Wabunge wa Tanzania wajue sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa. Not every aspect of state security should be clarified to politicians.

images (1).jpg

Mfano wabunge wanaowakilisha majimbo mbalimbali ndani ya jiji la Dar wanaweza kuomba kujua "Informers wa Police" wote waliopo ndani ya jiji zima kwa maana wanalipwa kupitia pesa ambazo ni kodi za watanzania.

Je, hii ni sahihi kwa waziri wa mambo ya ndani kutoa majina yao? Kuna mambo ya kutolewa taarifa na mengine ya kukatalia kutoa taarifa (sahihi). Full Stop...!!!!!

Huko Marekani magaidi waliokubali kuwa recruited na CIA na kutumika kama double agents wao kwa Al Qaeda walifutiwa mashikata na ofisi ya DPP wa Marekani na kuachiwa kwa kazi maalum kwenda nchi za waarabu kama vileQatar, Jordan na Lebanon kupeleleza viongozi waandamizi wa makundi mengine ya kigaidi. Waliokataa kutoa ushirikiano walipewa mashtaka mengine zaidi kwa maslahi ya kiulinzi ya Marekani.

Ofisi kama hizo za DPP na ile ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG) zinafanya kazi kwa ukaribu mkubwa sana na vyombo vingine vya usalama hivyo msiwalaumu wanapotimiza wajibu wao unaoweza kuwakera nyie kama vile kubambikia watu kesi au kunyima dhamana ila ni kwa maslahi ya taifa. Kwa nchi kama Marekani, kuna wakati kunyima watu dhamana (Coercion) ni muhimu ili mtuhumiwa aweze kutoa ushirikiano kwa dola.

UTANGULIZI
==========
Baada ya tukio la kigaidi la September 11 mwaka 2001, aliyekuwa director wa Central Intelligence Agency (CIA) kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa kuhusiana na masuala yahusuyo ulinzi na usalama wa taifa hilo.

Moja kati ya maswali mengi aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence Wing), FBI pamoja na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya ardhi ya marekani.

images.jpg

Director wa CIA hakutoa ufafanuzi wowote ule zaidi ya kutoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena, which means not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA ZIMA LA KUWACHUKUA MATEKA WATU WABAYA (WITH REFERENCE TO CHINA)

Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana.

Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa wachina kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Alafu kuhusiana na Police ni kwamba, hawa jamaa hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni kati ya vituo vya police na nyumba za ibada.

Police kuwa wakali sana inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa kama vile ulawiti lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police akakutana na wale jamaa wa stakishari au Oysterbay, hivyo ana ahirisha mara moja kutenda uhalifu.

ANGALIZO: Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED. NINAKARIBISHA WAKOSOAJI.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO

Wakili Mwanadamizi Slyvester Mwakitalu ni moja ya Mawakili waliokuwa chini ya DDP aliyepita na ambao walisimama kidete kutete Jamhuri kuhusu watuhumiwa kunyimwa dhamana.
Beatrice Kamugisha, mambo mengine ni ya mslahi ya Taifa zaidi mkuu. Huko Marekani magaidi waliokubali kuwa recruited na kutumika kama double agents wa Al Qaeda walifutiwa mshikata na ofisi ya DPP wa Marekani na kuachiwa kwa kazi maalum kwenda nchi kama Jordan na Lebanon kupeleleza viongozi waandamizi wa makundi mengine ya kigaidi.

Ofisi kama hizo za D.P.P na ile ya mwanasheria mkuu wa serikali - AG (Attorney General) zinafanya kazi kwa ukaribu mkubwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama kama vile Police hivyo msiwalaumu wanapotimiza wajibu wao unaoweza kuwakera nyie ila ni kwa maslahi ya taifa.

Kwa nchi kama Marekani, kuna wakati kunyima watu dhamana (Coercion) ni muhimu ili mtuhumiwa aweze kutoa ushirikiano kwa dola.
 
Mimi nawapongeza wanausalama wote kwa kazi nzito lakini iliyoleta matokeo huko Kibiti.
Nawashauri waendelee kutumia nguvu stahiki kukabiliana na wapuuzi wote wanaotaka kuvunja amani.

