chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,392
- 24,958
Huu ukiwa ni muendelezo wa kumpinga Naibu spika Tulia Ackson.
=======
Dodoma. Katika kuonyesha bado wana kinyongo na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamesusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kuwa mgeni rasmi alikuwa naibu huyo.
“ Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli ya kufuturisha na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema jana Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale, muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.
Uamuzi huo umelifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawa imani naye.
Chanzo: Mwananchi