Wabunge wa Zanzibar na Ushiriki wa Bunge la Tanganyika Keshokutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Zanzibar na Ushiriki wa Bunge la Tanganyika Keshokutwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Jun 10, 2012.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Wakuu Salaam;

  Siku ndio hivyo zimewadia na kile kikao muhimu cha kuijadili nchi yetu Tanganyika kinaanza kesho kutwa (12/06/2012) huko Bungeni ambapo bajeti kuu ya nchi na mambo mengine mbalimbali yatajadiliwa. Tutarajie nini kwenye kikao hiki? Nimejiuliza mambo kadhaa:-

  (i) Ukizingatia mambo ya aibu yaliyotokea huko Zanzibar, tuwatarajie wabunge wa Visiwani bila soni kuingia ndani ya nyumba na kula posho na mishahara kwa jasho la waTanganyika? Kama kweli hawaupendi Muungano angalau waoneshe kwa vitendo kwa kutokanyaga ardhi ya Tanganyika.

  (ii) Vinginevyo kama wabunge wa Zanzibar watashiriki vikao vya Bunge na wakiwa ndio wawakilishi halali wa wananchi ile dhana ya Uamsho kwamba waZNZ wengi hawautaki Muungano hata kufikia hatua ya kuwaamuru wabara waondoke ZNZ inakuwa na mashiko? Nategemea kauli nzito za kulaani matendo ya UAMSHO hususan kutoka kwa wabunge wa Zanzibar vinginevyo nao watakuwa wanafiki wasio na mfano. Halafu, wafumbe midomo yao pale masuala yanayoihusu Tanganyika pekee yanapojadiliwa - Wizara zisizo za Muungano zinaeleweka.

  (iii) Tutegemee nini kutoka wabunge wa Magamba? Mipasho kama kawa au? Natumaini 'hotuba' za CCM jana pale CHADEMA Square zimeonesha kwa ufupi mwelekeo wa nchi kwa mwaka ujao wa fedha - 2012/13. Ha ha ha ha! Tutegemee maumivu zaidi.
   
 2. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
Loading...