Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Viongozi na Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wameweka msimamo kuhususiana na namna bunge lilivyoendeshwa kwenye mjadala wa kupitisha miswada ya rasilimali za nchi.
Katika mapitio ya miswada hiyo iliyoletwa kwa hati ya dharura, Wabunge wa upinzani walipeleka majedwali ya marekebisho ya vifungu vya Sheria (schedule of ammendments) kwa katibu wa Bunge kwa maslahi ya nchi lakini cha kushangaza mapendekezo hayo yalikataliwa.
Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo (Julai 3) wamevaa mavazi meupe na meusi wakipinga miswada inayozungumzia usimamizi na umiliki wa rasilimali kuwasilishwa kwa hati ya dharura.
Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe amesema hatua hiyo inalenga kuonyesha msiba kwa Taifa unaoendelea kutokea katika uchumi kutokana na kukosekana kwa muda wa kutosha kuchambua na kujadili miswada hiyo.
Miswada hiyo ni ya sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti katika mikataba ya maliasili za nchi na muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusu umiliki wa maliasili.
Alipoulizwa kama kesho watavaa mavazi hayo kwa sababu hata muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017 umewasilishwa kwa hati ya dharura, Mbowe amesema kesho ni kesho.