Wabunge wa upinzani nchini Kenya wamezuia Mwenge kufikishwa Bungeni

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,574
29,959
15665839_1075393165904990_574938734945808766_n.jpg


Wabunge wa upinzani nchini Kenya wamezuia Mwenge kufikishwa Bungeni kutokana na kutofautiana na chama tawala kuhusu kuandaliwa kwa kikao maalum cha bunge kujadili mabadiliko ya sheria mbalimbali nchini humo.



=============================
Mvutano ulianzia hapa

MUUNGANO wa Upinzani, Cord, umeendelea kukaa ngumu kuhusiana na marekebisho yanayopendekezwa na Jubilee kwa sheria za uchaguzi.

Kinara wa muungano huo, Bw Raila Odinga, alisema jana kuwa upinzani utatumia kila mbinu kuzuia marekebisho hayo yanayopangwa kujadiliwa na Bunge kwenye kikao cha dharura leo.

Raila alitangaza msimamo wake huo alipohudhuria Tamasha za Utamaduni wa Wajaluo katika Shule ya Upili ya Homa Bay.

Jijini Nairobi, Seneta wa Siaya, James Orengo, alienda kortini kuzuia za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutumia sajili ya wapiga kura iwapo vifaa vya kielektroniki (BVR) vitafeli.

Bw Odinga alidai kuwa viongozi wa Jubilee wana njama ya kubadilisha sheria za uchaguzi ili ziwapandelee katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

“Tunataka kuwaambia kuwa mipango yao haitafaulu.
Nimeongea na Wanga (Mbunge Mwakilishi Mwanawake Homa Bay) na kumtaka abebe maji ya kutosha bungeni ikiwa watajaribu kuleta mabadiliko hayo,” akasema Bw Odinga akizungumzia kisa ambapo Bi Wanga alionekana akimwagia maji Naibu Spika, Dkt Joyce Laboso wakati wa kikao maalumu cha Bunge kujadili sheria za usalama mnamo 2014.

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, ameitisha kikao maalumu cha Bunge leo ili wabunge wajadili uwezekano wa kufanyia sheria za uchaguzi mabadiliko.
Wabunge wa Jubilee wanashinikiza mabadiliko ili daftari la wapiga kura litumiwe iwapo mfumo wa kieletroniki utakosa kufanya kazi katika uchaguzi huo wa Agosti 2017.

Jumatatu, Bw Orengo alimwambia Jaji George Odunga kuwa sheria ya uchaguzi iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2016 inatoa nafasi ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kutambua wapigakura na uwasilishaji wa matokeo.

Akiandamana na wakili Antony Oluoch, Bw Orengo aliambia korti kuwa, katika sheria ya uchaguzi, sajili ya wapigakura itakuwa ya kielektroniki ambayo ina mitambo ya kutambua alama za vidole, mikono, macho, sauti na sahihi za mtu.

“Washtakiwa wametoa zabuni ya sajili ya wapigakura ikiwa na muundo, maelezo na mambo ambayo hayaafikiani na sheria. Nia ya Cord ni kuhakikisha watu wa Kenya watakuwa na uchaguzi huru na wa haki,” akasema Bw Orengo.

Jaji Odunga alisimamisha kwa muda zabuni ya Sh2.5 bilioni ya kuchapisha karatasi za kura iliyotolewa na IEBC kwa kampuni ya Al Ghurair Co, yenye makao yake mjini Dubai.

Jaji pia aliagiza IEBC isichapisha sajili ya wapigakura na kwamba agizo lake lichapishwe katika magazeti mawili yanayosomwa kote nchini.

Aliagiza stakabadhi za kesi kuwasilishwa kortini kesho ili kesi isikilizwe Desemba 21.
 
Back
Top Bottom