Wabunge wa upinzani wana uwezo wa kutetea wananchi kuliko wa CCM

Oct 13, 2018
35
259
Wakati Ester Bullaya mbunge wa upinzani anapoteza Muda pamoja na Fedha kwa ajili ya kutetea maslahi ya wastaafu na watukishi nchini Waziri na Mbunge wetu wa CCM amesema hadharani kuwa wao CCM wapo kwa ajili ya matumbo yao. Haya ni matusi ya wazi wazi kwa wananchi, ni matusi kwa walipa kodi ni kejeli kwa mtu ambaye Leo au Jana amepoteza maisha kwa kukosa fedha ya kujitibu.

Hiki ni kiburi cha hali ya juu kabisa kuwahi kukiona, na ndio Tunavyotafsiriwa sisi ccm.

Inductive reasoning inatutaka ku draw conclusion from particular to general.Ndio maana nasema kama Kigwangala ni mbunge wa ccm na ni waziri wetu basi wabunge wote na mawaziri wote wanahangaikia matumbo yao sio wananchi. Kama Kigwangala anafikiria hivi PhD Holder vipi kuhusu ambao hawakufika ngazi za juu za Elimu?

Tunaenda kupigwa tena na upinzani kwa wananchi hii agenda ya mafao wanaipigania haswa kama walivyopigania ile ya Korosho na mpaka sasa Zitto ndiye Mshindi kwenye Korosho. Hapa Bulaya na wapinzani wataibuka tena kidedea.... Niliwahi kuhoji CCM inakosa watu Smart wa kudeal na agenda za wananchi.

Wanashindwa kumsaidia Rais kwa kila hali. Kungekuwepo watu Smart nyuma ya Rais wetu asingelipata upinzani huu anaoupata kwenye jamii.

Rais anafanya mambo makubwa kweli lakini wa chini yao wanahangaika na ugali wa matumbo yao. Wanashindwa kumshauri....

Huwa nashangaa CCM huwa tunashindaje wakati matatizo ya wananchi wanayopigia kelele huku mtaani hatujawahi kusimama nayo hata kidogo.

Ninashauri kila Siku kuwa badala ya polepole kuhangaika na madarasa ya Itikadi awasemee wananchi kwenye agenda zinazohit kama hizi. Wastaafu hawa ni baba na mama zetu na kwa taarifa yenu karibia kila familia hapa nchini ina Mtumishi wa Umma ndiye anayealisha na kuwavisha, ukigombana na mtumishi umegombana na karibia robo tatu ya wapiga kura.

Siku mtaruhusu mikutano ya hadhara mmtaliona hili, endeleeni kuwekeza kwa wanaotafuta ugali wa matumbo yao kama kina Mtolea na wengineo.

Inaumiza sana.... Kiongozi wa Umma lazma uchague kauli za kuwajibu watu. Wao ndio wamekupa hilo V8 na mshahara wako nk.

Ole Mushi
0712702602
 
Hajui asemacho.....
Hivi Zitto kwenye korosho ameshinda nn?
Maana sijaona alichokuwa anafanya zaidi yakuongea upuuzi ambao niwakupuuza kwa mwenye timamu kichwani.
Pensheni sio jambo lakisiasa ....Tulieni muone mwisho....
Mwacheni Ngosha aseleme....
 
Kigwangalla sijui kwanini Mungu alimponya kule Arusha.

Ni Moja ya mawaziri wasio na chembe ya utu hata kidogo tunaweza kusema ni watu ambao wako kwenye uongozi kwajili ya v8 tu ufala usiyo na kifani.

Wananchi wanateseka lenyewe halina habari linachojua kuwa lina v8 Mungu atunusuru hawa mashetani.
 
Wakati Ester Bullaya mbunge wa upinzani anapoteza Muda pamoja na Fedha kwa ajili ya kutetea maslahi ya wastaafu na watukishi nchini Waziri na Mbunge wetu wa CCM amesema hadharani kuwa wao CCM wapo kwa ajili ya matumbo yao. Haya ni matusi ya wazi wazi kwa wananchi, ni matusi kwa walipa kodi ni kejeli kwa mtu ambaye Leo au Jana amepoteza maisha kwa kukosa fedha ya kujitibu.

Hiki ni kiburi cha hali ya juu kabisa kuwahi kukiona, na ndio Tunavyotafsiriwa sisi ccm.

