Wabunge wa zanzibar kuchangia bajeti za wizara zisizo za muungano ni halali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa zanzibar kuchangia bajeti za wizara zisizo za muungano ni halali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muangila, Jul 9, 2012.

 1. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Wana JF hivi ni halali kwa wabunge toka Zanzibar kupewa muda wa kuchangia bajeti kwa wizara zisizokuwa za muungano je hii kitu ni halali? au ndo mapungufu ya kikatiba na kwa nini hakuna wawakilishi wa Tanganyika katika baraza la wawakilishi Zanzibar.Chetu ni chetu na wao na chao chao peke yao hii imekaaje?
   
 2. M

  Mtoi Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Tatizo sio hilo tu.tujiulize pia uhalali wa wabunge wa zanzibar kuwa mawaziri kwenye wizara ambazo siyo za muungano.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Tatizo si hilo tu wizara ambazo ni za muungano kwanini Zanzibar haichamgii ?.
   
 4. m

  mkataba Senior Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wizara zote ni za muungano, hakuna ya Tanganyika, kwa hilo si kosa.
   
 5. m

  mkataba Senior Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umesema.
   
 6. m

  mkataba Senior Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jee ivi kuna wizara za muungano na zina majina yepi, mfano wizara ya afya ya Tanzania au ya Tanganyika kama vle za znz.....utata mtupu !!!!
   
 7. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Si hilo tu, Kwa nini Spika wa Muungano aongoze mijadala inayohusu mambo ya Tanganyika?

  TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),

  tumbiri@jamiiforums.com
   
 8. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Hata Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii?
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sijijui lakini nafikiri Ifike mahali
  .............. Bunge letu, kambi zote za upinzani na chama tawala, ziwe zinatoa constructive criticisms ambazo haziishii tu kwenye kucriticise bali pia kutoa solutions...Maana sasa hivi ni kama vile wanakomoana, kuonyeshana nani anawezakutoa hoja ya nguvu ya nani amechemsha, amekosea au nani anaweza kukosoa hoja na kuumbuana bila kutoa suluhu!

  Na bahati mbaya sana watanzania wengi tunashabikia mashushuo na kubaki kukenua meno na kufurahia nani kaumbuliwa leo Bungeni na nani ameumbua bila kupima alivyoumbua ametoa suhulisho gani ya hicho alichokiumbua!!
   
 10. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  unataka kuniambia hata Mama Tibaijuka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ana mamlaka kwenye ardhi ya Zanzibar?
   
 11. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  unataka kuniambia hata Mama Tibaijuka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ana mamlaka kwenye ardhi ya Zanzibar?
   
 12. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 13. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Huo ni uzembe naweza kusema hivyo la muhimu tanganyika wadai utaifa wao kwani tanzania ni tanganyika na zanzibar kwa hivyo wizara zote ni za muungano kilichokuwepo hapo ni kiini macho tu kwani hakuna tanganyika vipi wabunge wa z'bar washindwe kuchangia la kama mmechoka tokeni katika muungano
   
 14. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Zanzibar ni koloni la Tanganyika..kwa hiyo hawana maamuz yoyote
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanajamii One, hoja yako ndiyo kila mara naisisitiza humu jukwaani, tupunguze kulalamika na kulaumu tuu!, lets move a step futher tutoe na mapendekezo what should be done to put things right or to make it better!.

  Hili la wabunge wa Zanzibar kuchangia wizara zisizo za muungano ni sawa na lile la wabunge wa Zanzibar kuwa mawaziri wizara zisizo za muungano.

  Kila Mzanzibari kwanza ni Mzanzibari na kisha ni Mtanzania hivyo anazo haki zote za Mtanzania kama ulizo nazo wewe. Uzanzibari is just an added advantage!.

  Lakini sio kila Mtanzania ni Mzazibari, hivyo Watanzania ambao sio Wanzanzibari hawana haki zile zimpasazo Mzanzibar! ila Mzanzibari anazo haki zote zimpasazo Mtanzania!.

  Haki hizo ni kama haki za ndoa, kila mume ana haki kupata huduma zote za kindoa kwa mkewe na vivyo hivyo kwa mke. Ila mume atapata huduma hizo pale tuu mke atakaporidhia!, ila mke atakapo taka huduma hizo kwa mumewe, mume lazima azitimize hakuna issue ya kuridhia!.

  Vivyo hivyo kwenye masuala ya access, mke ana full access kwa chochote kwa mumewe hadi kuperusi kwenye simu yako! wakati mume ana only limited access kwa mkewe kuna maeneo anakuwa restricted or not reachable ikiwemo handbag ya mkewe!.

  Kwenye muungano wetu, Tanzania ni mume na Zanzibar ni mke!. Mtanzania hana full access ya Zanzibar but only limited access kwa mambo ya muungano tuu!. Mzanzibar yeye ana full access to Tanzania kwa mambo yote yakiwemo yale ya muungano na yasiyokuwa ya muungano!.

  Kwa Kwa Mume Mtanzania, nambo yasiyokuwa ya muungano ni mambo ya Handbag ya mkewe Zanzibar au ni mambo ya Kijaluba, udi na chetezo ambayo kwa mumewe yako out of reach!.
   
Loading...