G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Wabunge wa Tanzania poleni sana!
Natanguliza pole kwa kuwa hapo bungeni mmekaa tu kama watu wanajadili huku wakiwa kwenye sherehe. Mnakaa na kupitisha bajeti, mnajadili hadi mishipa ya shingo inawatoka kisha ikienda kwa bwana mkubwa anaipanga upya!
Baada ya mwaka mnaletewa taarifa kuwa fedha za afya zilienda kukomboa ndege! Sehemu ya fedha za kilimo ilibidi zimalizie ikulu ya dharura Dodoma. Bajeti yote ya michezo ilibidi ihamishwe kubomoa jengo la Tanesco Ubungo.
Mbaya zaidi mnaletewa ripoti na Sii Ei Jiii kuwa kuna matrilioni yalitumika ila hayana taarifa yoyote na mbaya zaidi wala hayakuidhinishwa na nyie "wabunge wa sherehe"
Sisi watanzania tunatakiwa tuwazodoe kwelikweli wabunge! Tuwatukane matusi ya kila aina ili warudi na wautambue wajibu wao! Waelewe kuwa kwa umoja wao wana nguvu kuliko "BWANA YULE"
Tusipofanya hivyo kwa hakika wataendelea kukaliwa kichwani na kuacha mambo ili mradi yaende. Kwakweli huenda kwa sasa hawaujui wajibu wao! Tuwasimange hadi wautafakari upya wajibu wao.
Haya kwa mara nyingine pitisheni tena kisha ikifika kwenye meza takatifu inapangwa upya tena na kichwa kimoja huku nyie mkibakia tu hoi bin taabani. Naona na siku hizi mmehamia Jf kujificha nyuma ya kiibodi pamoja na sisi pangu pakavu. Sisi na nyie tunahemea jamvi moja la malalamiko hatimaye. Karibuni tena maana mlipasahau kwa muda.Mumegawanywa mkagawanyika haswaa.
Maajabu kwelikweli na yapo huku kwetu Tz.