Wabunge wa Zimbabwe na Wa Kusini, Nani mkali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Zimbabwe na Wa Kusini, Nani mkali?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkereketwa_Huyu, Jun 25, 2012.

 1. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  Jamani naomba kuuliza jambo; hivi wabunge wa hapa kwetu Tanzania watokao kusini na wabunge wa Zimbabwe nani mkali kwa kutoa mada zisizo na akili? Kuuliza si ujinga, nimeuliza hivyo kwa sababu wiki iliyopita huko Zimbabwe kuna mbunge alitoa hoja na kutaka wanawake wa zimbabwe kuwa wachafu (kunuka vikwapa na kutojipenda, na pia wasioge mara kwa mara) ili wapunguze matamanio toka kwa wanaume na kupunguza maambukizi ya ukimwi. Hivi kuwa sop sop ndiko kunamfanya mtu apate matamanio ya kufanya ngono zembe na yule amtamaniye? Mwanadamu gani asiyejipenda, binaadamu sharti uoge, unukie vizuri jamii nayo ikuheshimu siyo kukulamikia tu kila kukicha eti fulani ananuka. Hapa kwetu miaka ya nyuma kuna mbunge wa kusini pia alitoa kali ya mwaka. Wote tunafahamu ukata wa kusini; yule mbunge badala ya kutoa hoja za wananchi wake yeye aliona bora eti aombe pingu ili kupunguza uhalifu kule kusini. Najuwa wengi mtasema kama kuna uhalifu kwa nini asiombe hizo pingu? Watu wengi wa kusini walihuzunika sana kuhusu hili na kumponda mbunge wao kwani hawauoni huo uhalifu. Si hii tu, wabunge wengi wa kusini hawaongei bungeni wao kulala tu na kutoa hoja zisizo na maana kwa jamii za kwao. Na ndiyo maana nauliza, hivi wabunge wa kusini hapa Tanzania na wa Zimbabwe nani mkali kwa kuongea utumbo?
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mkuu sina uhakika na utafiti wako kuhusu mambo mawili uliyoyasema. Kwanza kuwa wabunge wa kusini (TZ na Zimbabwe) ni watu wa kuongea utumbo! Pili, kuwa wabunge wengi wa Kusini hawaongei bungeni na kazi yao ni kulala na kutoa hoja zisizo na maana kwa jamii za kwao. Nisichokielewa mimi ni hilo neno Kusini. Nchi zote zilizo chini ya "Equator" kwa mujibu wa Jiografia niliojifunza miaka ya 68's zipo Kusini! Kwa maana hiyo, nchi nzima ya TZ ipo Kusini. Hivyo wabunge wote wa TZ wapo Kusini! Kama hiyo haitoshi, Wazungu wameipanua hiyo Kusini na kuziita nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwahiyo, usijipe moyo ukasema kwamba wabunge wako kwasababu wanatoka Mwanza, Kilimanjaro, Manyara au Tanga kwamba wapo Kaskazini na kwamba wanzungumza mantiki wakiwa Bungeni, la hasha!
   
 3. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Nonsense., ptuuuuuuuuuuuu:mod:
   
Loading...