Nakumbuka kipindi mauaji yalipokuwa yanaendelea tuliwalaumu polisi sasa kuna amani bado tunataka kuwalaumu.
 
KAMA kuna cha kuiga kuzuia tusibague. Isije kuteka ,kutesa n.a. kuua kwa "masilahi ya usalama"n.a. ustawi wa nchi ionekane sahihi n.a. kutolewa mifano hiyo lakini "kuandamana,kukosoa n.a. kupinga" watawala inaonekana ni "uhaini" ilhali kwa hao uliowataja inaruhusiwa. Undumila kuwili n.a. unafiki!
 
Mawazo ya hovyo kabisa haya!

Yaani watu kama akina Ben Saanane hawajulikani walipo kwa takribani miezi 18 sasa; wewe unataka kuaminisha watu kwamba mambo kama hayo yanatokea kwa ajili ya usalama wa taifa?!

Mwandishi wa Mwananchi nae unaenda mwezi wa 4 sasa with unknown whereabouts; halafu unataka kuaminisha watu kwamba, hayo hayapaswi kuhojiwa kwa ajili ya usalama wa taifa!!

Kwa mfano, unaweza kueleza ni aina ipi ya security threat iliyosabishwa na mtu kama Ben Saanane kwa kuhoji PhD ya Mkuu wa nchi?!

Ikiwa Waandishi wa Habari wanaruhusiwa kwenda hadi uwanja wa vita kuripoti vita; ni hatari ipi ya kiusalama ambayo ingesababishwa na Ripota wa Mwananchi kwa kutaka kufuatilia kilichokuwa kinaendelea Kibiti?!

By the way, kila mmoja anafahamu Magaidi wakubwa kabisa waliokuwa wanahatarisha usalama wa Marekani walikuwa wanakamatwa na kupelekwa Guantanamo!

Unaweza kutueleza hapa hao wahatarishaji wakubwa wa usalama wa Tanzania wamezuiwa gereza lipi kwa miezi yote hii?!

Btw, hivi unafahamu tofauti kati ya kulinda taarifa za siri za kiusalama (classified info) na kuficha maovu yaliyofanywa na watu walio kwenye system?

All in all, yote yana mwisho haya na endeleeni kutetea udhalimu kwavile hayajawakuta!

Na uzuri ni kwamba, majority ya watetezi wa udhalimu unaoendelea wala hampo kwenye inner circle, na kwa maana nyingine; hata nyie hampo salama!!

Ikiwa hata Nape ameshawahi kutolewa bastola hadharani; seuze nyie ambao wengine hata kula yenu ni shida!!

Wengine mkikesha kuangalia filamu na tathimlia za kivita na kijasusi kutoka Hollywood, mnadhani tayari ndo mmeshakuwa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kijeshi na kijasusi!
 
UTANGULIZI
=======
Baada ya tukio la September 11 mwaka 2001, aliyekiwa director wa CIA kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa na bunge.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence) na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya marekani. CIA director alitoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena. Not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA LA KUCHUKUA WATU MATEKA WITH REFERENCE TO CHINA.
=============
Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana. Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa watanzania kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Police hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni vituo vya police na nyumba za ibada. Police kuwa wakali inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police hivyo ana ahirisha kutenda uhalifu.

Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED.

KIJANA KUWA MZALENDO, PENDA TANZANIA.

Hivi swala la watu kupotea na kuuwawa ni classfied!? Tunaongea hivyo labda kwa sababu wale walopatwa na maafa hayo si ndugu zako. Lakini ingekuwa ni wapendwa wako sidhani kama ungeliona classfied.
 
Ukiwa unakula na kushiba mara nyingi akili huwa zinahama. Hata NAPE alikuwa na mawzo haya. Subiri zamu yako...........
 
Naona pori la mauaji umelipa jina jipya la "classified" mkuu polisi wa Tanzania huwezi fananisha na china ama marekani kwa uweredi na utendaji kazi.

Mara ngapi tunasikia wakiua watu wasio na hatia, kubambikia kesi ama kusababisha ulemavu kwa watuhumiwa. na badae inathibitika waathirika hawakuwa na madhara ama kosa.

