Wabunge wa upinzani ni wachawi?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,870
2,000
Huko bungeni huko wabunge wa upinzani walituambia kuna:

1. wizi wa EPA ikawa kweli na watu wakaenda jela
2. mikataba mibovu ya madini ikiwa kweli na makanikia tumeyachukua
3. wizi wa richmond ikiwa kweli na waziri Mkuu akajiuzulu
4. Escrow ikiwa kweli na wako watu wako ndani hadi leo
5. Wakwepa kodi na misamaha ya hovyo ikiwa kweli na Rais Magufuli anahangaika nayo hadi leo

Hivi wanatabiri au wanayasema yaliyopo wazi lakini yasiyosemwa na wabunge wa CCM? Bila shaka hata waliposema kuwa mswada wa sheria ya vyama vya siasa ni mbaya itakuwa kweli tena. Lakini kama ni mbaya itakuwa ni kwa maslahi ya nani?

Ni heri wabunge na wanasiasa tuwasaidie watanzania kuiboresha barabara hii ya kwenda Ikulu kwa njia ya kidemokrasia isiwe na vumbi, visiki, kona, mashimo na vilima vingi sana. Kwani ndiyo barabara kuu tunayoitegemea vizazi vyetu vyote hata vile vitakavyokuwa na akili hafifu kupitia kwenda Ikulu.

Uwadilifu waliokuwanao Rais Magufuli, Spika Ndugai na Jaji Juma leo sio huo watakaokuwa nao watakaofuata baada yao. Ni katiba na sheria nzuri tu zitakuwa tegemeo la watanzania mambo yakijakuharibika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom