Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Mwamba wa Kaskazini

Nianze kwa kongole kwa Mbunge wangu kipenzi Halima Mdee na wenzake waliokubali kutimiza haki yao ya kikatiba leo kwa kukubali kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) kwenye Bunge la JMT.

Wabunge hao takribani 19 wa CHADEMA wameapishwa leo wakati mambo mawili yakitokea; mosi, Chama chao kikiwa kimefura wao kuapishwa (Katibu Mkuu wao Mnyika anasema hatambui wakati kina Mdee wenyewe wakikenua) lakini haya yanakuja wakati majamaa mawili ya Chama hicho yakiwa yanalelewa huko Ulaya!

Majamaa hayo Tundu Lissu na Godbless Lema yamekiuka kile wadada wa CHADEMA walichokienzi cha kufanya kazi ili wale kwa wao kwenda kukimbilia Kwenye Balozi na Mataifa ya Ulaya kulishwa bureeee kwa visingizio visivyokuwepo.

Kwa kifupi nasema Kongole kwa Mdee na wenzako, kwa kutimiza maandiko kuwa asiyefanyakazi na asile, kachapeni kazi sasa, msimamie hoja sio vioja, mtaendelea kula.
 
Kaanza hotuba kwa kumshukuru Mwenyekiti wake Freeman Aikael Mbowe

Halima akimaliza miaka hii mitano atakuwa ndio Mbunge wa Upinzani aliekuwa Mbunge kwa miaka 20 mfululizo

Nimefarijika sana huyu Binti kurudi Bungeni

Nilitangaza humu Jukwaani kumpa kura yangu jimboni Kawe dhidi ya Josephat Gwajima wa Chama changu

Nmependa sana hotuba yake ilivyokuwa ya Kitaifa zaidi
 
CHADEMA ni chama cha kihuni , kwa hili bila shaka chama ndio kinakufa rasmi
 
Kutokana na hali iliyojitokeza leo ya chadema kuunga mkono juhudi nami natangaza kuunga mkono juhudi kwa kuhamia ccm.

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze nimekuwa mdau mzuri wa harakati za kutafuta haki na maendeleo ya kweli kwa kushabikia upinzani.

Kitendo kilichofanywa na key leaders wa chama kutosikiliza kilio na maamuzi ya wanachama wao ni dhahiri kuwa chama cha chadema kimekufa rasmi.

Kuanzia leo sitoshabikia chadema ikiwa katika hali hii.

Kwaheri CHADEMA!
 
Utu ni kitu cha msingi sana. Shetani alipopoteza utu wake alibadilika na kuwa kitu cha kutisha. Ndio hao wenzenu sasa. Watasema kitu gani na kuvaa taswira tofauti na wabunge wa CCM?. Kuna hoja au tija gani watakayosema ikawa na mashiko?. Ama tu serikali kuifanyia kazi?. Tutegemee wao kuwa wabunge wa mahakama.
 
Utu ni kitu cha msingi sana. Shetani alipopoteza utu wake alibadilika na kuwa kitu cha kutisha. Ndio hao wenzenu sasa. Watasema kitu gani na kuvaa taswira tofauti na wabunge wa ccm?. Kuna hoja au tija gani watakayosema ikawa na mashiko?. Ama tu serikali kuifanyia kazi?. Tutegemee wao kuwa wabunge wa mahakama.
Watalipwa watapata hela, matumbo yatajaa, Ndio kuwa makini na wanasiasa...
 
Ndugu zangu,

Nimeona nitoe ushauri tu kwa mdogo wangu John Mnyika kuwa sasa anatakiwa ang'atuke kwani BAWACHA wamemzidi nguvu.

Ni dhahiri Halima Mdee ana baraka za "mwamba" Freeman Mbowe.

Kwa ufupi tu jiweke pembeni na CHADEMA.
Chadema ni chama cha kilaghai
 
Nchi hii ngumu sana.
Sijaamini mtu aliyeibiwa kura, alikamata mabox na mabegi ya kura feki leo anaamua kuwasaliti wananchi.
Nchi hii shetani ametamalaki, Watanzania hatuna mtetezi wa kweli bali wasaka tonge.
 
Ndugu zangu,

Nimeona nitoe ushauri tu kwa mdogo wangu John Mnyika kuwa sasa anatakiwa ang'atuke kwani BAWACHA wamemzidi nguvu.

Ni dhahiri Halima Mdee ana baraka za "mwamba" Freeman Mbowe.

Kwa ufupi tu jiweke pembeni na CHADEMA.
Mwamba Mbowe, mjasiriamali wa kisiasa, na dikteta, ataachaje kuchangamkia fedha ya ruzuku (wabunge wa viti maalumu hutoa 1m/- kila mwezi).
 
Watalipwa watapata hela, matumbo yatajaa, Ndio kuwa makini na wanasiasa...
Mwisho wa siku kansa za matumbo zitawala na kufa kifo cha uchungu mkubwa huku wakimtizama kuku aliyechemshwa na kujaa mafuta mezani pasipo kutamatani kumla kwa sababu ya uchungu na maumivu.
 
Kutokana na hali iliyojitokeza leo ya chadema kuunga mkono juhudi nami natangaza kuunga mkono juhudi kwa kuhamia ccm.

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze nimekuwa mdau mzuri wa harakati za kutafuta haki na maendeleo ya kweli kwa kushabikia upinzani.

Kitendo kilichofanywa na key leaders wa chama kutosikiliza kilio na maamuzi ya wanachama wao ni dhahiri kuwa chama cha chadema kimekufa rasmi.

Kuanzia leo sitoshabikia chadema ikiwa katika hali hii.
Kwaheri chadema !
Mkuu, soma hii mada yangu ndio utaelewa nini maana ya siasa za Afrika;

Sasa itakuwa mwisho kwangu kuongelea siasa maana hata hapa jf wanaweza kukuuza kwa vipande 30 vya fedha ukawapa watoto wako shida bure. Ila siku Mungu akiikumbuka tena Tanzania nitarudi humu kushangilia.
 
Back
Top Bottom