Wabunge wa upinzani wachangamane na wale wa CCM ili kuondoa mpasuko ndani ya bunge

2011996bd

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
270
95
Kwa mawazo yangu;

Ili kupata matokeo mazuri ndani ya bunge ni lazima wabunge wawe wamoja. Je, Umoja huu ndani ya Bunge utapatikanaje wakati Waheshimiwa wabunge walishaonyesha dalili za mpasuko kuanzia kwenye ukaaji wao?
Nakumbuka miaka ya nyuma nikiwa shule ya msingi walimu walijaribu kuleta umoja na ushirikiano kati ya gender zote mbili yaani me & ke kwa kutuchanganya ( yaani kwenye dawati moja wanakaa mvulana na msichana) kwa kweli system hii ilisaidia hata kupunguza kama sio kuondoa kabisa kelele darasani.

Sasa basi ili kuleta umoja huu unao tamaniwa na wengi ningeomba kama inawezekana huu utaratibu wa ukaaji( yaani wabunge wa upinzani peke yao na wabunge wa chama tawala peke yao) ibadilishwe lengo ni kuleta ushirikiano wa pande zote ili kulifikisha taifa letu pale tunapopataka.

Huo ni mtazamo wangu.
Unaruhusiwa kukosoa, kuchangia na pia kuongezea

Naomba kuwasilisha
 
Unadhani Mwta Waitara akikaa na yule mropokaji Nkamia nini kitatokea? Mtashangaa Nkamia anatema damu baada ya kula kibao cha kelbu.
Vilevile inasaidia kuona hoja za kijinga zinatokea upande gani


Ha ha ha ha yaani umenichekesha haswa
Mtu ananyuka na agenda kaam mtoto wa chekechea kweli lazima kibao cha kelbu
 
Ahsante kwa maoni yako. jaribu tena baadae labda unaweza kuja na maoni mengine
 
Back
Top Bottom