Rejea sakata la zombe na mfanano wake, unapo wapa pori la kujificha ndo unawapa moyo wa kuendelea kuua
 
Mimi nawapongeza wanausalama wote kwa kazi nzito lakini iliyoleta matokeo huko Kibiti.
Nawashauri waendelee kutumia nguvu stahiki kukabiliana na wapuuzi wote wanaotaka kuvunja amani.
Nakumbuka kipindi mauaji yalipokuwa yanaendelea tuliwalaumu polisi sasa kuna amani bado tunataka kuwalaumu.
Kwahiyo kupiga watu risasi na kuwaua bila kuthibitisha kwamba wanahusika ndo amani hiyo?!

Hongera kwa kuwa mfuasi mtiifu ambayo baada ya kushindwa kupambana na rushwa imegeuka kuwa ya kufanya mauaji bila kuthibitisha hatia!

Binafsi ningejisikia aibu kuwa mfuasi kindakikindaki wa serikali "iliyochaguliwa" huku ikitekeleza hukumu zake sawa na wanavyofanya Magaidi hatari duniani!

Hata Beberu Kuu Marekani, huwa anakamata Magaidi hatari kabisa, kuwahoji na kuwapeleka Guantanamo ili mradi tu wajiridhishe ikiwa wanahusika na tuhuma tajwa!

Tena basi wanafanya haya kwa watu ambao majority wala sio raia wake!

Na hata walio raia wake; majority wala sio raia wa asili but still they wanafahamu huwezi kukamata mtu na kummiminia mvua ya risasi simply because taarifa za kiusalama zilimtilia shaka mhusika au mhusika alitajwa!!

Na ndio maana haikushangaza kuona kwamba miongoni mwa waliotajwa hawakuwa na hatia na hivyo kuachiliwa huru!

Kinyume chake leo tuna serikali ambayo mtu kutajwa tu inatosha kupewa hukumu ya kifo bila hata ya kufanya intensive investigation!!

Mungu awalaani wote wanaotetea ushenzi na udhalimu kama huu kwa sababu yoyote ile!

Wananchi wanalipa kodi ili majeshi yetu yaweze kulipwa mishahara ili hatimae watumie weledi wao kuhakikisha haki inatendeka!

Unapokuwa na majeshi yanayofanya kazi kwa staili ile ile inayofanywa na Magaidi then hapawezi kuwa na tofauti kati ya Magaidi na askari wanaolipwa ili kulinda Wananchi!!

Kwa hakika nchi inahitaji maombi!
 
Usalama wa taifa. Si kila kitu ujue. Na Sio kila anaye potea ni watu wa usalama, matapeli pia wamo. Watu wamesahau kuwa kibiti sio POLICE na usalama walikuwa wakipambana na raia. Walikuwa wakipambana wasiojulikana (kawaida)wale waliokuwa wakiwaua watu wabunge wamewasahau.
 
UTANGULIZI
=======
Baada ya tukio la September 11 mwaka 2001, aliyekiwa director wa CIA kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa na bunge.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence) na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya marekani. CIA director alitoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena. Not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA LA KUCHUKUA WATU MATEKA WITH REFERENCE TO CHINA.
=============
Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana. Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa watanzania kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Police hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni vituo vya police na nyumba za ibada. Police kuwa wakali inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police hivyo ana ahirisha kutenda uhalifu.

Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED.

KIJANA KUWA MZALENDO, PENDA TANZANIA.

Haya uliyoyaandika ndivyo biblia inavyosema au ndio maoni ya hao waliojichukulia madaraka Kwa kuiba kura na kufuta uchaguzi na kutumia vyombo vya dola kukandamiza demokrasia na Uhuru ulioandikwa kwenye katiba?
 
Usalama wa taifa. Si kila kitu ujue. Na Sio kila anaye potea ni watu wa usalama, matapeli pia wamo. Watu wamesahau kuwa kibiti sio POLICE na usalama walikuwa wakipambana na raia. Walikuwa wakipambana wasiojulikana (kawaida)wale waliokuwa wakiwaua watu wabunge wamewasahau.

Kitabu gani kimesema hayo au ni maoni ya Lumumba??
 
Back
Top Bottom