Inductive reasoning inatutaka ku draw conclusion from particular to general.Ndio maana nasema kama Kigwangala ni mbunge wa ccm na ni waziri wetu basi wabunge wote na mawaziri wote wanahangaikia matumbo yao sio wananchi. Kama Kigwangala anafikiria hivi PhD Holder vipi kuhusu ambao hawakufika ngazi za juu za Elimu?

Tunaenda kupigwa tena na upinzani kwa wananchi hii agenda ya mafao wanaipigania haswa kama walivyopigania ile ya Korosho na mpaka sasa Zitto ndiye Mshindi kwenye Korosho. Hapa Bulaya na wapinzani wataibuka tena kidedea.... Niliwahi kuhoji CCM inakosa watu Smart wa kudeal na agenda za wananchi.

Wanashindwa kumsaidia Rais kwa kila hali. Kungekuwepo watu Smart nyuma ya Rais wetu asingelipata upinzani huu anaoupata kwenye jamii.

Rais anafanya mambo makubwa kweli lakini wa chini yao wanahangaika na ugali wa matumbo yao. Wanashindwa kumshauri....

Huwa nashangaa CCM huwa tunashindaje wakati matatizo ya wananchi wanayopigia kelele huku mtaani hatujawahi kusimama nayo hata kidogo.

Ninashauri kila Siku kuwa badala ya polepole kuhangaika na madarasa ya Itikadi awasemee wananchi kwenye agenda zinazohit kama hizi. Wastaafu hawa ni baba na mama zetu na kwa taarifa yenu karibia kila familia hapa nchini ina Mtumishi wa Umma ndiye anayealisha na kuwavisha, ukigombana na mtumishi umegombana na karibia robo tatu ya wapiga kura.

Siku mtaruhusu mikutano ya hadhara mmtaliona hili, endeleeni kuwekeza kwa wanaotafuta ugali wa matumbo yao kama kina Mtolea na wengineo.

Inaumiza sana.... Kiongozi wa Umma lazma uchague kauli za kuwajibu watu. Wao ndio wamekupa hilo V8 na mshahara wako nk.

Ole Mushi
0712702602
Thadei Ole Mushi, Unashangaa Kwamba CCM Huwa Mnashindaje Uchaguzi? Hahaha!

Kwa Ufupi Tu Ni Kwamba Huwa Mnashinda Kwa Bao Lenu Lile Maarufu Sana!
 
Lumumba hali ni tete mwanaccm inafika mahara anaweka namba ya simu jf ili apate uteuzi!!! Na bado chuma kinawaka moto 2020, haya mawazo yako mpelekee kenge ikulu.
 
Wenyewe wanategemea polisi na wakurugenzi.Hayo mambo ya kura hayawahusu wahesabu kura na watangaza matokeo ndo wanamatter kwao.Ila mziki wa 2020 ni mbaya mno!
 
Tatizo la wengi ni ubinafsi. Hadi tatizo limguse mtu mwenyewe ndo azinduke.

Huu utawala ushaonyesha utata kitambo, lkn wakosoaji wamekuwa wachache mno, na ndo wanaumizwa kila leo kwa kisingizio kuwa wametumwa, ni wapinga maendeleo, ni wasaliti, sisi wengine kimyaa.

Watu washaokotwa kwny viroba baharini na mitoni, watu washatekwa, watu wamepotea, watu wamevunjiwa nyumba wakati kuna zuio la mahakama... Uporaji na unyang'anyi wa kura umefanywa wazi mchana kweupe huku washindi wakipigwa chini, katiba ya nchi haiheshimiwi tena, na mengine mengi, wooote kimya. Yaani hadi mtu afikiwe yy binafsi ndo apaze sauti. Wenyewe tumemlea chatu amekomaa, acha kwanza ameze vichwa tuu
 
Tatizo wewe unachokiandika hujui kina maana gani kwani kama hujui nini zzk alichangia kwenye sakata la zao la korosho basi wewe ni zaidi ya fundofundo
Hajui asemacho.....
Hivi Zitto kwenye korosho ameshinda nn?
Maana sijaona alichokuwa anafanya zaidi yakuongea upuuzi ambao niwakupuuza kwa mwenye timamu kichwani.
Pensheni sio jambo lakisiasa ....Tulieni muone mwisho....
Mwacheni Ngosha aseleme....
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom