Wabunge wa UKAWA waliodaiwa Kumdhalilisha na Kumjeruhi Katibu Tawala wa Dar

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
735
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.


February 27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.


Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.


Aidha ameongeza ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
 
Mi ccm ni midude isiyo na aibu,akili,wala mawazo.watu wote hao wangemjeruhi huyo mwizi wa mhuri wamahaka,kuahirisha uchaguzi wa umeya, bado angekua hai ! Hapo ilibidi washtakiwa wamuombe hakimu aruhusu wafanye kama alivyodai alifanyiwa,alafu ushaidi ukamilike vilivyo.alafu eti Mmbando,chaga la wapi zoba kiasi hiki ? Tena mwanamke,hesabu miaka tu,litatimia kwa mwanao au mjukuu !mambo mengine ni laana wewe mama,sio yakukurupukia tu kisa uufurahishe utawala ! Utakapokua unajutia mazao ya ulichopanda,ccm na mtukufu wake watakua hawapo !
 
Back
Top Bottom