Wabunge wa upinzani wamshangilia mbunge wa viti maalum CCM

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Mbunge wa Viti Maalum Kiteto Koshuma ‘CCM’ ambaye aliikosoa Bajeti ya Wizara hiyo akiomba ifanyiwe marekebisho.
Mbunge huyo alizungumzia kuhusu TRA kukusanya kodi kwa watu wanaotaka kufungua biashara kabla biashara yenyewe haijaanza na kusema hii inawafanya watu wachukie kulipa kodi na kuwakimbia TRA mara kwa mara

Pia mbunge huyo alihoji kuhusu milioni 50 za kila kijiji akishangaa kutoziona kwenye bajeti ya mwaka huu wakati imeainishwa kwenye ilani ya CCM na bajeti yao imefuata maelekezo ya ilani ya CCM,amedai mwaka wa bajeti 2016/2017 zilitengwa bilioni 59kwa ajili ya kutekeleza ahadi hiyo lakini kamati inaonyesha haikutolewa hata senti na kwenye bajeti ya 2017/2018 haijawekwa kabisa kwenye bajeti



Pia amesema wizara ya maji inatakiwa kuwekewa helaya kutosha ili wananchi waweze kulima maana kwa sasa kilimo hakina dira kabisa na ndio kitatoa mali ghafi kwa ajili ya viwanda, amesema kwa sasa hatuwezi kuzungumzia viwanda huku kilimokipo hoi

 
Kaonyesha maana hakisi ya ubunge kwa ushauri wa kweli kweli kwa serikali yake na chama chake.
Sijui wabunge wengine wakiwemo na wa upinzani wanaweza kuiga mfano huo?
 
Katika hali ya kushangaza mbunge wa CCM ameshangiliwa na upinzani bungeni mara baada ya kuhoji zilipo Milioni 50 ambazo katika Ilani ya Chana cha mapinduzi zilitajwa kugaiwa kwa kila kijiji nchi Tanzania...
Alipongezwa na wabunge ambao wengi wao ni kutoka upinzani
Nini maoni yako katika hili?
Mbunge wa CCM ashangiliwa na Wapinzani bungeni Dodoma Leo.
Falsafa ya siasa/kanuni inasema hivi":WASHAWISHI,wakikataa":WADANGANYE,,
 
Kumbe bado hazijatoka.
Kuna mama mjumbe kanidanganya zilishatoka.
Acha nizisubirie.
 
Back
Top Bottom