na hawa wanaweza kupitisha muswada au kitu chochote bungeni ingawaje kama hawa 70 wasingepiga kura hawa 120 wasingefikia ile 50% inayotakiwa kupitisha muswada au jambo
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  1 ) Unaposema bara huwa umekusudia nani ??
  2 ) Ni wapi au sehemu gani imeandikwa Tanzania bara katika katiba ya Jamhuri wa Muungano.
  3 ) Umeandika Tanzania bara ,kwenye bunge hujadili mambo ya Jamhuri wa Mungano wa Tanganyika na Zanzibar na si ya Tanzania Bara.
  4 ) Napenda ufahamu tu Mambo yote yahusuyo Tanzania yanaihusu Zanzibar lakini si yote ya Zanzibar yanaihusu Tanzania.
  Hivyo Wabunge kutoka Zanzibar wanawajibika kikamilifu kuhoji,kuchangia,kupinga au kuunga mguu jambo lolote lile ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
  Hivyo Wabunge kutoka Zanzibar hawazuiliki kuchangia jambo lolote lile na hakuna kipengele chochote kinachothubutu kuwazuia.
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nahisi bado anahusika kwa vile Tanzania bara ingelikuwa ya Tanganyika basi tungeendelea kujadili, kwani hayo hayawahusu, kama wa Tanganyika yasivyo wahusu ya Zanzibar.
   
 12. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  mkuu hii bendera mbona kama ya israel??
   
 13. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Maelezo yako hayatoshelezi; kama wanakuja kwa ajili ya mambo yahusuyo muungano tu kwanini wanaruhusiwa kujadili mambo yasiyohusu muungano? Je katika bunge lao la mapinduzi/wawakilishi wanajadili mambo yanayohusu muungano? kama wanajadili ni kwa nini hatuna wabunge wa bara wanaowakilisha huko zanzibar??
   
 14. n

  nina90 Member

  #14
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwa sababu wao ni wawakilishi wa zanzibar ktk serikali ya muungano...muungano wetu una sehemu mbili tu zanzibar na serikali ya muungano..hakuna kitu kama bara hivyo wawakilishi hujadili, kuchangia pia kutoa maamuzi ktk bunge la muungano..hii ni kutokana na katiba ilivyo kwa sasa!
   
 15. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Asante kwa maelezo mazuri, naona sasa umuhimu wa kubadilisha katiba au kuwa na serikali tatu otherwise hawa wazenj watakuwa wanatuendesha sana nakushiriki katika maamuzi mengine yasiyowahusu. Ona sasa cuf si chama cha upinzani huko zanzibar kwani wako katika serikali na wanatekeleza ilani ya ccm huko kwao, vipi huku bara ambapo serikali ya muungano inaongozwa na ccm?? haijakaa vizuri hata kidogo hii
   
 16. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Karibu ya waZanzibari 90% wanataka tuwe na serikali tatu...hata katiba ya CUF inaeleza hivyo...Tatizo hapa Tanganyika watu hawana muamko wa kisiasa. Wanao lazimisha Muungano wa serekali mbili ni Tanganyika.
   
 17. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #17
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi kama Nyerere angefufuka leo ningemuuliza sababu ya kuiua Tanganyika maana nimesoma kitabu chake cha "uongozi wetu na hatma ya nchi yetu" nilichoona ni yeye kupinga utanganyika bila sababu yoyote yenye nguvu.
   
Loading...